Hamad Rashid aapa kuimaliza CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid aapa kuimaliza CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by marmoboy, Dec 13, 2011.

 1. m

  marmoboy Member

  #1
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magazeti ya jana 12/12/2011 yaliripoti habari juu ya mvutano mkubwa uliotokea manzese kati ya walinzi wa ofisi kuu ya CUF wakishirikiana na walinzi wa wilaya ya kinondoni kupambana na mabaunsa waliokodiwa na hamad rashid mohammed. Makundi haya hasimu yalivutana katika tawi la KOSOVO ambako hamad rashid alifika na viti na meza kwa ajili ya kuwakabidhi uongozi wa kata katika harakati zake za kuchukua nafasi ya ukatibu mkuu hapo mwaka 2014 kwenye uchaguzi wa ndani ya chama wa CUF. Mivutano hiyo ya jana iliisha salama salimini baada ya walinzi wa ofisi kuu ya CUF na wale wa wilaya ya kinondoni kuamrisha kusitisha zoezi husika kwa sababu chama ngazi ya wilaya na taifa hawana taarifa ya ziara ya hamad rashid wakisisitiza juu ya kanuni za chama hicho ambazo husimamia kwamba kiongozi yoyote wa juu wa chama au mbunge au mwakilishi hawezi kutoka katika jimbo lake la uchaguzi na kwenda katika jimbo lisilo lake wala wilaya isiyo yake wala kata isiyo yake bila kuomba kibali kwa viongozi wa wilaya husika au taifa ambao ndio wana wajibu wa kusimamia ziara zote za viongozi. Baada ya hoja hizo nzito kutoka kwa walinzi hamad rashid alisitisha zoezi lake na kuondoka.

  Shughuli pevu ilikuwa leo 13/12/2011 ambapo mbunge huyo wa wawi - Pemba alikuwa na ziara nyingine katika tawi la CHECHNIA lililoko kata ya mabibo. Baada ya walinzi wa taifa na wa wilaya kuzuia shughuli ya KOSOVO inaonekana hamad rashid na wenzie walijipanga zaidi na kukodi kundi kubwa la vijana wapatao 150 ili kulinda mkutano wake wa mabibo. Majira ya saa 8.00 mchana vijana kadhaa walianza kufika ukumbi wa mkutano wengine wakiwa na makoti na wengine wakiwa na kofia za mazoezi maarufu PAMA. Wengi wa vijana hao walionekana kuwa na nyuso nzito na baadhi yao walionekana kama wamepata kilaji kidogo.


  Majira ya saa 9.00 walifika hapo ukumbini(ukumbi wa kukodi) wajumbe watatu wa baraza kuu la uongozi la CUF wakiambatana na baadhi ya wanachama wanaompinga MAALIM SEIF. Walipofika ukumbini wanachama na wananchi mbalimbali walianza kukusanyika. Wakati kusanyiko linaendelea ghafla gari ya ofisi kuu ya CUF ikapaki mita 100 hivi kutoka ukumbini. Baadaye walishuka walinzi wawili wa wilaya ya kinondoni na kwenda kwenye mlango wa ukumbi kuuliza kulikoni kikao hicho kifanyike bila wilaya kupewa taarifa?

  Walipouliza walijibiwa na mjumbe wa baraza kuu la CUF ndugu DOYO kuwa kikao kile ni halali na ni cha katibu mkuu wa watu! Walipozidi kuhoji ndipo DOYO akakasirika na kuamrisha lile kundi la vijana 150 waliotapakaa nje ya ukumbi wahakikishe wanafanya kazi iliyowaleta. Kivumbi kikaanzia palepale, wale walinzi wa CUF walianza kukatwakatwa mapanga. Mmoja amjeruhiwa mara tatu kichwani na kuzimia, wa pili amekatwa mapanga mawili shingoni, mwingine amechomwa na chupa ya soda pajani. Wengine wawili wamjeruhiwa pajani na mgongoni.

  Baada ya majeruhi hayo vijana hao walianza hatua ya kuchoma gari la chama hicho. Kilichookoa gari hiyo ni wananchama wa chama hicho waliotoka ukumbini kuja kutuliza walinzi wa kukodi wa HAMAD RASHID na wale wa CUF wilaya ya Kinondoni.

  Baada ya tukio hilo, mwenyekiti wa CUF wa tawi la CHECHNIA ndugu MUHAJI aliwasili na akasisitiza kuwa hakuna kikao kufanyika lakini kundi lilelile lililokata wanachama na walinzi mapanga likamuonya kuwa akileta ujanja watamtoa roho kwani alishakula hela za wakubwa.

  Baada ya onyo hilo, katibu wa tawi hilo ambaye anaunga mkono harakati za hamad rashid alisoma risala fupi kwa dakika mbili hivi na kueleza kuwa tawi hilo halina ofisi na kwamba wangeomba kusaidiwa shilingi 350,000 kwa ajili hiyo.

  Palepale hamad rashid alitoa shilingi 250,000 na kuahidi kuwa zingine zingemaliziwa kesho yake. Baada ya kutoa fedha hizo aliendelea kutoa shutuma nyingi sana kwa viongozi wenzie. Alieleza namna gani ambavyo MAALIM SEIF ameshindwa kuisimamia CUF na kuwa chama hicho kimepoteza muelekeo na akasisitiza kuwa ili kukiokoa chama hicho lazima wanachama wamuami yeye HAMAD RASHID ili akiwa katibu mkuu CUF iamke tena tanzania bara.

  Aliahidi pia kuwa akiwa katibu mkuu wa chama hicho matawi yote yatakuwa yanawezeshwa nchi nzima na kuwa atayatembelea mara kwa mara na kutatua shida zilizoko. Pia aliahidi kuwa atafungua vikundi vya kijasiriamali kila eneo ili wanachama wa chama hicho wanufaike kuliko ilivyo hivi sasa ambapo wanatumiwa kukijenga chama bila kuwa na malipo yoyote.

  Aliendelea pia kuwajulisha wanachama hao kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo tazanzania bara kwa sababu amekabidhiwa unaibu katibu mkuu mtoto mdogo Julius Mtatiro(29) na kuwa bwana mdogo huyo ana dharau na ndiye anakiua chama kwa upande wa bara.

  Alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Lipumba amekosa mtu wa kumsaidia na kuwa yeye ndiye mwarobaini wa CUF kwa kuwa ana ujasiri, amewahi kukaa gerezani miaka mingi na kuwa yuko tayari kufa kwani alizaliwa siku moja na atakufa siku moja na aliwasihi wananchama wamuunge mkono ili apate ukatibu mkuu na kutibu matatizo ya CUF kwa kupambana na CCM kwani yeye peke yake ndiye aliyebakia na ujasiri huo baada ya chama chake kuolewa na CCM upande wa Zanzibar.

  Ameahidi kuzunguka nchi nzima na kuwahamasiha wanachama waandamane hadi makao makuu ya CUF na kumshinikiza MAALIM SEIF aache ukatibu mkuu ili anakie na umakamu wa rais wake.

  Nimebahatika kuingia katika kikao husika na ku-note vitu vingi sana, MASIKINI MTATIROOOO!
   
 2. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hakika strategy za CCM ktk kuvuruga upinzani zinafanya kazi vizuri
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  CUF! Ni unga wa ngano! Hamad apelekeshe huko, mbinu zao tunazo kitambo.
   
 4. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kenge mimi wao vichenchede............hawataki wasi wao makenge wasio na mkia
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Mmmmmmhh! Mwongozo kidogo tunaomba hapo ktk lugha!
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Asante mleta hoja, yote tisa kumi ni hapo kwenye bold kama ni mameno yake basi wasilalamike wanapoambiwa wao ni CCM-B.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Well, Ni leo ndio wamekuja fahamu ukweli? mbona siku nyingi tunawaambia wafuasi wa CUF kwamba Maalim Seif ni Pandikizi na Opportunist anayependa sana madaraka, hivyo hakuwa akipigania lolote zaidi ya yeye mwenyewe kuwa rais ama makamu wa rais. Na ajabu ya Mungu huyu baba alipokuwa Waziri wa elimu Zanzibar na Waziri kiongozi alionekana hafai kabisa leo ndio kenda kuwa kioo cha watu.

  Hamad Rashid vita hii wala hataiweza na ijulikane tu kwamba sasa hivi anapambana na CCM ndani ya CUF maana wameisha penyeza. Unapomshambulia Seif Hamad unaishambulia CCM mchezo ndio huo. Maadam CUF imeungana na CCM visiwani ni bora mkubali kuwa CCM kabisaa au kuunda chama kingine kupingana na CUF. Ama ajiunge Jahazi Asilia maana hawa ndio haswa wapinzani wa Seif Hamad toka kuundwa kwa chama hicho.
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hamad Rashid anaweza kuwa na point lakini problem yake ni kwamba anatakiwa kufuata katiba ya CUF namna ya kupata Ukatibu mkuu..

  Sidhani kama ni wakati wa campagn au hata uchaguzi umefika??

  Time will who is right
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Hamad R hata kama yuko sahihi lakini strategy anayotumia ya kupambana kwa nguvu aslani hatafika popote mbele ya Seif. Ingawa hadi sasa sielewi nani anatumiwa kati ya Hamadi na Seif lakini HR aelewe Seif ndiye kashika mpini hata kama CCM wanamtumia HR hawatamuacha mshirika wao mkuu Seif.
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Hapa nitarudi asubuhi kwa saa za East Africa. nimeweka mark ili thread hii isinipotee asubuhi.
   
 11. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  jamani inakuwaje mama (mke) na watoto wanagombana halafu baba anakaa kimya kunusuru familia? hii ndoa inawalakini baina ya kile chama chetu na hiki chama chao!!!! kiufupi viongozi wa CUF ( hamad na maalim) wamejaa ubinafsi na uchu wa madaraka, both bwa mkubwa makamu prezidaa ( wa zenjibari) na mwenzie kiongozi asiye rasmi wa kambi ya upinzani mjengoni wanapenda madaraka....sasa imefikia wakati wako tayari kuona chama kinakufa kwa ajili ya tamaa zao hizo..... hamadi kainanga chadema weeeeeee... akasahau kuwa " mwenzio akinyolewa....", haya mwiteni mzee (mume) sasa aje kuwaweka sawa.....
   
 12. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwanini mnaumiza kichwa kuchambua hii mada wakati ndivo inavotakiwa iwe??

  Hawa CUF wanatofauti gani na makundi ya kipiganaji kule somalia?? Kwanza ukiangalia hata majina ya matawi yao yanaashiria kumwaga damu...eti tawi linaitwa kosovo, chechnia what do you expect will come out from those places?? Kama wenyewe kwa wenyewe wanachukiana kwa kiasi hicho je itakuaje pale wataposhika dola?? Ndo maana nawaambieni JK pamoja na mapungufu yake lakini ni mtu mvumilivu sana....

  Ingekua mmoja wa hawa wanaokatana mapanga kisa kupata nafasi ya kutoa misaaada tena ya lazima ndio yupo pale magogoni sijui ingekuaje.... sasa wote ni wazanzibari wanagombania kuwa makatibu wakuu ili kuinua upinzani "bara" wakati huohuo wanadai muungano hauna tija kwao...how can this be possible?? Huyu Hamadi anakaa Mikocheni halafu sometimes anaponda muungano...??? Toka akose nafasi kwenye ile serikali mpya ya Znz hajawa kama wa zamani kipindi kile mwenyekiti wa kambi ya upinzani.

  Leo ndo najua madaraka ndio chanzo cha yote haya... kazi ipo CUF... na wewe Mtatiro sijui ni kitu gani kilikupeleka huko... Pima mwenyewe then fanya maamuzi mapemaaaaaa
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CUF sasa mapanga 'sha' [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 12 December 2011 20:39 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Aziza Masoud
  UPEPO wa kisiasa ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF), unaendelea kuvuma vibaya baada ya jana, mashabiki wa chama hicho kupambana wenyewe kwa kutumia silaha za jadi yakiwamo mapanga.Tukio hilo limekuja siku moja tangu mabunsa waliotoka kusikojulikana, kuvamia mkutano wa mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed, kufanya vurugu na kumtoa mbunge huyo kwa nguvu.

  Jana, Hamad Rashid aliendelea na ziara yake kwenye matawi ya chama hicho Kata ya Manzese. Kabla hajaanza mkutano wake katika tawi la Chechinia, lilitokea gari aina ya Mitsubishi Fuso likiwa na watu waliokuwa na silaha mbalimbali yakiwamo mapanga na mawe na walipofika eneo la mkutano huo, walianza kupambana na wafuasi wa chama hicho waliokuwa wakimsikiliza Hamad.

  Awali, watu wasiojulikana walisambaza ujumbe mfupi wa simu wakionya wanachama wa CUF kutohudhuria mkutano huo kwani ungegeuka kuwa sehemu ya mauti yao.Hata hivyo, wanachama hao wa CUF katika tawi hilo la Chechnya walikuwa wamejiandaa vema kukabiliana na chochote ambacho kingetokea kama ilivyokuwa juzi.

  Baada ya kufika walianza kushambuliana kwa mapanga na ndipo mtu mmoja alipojeruhiwa huku watu hao waliovamia mkutano huo, wakikimbia na kuacha gari hilo.

  Kufuatia kukimbia na kutelekeza gari hilo, baadhi ya wanachama walilichukua na kulipeleka ofisi za chama hicho kwa ajili ya taratibu zaidi.


  RPC alonga

  Hata hivyo, alipoulizwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema hadi jana jioni, hakuwa na taarifa zozote kuhusu tukio hilo.

  Kamanda Kenyela alibainisha kuwa kama vurugu hizo ni za ndani ya chama, polisi wasingeweza kuingilia, lakini wakitoka nje na kuanza kufanya vurugu katika jamii wangedhibitiwa.


  Hamad Rashid

  Jana, mbunge huyo alirejea kueleza dhamira yake ya kumvaa Katibu Mkuu wa sasa Maalim Seif Sahrrif Hamad katika nafasi hiyo ya utendaji mkuu wa chama.

  Hadi jana jioni Hamad Rashid alikuwa akiendelea na mkutano wake huku hali ikiwa imetulia baada ya wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono, kudhibiti wavamizi hao.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  To divide and rule would only,tear us apart
  And in this judgment there is, no partiality!
  Source: bob marley in Zimbabwe
  Hongera CCM, mafanikio yanaanza kuonekana
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HAMAD RASHID MOHAMED AKAIUWE CUF MARA NGAPI HUKO ZAIDI YA MADHARA YOTE ALIOKWISHAKIFANYIA CHAMA HIKI HUKU BARA???

  Akaimalize CUF mara ngapi, huyu naye bana!!!

  Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu atakayefurahia chama chochote cha USHINDANI nchini kinapogeuka NDEMBENDEMBE kwani ushupavu kwao ni faraja ya wapiga kura na kupanua zaidi ushindani wa ki-demokrasia na kuongeza ufanisi zaidi kati na ndani ya vyama vyote husika.

  Kwa matokeo mema yote ya ushindani kwa watu hamuoni leo hii hata kile chama, chenye kiburi kama kobe kugoma kutembea pindi aguswapo au mwenye majivuno makali sawa na mnyama kinyonga tembea zake kuvuka barabara ya lami, cha CCM CONSERVATIVES nao siku hizi wanalazimika kwenda kusimama kando kando ya barabara kwenye njia panda sawa tu na vyama vingine kwenda KUTUTONGOZA sisi Waheshimiwa wapiga kura??

  Kila unapomuuliza mwananchi yeyote huku bara kwamba chukizo lake kwa Chama Cha Wananchi CUF huku Bara ni nini hasa jibu litakua ni simpo; (1) nikifikiria USALITI WA HAMAD RASHID kwa Umma wa Tanzania Bungeni kwa kuabudu Malslahi binafsi za CCM naona kero kusikia chochote kuhusiana na chama hiki.

  Ndio, (2) kila nikikumbuka visu vya Mahita vyenye Tomato Sauce, nahisi ugaidi mle, na (3) kila ninapoona vyama vingine vya upinzani vikizuiliwa kuingia katika ngome zake huko visiwani kufanya kampeni na uenezi kwa amni bila bughudha, naona udini tupu. Prof Lipumba, hayo ndio mambo matatu makuu ya kupiga vita ili CUF ipate kurejea katika afya yake ya hapo awali laa sivyo chama hiki ni kuzikwa shimo kaburi moja na CCM hivi karibuni.

  Aheri ya CUF ya Mama Maghimbi yenye msimamo na kuhoji mambo kwa maslahi ya Umma wote wa Tanzania kule kwenye Bunge la Muungano kuliko haka ka-CUF muhuri wa CCM chini ya Hamad Rashid kule mjengoni Dodoma inayofanya kazi kwa maelekezo na fikra sahihi za TUMBO.

  Toka Lwakatare akose ubunge na kukosa pia nafasi ya kuendelea kusimamia vema ngome na HESHIMA ya CUF kule bungeni, tangu hapo hakuna kitu tena ni bure kabisa!!!

  In a nutshell, uongozi wa CUF wakiniuliza juu ya nani aliyeiua ile CUF ya miaka ile kote Tanzania Bara jibu langu ni rahisi tu kwao; ni hawa Ma-Kada wa CCM
  Hamad Rashid Mohamed pamoja na Mzee Omar Mahita na ule mchezo wa mkokoteni wa visu vilivyopakwa Tomato Sauce kuonyesha kwamba hiki ni chama cha KIGAIDI kumbe utumbo mtupu!!
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wapi Zawadi Ngoda?

  Habari hizi zilipokuja kwa mara ya kwanza Zawadi Ngoda alibisha sana na kudai kwamba barua iliyonukuliwa kwenye gazeti ilikuwa ni ya kughushi. Sasa mambo yamekuwa dhahiri, nadhani hakuna mtu atauliza source wala kubisha kwamba ndani ya CUF kuna mgogoro unafukuta na unaweza kuwa mkubwa sana.

  Hamad Rashid anadanganya wana chama wake, huwezi kusema eti utatembelea matawi yote nchi nzima. Yeye angesema kwamba atajitahidi kuweka ofisi za chama kila wilaya na kama uwezo utaruhusu basi wanaweza kufungua na kwenye Kata.

  Risala imekaa kiwizi wizi tu, sasa shilingi 350,000 ndo zitajenga ofisi? Au ndio pango la kodi ya mwaka mzima? Hapo ndipo panapoonyesha kwamba waganga njaa wako wengi sana. Je, Hamad Rashid yuko tayari kuwapa hizo laki tatu na nusu matawi yote ya Tanzania Bara?

  Hoja yake ya ujasiriamali haina mashiko, naona anacheza na hisia za vijana ambao ni wanachama wa CUF. Anasaka jeshi la vijana wa CUF limsaidie kumng'oa Maalim Seif Shariff Hamad.

  Kwani vijana hawatakiwi kupewa uongozi? Mtatiro ana udogo gani hapo? Labda kama ana hoja ya dharau au matatizo mengineyo, na kama ana matatizo basi chama kingekuwa kimeisha mchukulia hatua za kinidhamu. Halafu vijana watamuunga mkono kwamba kijana Mtatiro ang'oke ili aingie mzee? Vijana wataongoza lini?

  Hamad ana machungu ya kupoteza uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, kama CUF wangekuwa na majority, wala kusingekuwa na huu mgogoro unaoendelea sasa. Swala la CUF kutokuwa na wabunge huku bara siyo geni, lipo miaka yote. Wabunge karibu wote wa kuchaguliwa wa CUF huwa wanatoka Pemba, huku bara wengi wao huwa ni wa kuteuliwa na wakishateuliwa wakilamba mshiko miaka mitano huwa wanakimbilia CCM. Mmojawapo ni Teddy Kasela-Bantu na mwingine ni Mama mmoja wa Mwanza, aliachia ngazi walipomaliza kikao cha mwisho cha Bunge la Tisa.
   
 17. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mleta hoja anaonyesha ushabiki na upendeleo. Hamad halengi kuimaliza CUF maana hakuna awezaye kuimaliza CUF isipokuwa wanachama wakiamua imalizike. Kimsingi anachofanya Hamad kilichelewa. Maana Seif aliitumia CUF kutafuta ulaji binafsi bila kujali kuwa kuna watu tena wasio na hatia waliomwaga damu zao wakiamini wanapigania ukombozi wao kumbe ni ulaji wa Seif. Seif kwa sasa hana bao wala hadhi. Ana hali mbaya kama Lyatonga Mrema kutokana na tamaa na upogo. Ni jukumu la wana CUF kuhakikisha hawatapeliwi tena. I wish you well. Good luck guys.
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Acha propaganda na udini wako wewe..
   
 19. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sijui tufanyeje kukinuru chama
   
 20. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa nasikiliza matangazo ya Idhaa ya kiswahili ya ujerumani na mtangazaji akamuuliza Ismail Jussa kwama Kuna tetesi kuwa Hamad Rashid ameahidiwa kuwa Mgombea mwenza kwa ticket ya CCM kwenye uchaguzi ujao wa 2015, na amekuwa jirani na kigogo wa juu wa CCM na serikali (inasemekana) ni mizengo Pinda. Ismail alikubaliana na mtangazaji huyu.

  Kwa hiyo hili ni kweli na hiki kinachofanyika ni strategy ya CCM kuimaliza CUF hasa kule Zanzibar kwani kwa bara CUF kwishney. Wanataka waimalize na Zanzibar kwa kuwa wameonekana wameanza kupata nguvu hata Unguja na inasemakana hata uchaguzi ulopita maalim Sief alishinda na akahongwa umakamu wa rais ili akubali matokeo.
   
Loading...