Badala ya kutumia Kiswahili fasaha Halotel hupenda kutumia kiswahili cha mtaani au cha Kizaramo kama hivi: HAUNA salio la kutosha.... badala ya kiswahili fasaha cha;HUNA salio la kutosha...Hauna hutumika kama vile; Muungano huu HAUNA faida kwa upande mwingine na huwezi kusema;Muungano huu HUNA faida kwa upande mwingine.Vyombo vya mawasiliano kama Tigo, Voda,Halotel nk ni kioo cha jamii katika nyanja ya taaluma.Na hawa Tigo nao wanao vilaza wa lugha kwenye vitengi vyao.Tigo huchapia sana kwa lugha ya Kizaramo pia.Wao hutumia "Ivi "hujui kama ....badala ya ; "HIVI " hujui kama....