Hamad Rashid abwagwa kortini

Hamad Rashid abwagwa kortini

Mahakama imejiridhisha kwamba, amri ya mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR na wenzake wanne haikufikishwa kwa chama kwa hivyo kikao husika kilikuwa halali.
okay.... kwa hiyo kikao kilichowafukuza kilikuwa halali meaning walifukuzwa kihalali...

Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013
kesi ya msingi kivipi tena wakati ushasema mahakama imeamua kwamba kikako kilichowafukuza kilikuwa halali, hiyo sio kesi ya msingi? Kesi ya msingi maana yake nini?
 
okay.... kwa hiyo kikao kilichowafukuza kilikuwa halali meaning walifukuzwa kihalali...

kesi ya msingi kivipi tena wakati ushasema mahakama imeamua kwamba kikako kilichowafukuza kilikuwa halali, hiyo sio kesi ya msingi? Kesi ya msingi maana yake nini?

Kesi ya msingi ni ya Hamad Rashid kupinga kufukuzwa uanachama.Hii ya sasa ilikuwa ni ya Hamad dhidi ya CUF kukaidi amri ya mahakama ya kuendesha kikao cha kumfukuza Hamad
 
nilifika jimboni kwake mwezi uliopita nikaongea na watu wa huko yaani wapiga kura wake jamaa hana ushawishi kabisa na walimkataa uchaguzi uliopita akaenda katibu wake kuwabembeleza wampe kura kwakuwa katibu huyo anaushawishi mkubwa pengine kuliko kiongozi yoyote znz walimsikiliza, hii inamaana waweza kuwa mwisho wa HR umefika..
 
kutoka mujibu wa julius mtatiro...

my take
nini hatma ya hamad rashid kisiasa maana ni wazi upepo si mzuri kwake?
Je ni wakati sasa wa cdm kufikiria kumpa nafasi mh. Rashid ili kuendelea kujijenga visiwani zanzibar baada ya kuwa na makada wa aina ya profesa safari?

Ni wazi mchango wa hamad rashid katika kuleta mageuzi nchini si wa kubeza. Aliweza kuiongoza kwa ushupavu kambi ya upinzani bungeni 2005-2010 na ikaleta matunda mazuri. Pamoja na kuhusishwa na adc (hakuna ushahidi) anaweza kupewa nafasi cdm?

Tujadili hoja, bila matusi

nadhani hamad rashid anaweza kuwa nguzo muhimu kwa chadema upande wa zanzibar kama akiamua kujiunga nacho!hakuna anaeweza kubisha namna hr anavyokubalika zanzibar hata kama hamzidi maalim seif lkn kwa cdm anaweza kuwa lulu!uzuri ni kuwa kimsimamo cdm na hr wanaelekeana hasa kuhusu hoja za msingi za muungano!kila la heri hr na cdm katika kuimarisha demokrasia na wigo mpana wa uchaguzi kwa watanzania!
 
Kesi ya msingi ni ya Hamad Rashid kupinga kufukuzwa uanachama.Hii ya sasa ilikuwa ni ya Hamad dhidi ya CUF kukaidi amri ya mahakama ya kuendesha kikao cha kumfukuza Hamad

kwa mtu mwenye chembe ya akili baada ya maamzi haya ya mahakama sioni tena HR kama atashinda itakuwa kama ya madiwani wa cadema kule Arusha nanina mshauri afute kesi hiyo kupunguza garama atakazo kuja kutozwa..
 
Ni kweli mkuu kwa hukumu hii ya mahakama Hamad Rashid akubali aibu tu awithdraw kesi yake maana hakuna dalili za kushinda hapo. Kama mahakama imeshathibitisha kikao kilichokufukuza uanachama kilikuwa ni halali basi hata maamuzi/maazimio yake yatakuwa ni halali vilevile. Hili litamkuta na David Kafulila muda si mrefu.
 
Kesi ya msingi ni ya Hamad Rashid kupinga kufukuzwa uanachama.Hii ya sasa ilikuwa ni ya Hamad dhidi ya CUF kukaidi amri ya mahakama ya kuendesha kikao cha kumfukuza Hamad
Kesi moja Hamad alipinga kufukuzwa uanachama (haijawekwa sababu).

Kesi nyingine Hamad alipinga kufukuzwa uanachama kwa sababu kikao kilichomfukuza uanachama alidai si halali maana kilikaidi mahakama.

Sasa hapo kwa nini tuseme kesi moja ni ya msingi kuliko nyingine, tena ambayo haina maelezo ndio ya msingi, kesi ya msingi maana yake nini?

Waandishi wetu wa kibongo hamtutendei haki kabisa, hamueleweki!
 
Mkuu labda wanasheria waje wasaidie.Lakini tunaposema kesi ya msingi ni kesi kuu iliyofunguliwa na mdai. Utakumbuka Hamad Rashid alifunguwa mashtaka ya kupinga kufukuzwa kwake uanachama (Kesi ya msingi hii) sasa kama ingetekelezwa Hamad Rashid angetemwa Ubunge. Alichokifanya Hamad Rashid mbali na kesi yake ya msingi ya kupinga kufukuzwa uanachama alipinga pia uhalali wa kikao kilichomfukuza maana kilikuwa na zuio la mahakama ambalo ndiyo hilo Mahakama imeliamua juzi.
 
Inna Lillahi wainna Ilaihi rajihunna.Pole sana Mh Hamad Rashid.Siku zote ukipanda UPEPO basi ujue utavuna DHORUBA. Kazi kwako.
 
Binafsi ningefurahi kama HR angejiunga na CDM, Tungekua rtumepata mshirika mzuri ktk siasa za Znb na wale waumini wa siasa za kidini ambao wamekua wakiongezeka sana ktk siku za karibvuni

Muumini wa siasa za kidini ni huyu: Mzee Edwin Mtei >> Muasisi na mlezi wa CDM.

http://1.bp.blogspot.com/-xTseBL2c_9...00/KATIBA2.png

Ya huko nyuma labda watu waliyasahau, lakini haya ya kutaka tume ya mabadiliko ya katiba iwe na uwiano wa wateuliwa kulingana na dini zao ni nini? Sio udini?

Ubunge. Alichokifanya Hamad Rashid mbali na kesi yake ya msingi ya kupinga kufukuzwa uanachama alipinga pia uhalali wa kikao kilichomfukuza maana kilikuwa na zuio la mahakama ambalo ndiyo hilo Mahakama imeliamua juzi.
Kwa hiyo ni kesi mbili tofauti, zote mbili zilipinga maamuzi ya CUF, moja ilipinga maamuzi kwa madai ya kutokuwepo uhalali wa kikao kilichofanya maamuzi, nyingine inapinga maamuzi na sababu ambazo hatujapewa. Bado sioni kwa nini moja iwe kesi ya msingi kuliko nyingine.
 
Mkuu fanya na ufuatiliaji kidogo wa issue hii huko nyuma. CUF walipanga kufanya kikao cha kamati ya maadili ambacho pamoja na mambo mengine kilikuwa na agenda ya kumfukuza Hamad Rashid. Sasa Hamad alikimbilia Mahakamani kuzuia kikao hicho (Kesi ya kwanza hii-CUF kukaidi agizo la Mahakama ambayo sasa imetupwa). Kesi ya pili ni kwamba pamoja na zuio la Mahakama (ambalo sasa limeshatupwa), CUF bado waliendelea kufanya kikao na hivyo kumfukuza Hamad Rashid uanachama, Hamad akafungua kesi nyingine kupinga kufukuzwa kwake. Kesi zinaendeshwa na jinsi ulivyozifungua,zinaweza zikawa hata tano kuhusu suala lilelile moja ni suala la kutumia Sheria kutafuta haki.
 
Nampa pole kwa kufiwa na mke mdogo. Inaonekana hawa wapemba mke mbili ndio utaratibu wao.
Pole kwa kufiwa na mke mdogo! nani humu asiejua raha ya mke mdogo? Ukimtuma maji unamuangalia mgongo! Akikuletea maji unamuangalia usoni, daah; pole sana Mkuu!
 
Naomba kujua ili twende sawa. Huyu HR ni yule alokuwa akishabikia wabunge wa CDM kufukuzwa bungeni ili yeye na wenzake waunde kambi rasmi ya upinzani bungeni, au ni mwingine huyu? na kama ni mwenyewe mbona alishahojiwa live kuhusu hatima yake baada ya kuvuliwa uanachama cuf akasema yeye si malaya wa kisiasa wa kudandiadandia vyama sababu hata ccm alitoka tu kwasababu yeye pamoja na Sharif Hamad walifukuzwa. Mimi nilimwelewa kwamba bado an mapenzi na ccm hivyo wakimrudisha kundini atavaa kijani.
 
My Take
Nini hatma ya Hamad Rashid kisiasa maana ni wazi upepo si mzuri kwake?
Je ni wakati sasa wa CDM kufikiria kumpa nafasi Mh. Rashid ili kuendelea kujijenga visiwani Zanzibar baada ya kuwa na makada wa aina ya Profesa Safari?

Ni wazi mchango wa Hamad Rashid katika kuleta mageuzi nchini si wa kubeza. Aliweza kuiongoza kwa ushupavu kambi ya upinzani bungeni 2005-2010 na ikaleta matunda mazuri. Pamoja na kuhusishwa na ADC (hakuna ushahidi) anaweza kupewa nafasi CDM?

Tujadili hoja, bila matusi[/QUOTE]
# unaogopa matusi
 
Nampa pole kwa kufiwa na mke mdogo. Inaonekana hawa wapemba mke mbili ndio utaratibu wao.
Aksante kwa ufafanuzi maana nimesikia tu kuwa huyu kaka kafiwa na mkewe nikahuzunika mno japo ni miaka mingi lakini mkewe namfahumu, hata hivo pole zimfikie kwani kifo ni kifo tuu.
 
CUF walipanga kufanya kikao cha kamati ya maadili ambacho pamoja na mambo mengine kilikuwa na agenda ya kumfukuza Hamad Rashid. Sasa Hamad alikimbilia Mahakamani kuzuia kikao hicho
Mara ya kwanza ulisema kikao kilichomfukuza uanachama ambacho Rashid alipinga uhalali wake kwa vile kulikuwa na barua ya mahakama ni Baraza Kuu. Sasa hivi unasema ni kikao cha kamati ya maadili. Maelezo yako yana matatizo.

Halafu kitu kingine, kwenye sheria huruhusiwi kufungua "kesi tano kwa kitu kile kile." Ni vitu tofauti. Ninachojaribu kuelewa ni kwa nini hiyo kesi ambayo hujatuambia msingi wa pingamizi lake kwa nini hiyo ndio uiite kesi ya msingi?

amri ya mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR
 
nilifika jimboni kwake mwezi uliopita nikaongea na watu wa huko yaani wapiga kura wake jamaa hana ushawishi kabisa na walimkataa uchaguzi uliopita akaenda katibu wake kuwabembeleza wampe kura kwakuwa katibu huyo anaushawishi mkubwa pengine kuliko kiongozi yoyote znz walimsikiliza, hii inamaana waweza kuwa mwisho wa HR umefika..

Mzee mimi niko pemba na kama umesema uliongea na wapiga kura wa jimbo la wawi kuhusu MH hamad na hawana ushawishi nae na uchaguzi ulopita aliingilia katibu mkuu ili wananchi wamchague lakini hebu niambie ni mbunge wa jimbo gani wa CUF huku pemba anamvuto? Ninavojua mimi hii hoja ya kuingilia kati katibu mkuu iko kwa wabunge wengi huku nyumbani, tatizo la wabunge wa Pemba na akiwemo Hamad ni kukaa bila ya kufanya chochote jimboni kwake na ndio maana leo hii hana la kuwambia wananchi wake vilevile ni kwa wabunge wote waliobaki wa cuf huku pemba, hata Mh. Halifa ambae ameshakaa muda mrefu bungeni kama miaka 17 tuambie amefanya nini jimboni kwake, halafu niletee jibu hapa, huyu mh hamad alikua mbunge wenu cuf tena kwa muda mrefu mpaka akawa kiongozi kambi ya upinzani lakini leo unasema hawezi kurudi jimboni kwake ni mfano tosha kwamba wabunge wenu hata hao walobakia hawana wanalolifanya ni kula kodi zetu tuu na ndo mimi kama ningelikua ninauwezo wa kuzifuta hizi nafasi za ubunge ningezifuta kwa upande wa znz.
 
Back
Top Bottom