Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,135
- 10,848
Uasi wa Hamad Rashid ndani ya CUF umepata uungwaji mkono usio wa kawaida katika vyombo vya habari Tanzania kama kwamba tukio kama hilo halijapata kutokea kwa vyama vyengine au ni mara ya mwanzo katika CUF.
Zaidi ya uungwaji mkono huo, sasa msajili wa vyama bwana Tendwa na Jaji Werema nao wameingilia kati kuonesha kutoridhishwa kwao na uamuzi madhubuti uliochukuliwa na uongozi wa CUF. Haipendezi kwa wanasheria hao kushikilia habari za mahakama ilhali viongozi wa CUF wameshasema hawakupokea amri ya mahakama.
Ukweli ambao wanasiasa na wanaJF hawapendi kuusema ni kuwa Hamad ni mtaji maalum wa kukivuruga CUF. Na kwanini iwe CUF? Ni mkakati wa kuimeza Zanzibar.Kwa upande mwengine CUF si chama cha kiislamu lakini kwa vile kimeasisiwa Zanzibar waislamu ni wengi na hii imekuwa nongwa. Katika mtazamo uliompana huu ni mwendelezo wa kuzima ushiriki wa waislamu katika siasa na hii ni vita ya kimataifa dhidi ya uislamu.