Hamad Rashid: Hakuna haja ya Serikali tatu

Hamad Rashid: Hakuna haja ya Serikali tatu

Kama 2 ziliwezekana kwanini 3 zisiwezekane??uzoefu wa serikali 2 upo wapi duniani?inakuwaje mtu anaongea kwa lengo la kufurahisha watu fulani?serikali 2 ni ulaghai wa ajabu!!nchi ndani ya nchi!!mipaka ndani ya nchi!!amiri jeshi wakuu wawili ndani ya nchi!!
Suruhisho hapa ni serikali moja

Mwambie Marekani wana serikali tatu kwa maana wana United States (serikali ya Muungano) na utitiri wa serikali aina ya Tanganyika na Zanzibar (states). Hata kule Nigeria - wana Federal State halafu serikali nyingi (usiseme majimbo maana utararuliwa hapa).
 
Watu wote wenye akili ya kuweza kupata A+ watakuja na jibu kama lako, na wale wanaoweza kujikongoja na kupata D ndio mashabiki wakuu wa serikali mbili. Wa serikali tatu ndio wamo katikati ya hizi marks mbili. Mwenye akili na aelewe tuliposimama!

Sifa za wale wa serikali tatu:
1. Awe mfuasi na mwanachama wa CHADEMA
2. Awe anatoka kaskazini
3. Awe anapenda Madaraka
 
Mwambie Marekani wana serikali tatu kwa maana wana United States (serikali ya Muungano) na utitiri wa serikali aina ya Tanganyika na Zanzibar (states). Hata kule Nigeria - wana Federal State halafu serikali nyingi (usiseme majimbo maana utararuliwa hapa).

Ainisha serikali 3 za Marekani.
 
Mwambie Marekani wana serikali tatu kwa maana wana United States (serikali ya Muungano) na utitiri wa serikali aina ya Tanganyika na Zanzibar (states). Hata kule Nigeria - wana Federal State halafu serikali nyingi (usiseme majimbo maana utararuliwa hapa).

Kama unajua anaweza kuambiwa na mtu wa humu JF, basi mwambie wewe.
 
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani

Siku ya kwanza alipokwenda kujisaidia hajakubwa alipewa uzoefu na Maalim?
 
Ni Watanganyika ndio wanaodai Tanganyika yao,yeye Mzanzibari yanamhusu nini?

Atajibu nini iwapo ataulizwa kuwa mbona nyinyi Wazanzibari mna nchi ndani ya muungano halafu hutaki Watanganyika wapate nchi yao?

Huyu anamsaidia Pengo bila ya kujijua.

Kakaa sana bara anajisikia Mtanganyika.
 
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani

Aisee! Viongozi wengi wanaongea pumba lakini Wazanzibari wamezidi!
...
Hakuulizwa uzoefu wa serikali mbili umetolewa wapi?
 
Ulitarajia mawazo gani kutoka kwa mbunge wa mahakama na pandikizi la ccm.

Hoja ya serikali mbili lazima itapitishwa na wajumbe zaidi ya robo tatu, sijui CHADEMA mtasimama wapi kupiga mavuvuzela yenu.
 
Hawa watu ni wehu, kila siku malalamiko yalikuwa Tanganyika imeifanya Zanzibar kuwa koloni lake sasa fursa ya kujitoa kwenye hilo koloni imepatikana , wanaanza mara ohh hakuna haja ya serikali tatu......wanaangaliaa Ubunge wao tu na wala sio masilahi ya Zanzibar hawa .......

Aisee!
Si alikua kambi ya upinzani huyu?
 
Yeye kama mtu alierubuniwa kuigawa CUF sasa anataka kulipa fadhira miaka yote hamsini kero hizo zimeshindikana leo ndo zitaisha !!? Kwa kuwa yeye ni mzanzibar ningempongeza kama angependekeza seikali moja kuliko kuja na porojo zake hizo huyu mwanzilishi wa ADC.

Ningeshauri serikali, kabla ya wajumbe wa bunge la katiba kuanza mchakato, wangewapeka hospitali kuwapima akili!
 
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani

Kero kuu ya muungano ni kutokuwepo kwa Tanganyika na serekali yake hiyo kero ikitatuliwa muungano utaendelea kuwa hai.Ila wazanzibar hawawezi kuiona hiyo kero kwa sababu maisha yao wameyawekeza Tanganyika.Serekali ya Tanganyika ikirudi hakuna mwakirishi yeyote kutoka Zanzibara atakayeruhusiwa kuingia kwenye bunge la Tanganyika na kujadili mambo ya Tanganyika wao watasubiri kuingia kwenye mambo ya muungano tu.
 
Jana,wabunge waliketi kwa dk 25 tu,kila mbunge,akapatiwa laki 3, wakadai ni ndogo,yaa laki moja na ushee per minutes! Nadhani hili bunge,limefanya wa2 wasihoji matokeo ya form 4. Na hisi machafuko! 129,000,000,kwa dk 25! Huku madawa,madawati,hakuna! Zanzibar wamelipuwa makanisani! Raisi anahutubia leo,huenda akawaambia wakristo,uvumilivu una mwisho wake,wasitegtmee polisi kama alivyotuhasa sisi wafuasi wa magamba.
 
Wajanja wote hawawezi kuunga mkono serikali tatu kwa dakika moja.

Kwaiyo unataka kusema majority ya Watz ni wajinga! Si ndio?
Mjanja ni wewe Maccm na huyo mpu.uzi (H. Rashid) anaetapatapa?
 
Back
Top Bottom