Hamad Rashid abwagwa kortini

Hamad Rashid abwagwa kortini

Nadhani CDM inahitaji zaidi ya kuongeza watu wenye majina ya kiislamu ili kufuta/kuondoa au kupunguza dhana ya udini inayokigubika chama hicho.

Prof. Safari hajawa na impact yeyote so far
 
Aanzishe chama chake mapema!

Ooooh bora aelekee ADC
 
mwanzoni alivuruga ccm akatimuliwa, kavuruga cuf akatimuliwa, hamuoni huyu mtu ana cv yenye utata?? Kwani cdm ni jalala?

hatumtaki cdm.
Cdm si jalala la kuokota mifupa aliyoshindwa fisi amelikoroga mwenyewe na alinywe
 
WOWOWO Hivi Hamad na Mtatiro wana utafauti wowote? Labda Sura lakini si wote wako kwenye Payroll ya CCM kuuvuruga UPINZANI? TAFAKURI

Sina hakika lakini ninachofahamu kuna utofauti mkubwa sana kati ya Mtatiro na Hamad Rashid. Mimi naamini Hamad kazi aliyoifanya kuipa nguvu kambi ya upinzani 2005-2010 haiwezi kupuuzwa kwa kumpachika majina ya u payroll wa CCM.
 
Akaribishwe CDM. Na nafikili anaweza hata kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CDM. Mnasemaje wadau
 
kutoka mujibu wa julius mtatiro...



my take
nini hatma ya hamad rashid kisiasa maana ni wazi upepo si mzuri kwake?
Je ni wakati sasa wa cdm kufikiria kumpa nafasi mh. Rashid ili kuendelea kujijenga visiwani zanzibar baada ya kuwa na makada wa aina ya profesa safari?

Ni wazi mchango wa hamad rashid katika kuleta mageuzi nchini si wa kubeza. Aliweza kuiongoza kwa ushupavu kambi ya upinzani bungeni 2005-2010 na ikaleta matunda mazuri. Pamoja na kuhusishwa na adc (hakuna ushahidi) anaweza kupewa nafasi cdm?

Tujadili hoja, bila matusi


wao kivyao vyao,,cuf na ccm si bibi na bwana?nani hajui??


Pia nani kakuambia cdm ni kimbilio la watu waliopoteza tumaini la kisiasa??
 
Julius Mtatiro, tafadhali nisaidie majibu ya maswali haya:-

Nani ka kwakwambia kwamba CDM wanamtaka Hamad kuimarisha chama visiwani?
Mambo ya CDM yanakuhusu nini wewe Kama kiongozi mkubwa wa chama Chako?
Huoni Kama unapoteza muda kwa kitu ambacho hakikuhusu?

Mkuu acha jazba hebu soma vizuri mleta uzi then ndiyo uanze kukomenti
 
Last edited by a moderator:
Mi ningependa angehamia chadema, hamad ni kariba ya wanasiasa wanaoweza kukibeba chadema kwa hoja na mawazo yake, ana wafuasi wa kutosha upande wa zanzbar na bara pia..naamini mbowe na zitto watatupa nyavu kujaribu kumnasa
 
Nadhani CDM inahitaji zaidi ya kuongeza watu wenye majina ya kiislamu ili kufuta/kuondoa au kupunguza dhana ya udini inayokigubika chama hicho.

Prof. Safari hajawa na impact yeyote so far
Nakubaliana na wewe kamanda, kuna watu humu jf wanadhani chadema itakuwa na kushinda urais pasipokuwa na ujanja wa kuwinda nyenzo muhimu kama hizi, ndo maana ccm wanasumbua kwasababu huwezi kuwasikia wanamkataa mwanasiasa kutoka upande wa pili maana kila mtu ana nafasi yake kwenye mchezo huu, hamad, sumaye, hata wasira waje tu cdm ili chama kiimarike tuache ushabiki usiokisaidia chama
 
udini imekuwa lugha nyepesi hapa jf, ila hilo mnalolipalilia na kulishabikia, kuna siku mtaliona. Si mimi wala wewe atakayepitwa na hili. Madhara yake makubwa sana.
Tamaa zenu ambao mpo na mamlaka na hamtaki kuyaachia,,,na wale mnaotaka mamlaka hayo. Kimsingi nyie ni wabaya na humu jitambulisheni kwa majina yenu, sio mnajipa mijina uchwara kwa ajili ya kuleta chokochoko.
 
Hamad Rashidi ni mwanasiasa mzuri tu kama hana nafasi huko mimi napendekeza aje CHADEMA ila aingie kwa Moyo wote sio atuletee siasa za SHIBUDA,na pia apunguze jazba
 
udini imekuwa lugha nyepesi hapa jf, ila hilo mnalolipalilia na kulishabikia, kuna siku mtaliona. Si mimi wala wewe atakayepitwa na hili. Madhara yake makubwa sana.
Tamaa zenu ambao mpo na mamlaka na hamtaki kuyaachia,,,na wale mnaotaka mamlaka hayo. Kimsingi nyie ni wabaya na humu jitambulisheni kwa majina yenu, sio mnajipa mijina uchwara kwa ajili ya kuleta chokochoko.
Udini umepandwa na ccm na umeanza kuota, kujifanya hujui ni kujidanganya tu, isipokuwa nadhani itafutwe namna rahisi ya kuondoa hayo mapando, kwangu naamini chama kama chadema kimeathiriwa sana na hii propaganda ya udini kuliko ile ya ukanda, na ndo maana kinapata shida sana kujiuza mikoa ya pwani, kama kitampata mtu kama Hamad rashid na wenzake, kitajenga taswira inayoweza kukisogeza hatua kadhaa mbele kwa urahisi zaidi

Tatizo tanzania ni wale waliopo madarakani wanapandikiza mbegu mbaya za ubaguzi vichwani mwa wananchi lakini kibaya zaidi ni uelewa mdogo sana wa watu wetu wa kuweza kugundua hila za wanasiasa hao, wao wanameza tu, kwahivi sual a hapa si kukuza udini bali ni kutafuta namna ya kufisha mambo machafu akilini mwa watu kwa kuwaletea picha tofauti na waliyoonyeshwa awali.
 
Jamani hivi Shibuda yupo,,,,maana naona kimya,,au mawazo yake ya urais yamexpire,ama kweli Shibuda ni kiazi!!!
 
Hamad Rashidi ni mwanasiasa mzuri tu kama hana nafasi huko mimi napendekeza aje CHADEMA ila aingie kwa Moyo wote sio atuletee siasa za SHIBUDA,na pia apunguze jazba
CDM haihitaji mtu desperate kama wewe. Aje CDM kufanya nini? Huyu tayari ana chama chake ADC.
 
emashila-katika wapuuzi wewe ni mmojawapo? Kipi ambacho hakielekweki hapio unachohoji kutoka kwa mtatiro? Au wewe ndo umegeuka CDM kuliko wenye nacho wanaopeana vyeo kwa ukoo na mapenzi? Ukiwa huna la maana ni bora kunyamaza. Mstaarabu hapingi kila kitu hata kama kitu hicho kwake hakina maana. CDM kama CUF kufa ni palepale tu-wanadamu wanakufa sembuse kilichoanzishwa nao?
 
Back
Top Bottom