Bakar Hamad Bakar: Bidhaa Inayotoka Zanzibar Kuja Bara Isilipishwe Kodi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR - BIDHAA INAYOTOKA ZANZIBAR KUJA BARA ISILIPISHWE KODI

KODI ZA BANDARINI KERO KWA WANANCHI

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi katikaBunge la JMT (Zanzibar) Mhe. Bakar Hamad Bakar akiwa anachangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali lakini zipo changamoto mbalimbali hasa kwenye mizigo kutoka Zanzibar kuja Bara kuwa imeondolewa kodi kodi lakini bado inaonekana ni changamoto hasa kwa mizigo midogo midogo.

Pia Mhe. Bakar Hamad Bakar, ameendelea kusema kuwa haiwezekani Mtu anatoka Zanzibar na Sukari kilo mbili kujanayo Bara anaambiwa alipe kodi, jambo hilo lilimfanya Mbunge wa Baraza Wawakilishi kuitaka Serikali kulifanyia kazi jambo ili kuondoa kero kwa Wananchi.

"Haiwezekani mwananchi amesafiri kutoka Zanzibar na kilo 2 za sukari, TV used [iliyotumika] moja anakuja kutumia nyumbani anafika Bara anaambiwa alipe kodi, hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja, haiwezekani anayetoka Morogoro kwenda Dar es Salaam halipi kodi, lakini anayetoka Zanzibar kuja Bara akifika Dar es Salaam anatakiwa alipe kodi.” – Mbunge Bakar Hamad
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-26 at 20.31.54(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-26 at 20.31.54(1).jpeg
    23 KB · Views: 7
Back
Top Bottom