Hamad Rashid: Zitto ataondoka na wengi!

Hamad Rashid: Zitto ataondoka na wengi!

Zitto anapenda kuwa mpinzani daima, ameona dalili za wazi kuwa chadema wanakabidhiwa ridhaa na wananchi kuwa chama tawala, yeye hataki kuwapata ridhaa hiyo, mwacheni.

"Kutoka na wengi" ni maneno ya shetani wacha mungu tunayafahamu, ni uzao wa shetani ndio utaambatana na baba yao.
 
Hiyo ni kauli ya Zitto ambapo gazeti limeripoti akisema watamkoma na huku Hamad Rashid akisema ataondoka na wengi.

Kichwa cha habari katika gazeti kinasomeka:
"Zitto:Watanikoma"

CHANZO:Jamboleo

My take;
Kama kweli hayo ndio matamshi ya Zitto,basi huyu dogo ni very arrogant na hapaswi kuhurumiwa hata kidogo.


Maneno ya mkosaji, na "mfa maji...."
 
Hivi hakuna namna nyingine ya kufanya siasa bila malumbano ya namna hii?

Hivi Ni kweli kuwa ni lazima kuwa na hali hii ktk kujadili masuala yanayotukabili kupata viongozi watakao tufokisha tunakotaka kwenda? Ni lazima tuwe na misimamo ya namna hii?
 
Heading ya Zitto kasema ndio mbaya, lakini Hamad Rashid kasema haina ubaya wowote kwa Zitto sababu hiyo kauli inasemwa na wengi.
Unachosema ndio nilichomanisha.

Hata hivyo, sitaki kuamini hiyo heading kama inavyosomeka katika hilo gazeti ila kama kweli Zitto katamka hivyo basi atakuwa na mapungufu makubwa.
 
Kauli za namna hii ni za kushangaza...ni sawa kwamba kapata ngoma kwa uzembe wake halafu kwa makusudi anaamua kusambaza kwa wengine ili wafe wengi...na atakaye ondoka naye atakuwa na akili ya kushikiwa...
 
Kuna member wa jf alimtahadharisha kuhusu malumbano ya vyombo vya habari na athari zake lakin zitto haambiliki
 
Watamkoma?Yani anaanzisha Chama kukomesha Chadema?kweli huyu anatumiwa,mi najua lengo la Chama chochote cha Siasa ni kuchukua dola adui yake alotakiwa awe CCM.

Zitto hata akiondoka na wasaliti wake kwenda kuanzisha chama au kwenda kujiunga chama kingine haitachukua muda,watu tutaanza kusikia pua yangu,mdomo wangu, mwenye kupigwa jicho atasika akiugulia maumivu ya jicho.

Huwezi ukatenda dhambi ya usaliti ukalipwa uzima,lazima uvune mauti.
 
Jambo leo haliaminiki.

Sidhani kama Zitto anaweza kutoa reckless statement kiasi hicho.

Labda awe amelishwa maneno.Mwanasiasa makini hawezi kujitolea kauli hiyo katika kipindi hiki

Hata kama siyo Zitto mwenyewe lakini Zitto ndiye karuhusu kupakaziwa mambo ya kipumbavu kwa upumbavu wake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom