Haloteli kuhusu kasi ya internet mmeanza kuyumba, jirekebisheni

TOHATO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
1,170
3,775
Kwanza niwape hongera kwa kuwa moja ya mitandao inayotoa huduma nyingi kwa bei nafuu,kuanzia msg,dakika , kutoa na kutuma hela kwa Halopesa.

Ila sasa mmezingwa na jambo la Kasi ya intenet kuwa ndogo sana.

Mawazo yangu nadhani kwa vile kumekuwa na wigo kubwa na wahamiaji kwenye mtandao wenu hasa kwasababu ya unafuu wa bando. Hivyo Jitahidini kurebisha hili suala.

Imekuwa kero sasa hadi uvizie usiku ndo angalau.

Naongea nikiwa mmoja wa mteja wenu tangu mwaka mnaanza huduma zenu 2015. Na kipindi chote hicho mlijitahidi ila tangu mabadiliko ya vifurushi yalipotokea hadi sasa mmezidiwa nguvu.
 
Mi najuta kutumia huduma ya halo yako ya kuweka akiba ya malengo.. ni najuta mnoo sitakaa nirudie
 
Back
Top Bottom