KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Hamad R hata kama yuko sahihi lakini strategy anayotumia ya kupambana kwa nguvu aslani hatafika popote mbele ya Seif. Ingawa hadi sasa sielewi nani anatumiwa kati ya Hamadi na Seif lakini HR aelewe Seif ndiye kashika mpini hata kama CCM wanamtumia HR hawatamuacha mshirika wao mkuu Seif.
HAMAD RASHID anaweza kuwa yuko right,sishangai kabisa kinachompata,Hivi vyama vyenu vyote vinavyolilia demokrasia kiukweli ndio vimekua vya kwanza kuminya na kubaka demokrasia ndani ya vyama hasa katika chaguzi za ndani,ni jambo la kawaida sasa kwa wenyeviti wa vyama mbadala vya Tanzania kuiona nafasi ya uenyekiti kama ni taasisi yao binafsi,anapotokea mtu kutaka kuwapa challenge kwenye nafasi hiyo unapoitishwa uchaguzi kwa mujibu wa katiba za vyama hivyo wenyeviti wetu hawa hununa na kufanya hila za kuwazuia,hawapendi kuwa tested,wao wangependelea zaidi kuwa wenyeviti wa maisha;sizungumzi kwa majungu ipo mifano hai ambayo ndio hata imechangia wetu wengine kama mimi kutokua na vyama na kuamua kutofungamana na upande wowote kutokana na kutotaka kujiweka karibu na demokrasia za kinafiki,mifano ni kama ifuatayo:
Kila mtu aliona mutungirehi alivyonyanyasa na kugombana na mrema alipotangaza kugombea nafasi ya "mzee" kwenye uchaguzi mkuu wa tlp,mwanzoni walikua marafiki na mrema kumchulkulia kama kijana wake lkn aliposema mzee na mimi nataka nikupime ubavu akaonekana hana adabu!
Tukaja kuona jinsi profesa safari alivyodhalilishwa na cuf kisa kutaka kumpima ubavu Lipumba!wakasema eti kwa kutaka kuyumia haki yake ya kupigiwa kura ama kuchaguliwa ndani ya chama chake na wanachama wenzake eti ametumwa na adui(ccm)!!!!!!!
Pia kila mtu hapa anakumbukumbu ya kilichompata marehemu chacha wangwe pale alipojaribu kumpima ubavu "bwana mkubwa" wa chadema,kwanza alianza kwa kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti,mwenyekiti mboe akafanya kila analolijua kumzuia asigombee akashindwa,then akatumia kila mbinu chafu na safi ili jamaa asipate kura za kutosha pia ikashindikana marehemu chacha akaibuka kidedea bwana mkubwa akanuna sana,hakuipenda demokrasia iliyotumika kumuweka madarakani rasta,alitaka aweke mtu wake wanachama wakamwambia no mzee kura yako ni moja tu ndio unatakiwa uitumie hiyo kumzuia kwenye sanduku la kura!kura yake haikutosha kumzuia chacha bahati mbaya!chacha wangwe hakuishia hapo akamwambia mwenyekiti sasa naitaka nafasi yako!mwnyekiti akaona hii sasa balala,akaanza mikakati ya kumzuia,this time akafanikiwa!kweli chacha wangwe hakugombea uenyekiti wa chadema na hatakuja kugombea milele nafasi hiyo!
Ikawadia zamu ya zitto kumpima ubavu mwenye kigoda,kilichotokea wengi tunajua,kwani wengi humu kipindi hiki mlikua mmeshaingia chadema...rejea nini kilitokea!
Rai yangu kwa wenyeviti wa vyama mbadala hapa wanacho angalau japo kidogo cha kujifunza kutoka magamba,japo nao wana kamchezo eti ka kumuachia mwenyekiti amalize muda wake! upuuzi mtupu,hakuna demokrasia ya namna hiyo,wenyeviti wakubali kuwa tested kwenye chaguzi za ndani.Nawasilisha.