Matumizi ya Lugha ya Kiswahili

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,042
1,454
Ninaimani wote hatujambo.

Nimekuwa nafuatilia kwa karibu sana kuhusu hoja ya matumizi ya kiswahili hapa nchini hadi tumefika hatua baadhi yetu tunatamani kiswahili kitumike katika ngazi zote za utowaji wa elimu.

Sababu kubwa imekuwa watanzania wanafahamu vizuri kiswahili hivyo kuwafundisha kwa kutumia kingereza ambacho hakifahamiki vizuri kunachangia kufanya wengi wao kumaliza shule au vyuo bila kuelimika vizuri.

Pia tumekwenda mbali zaidi na kutolea mitano ya nchi kama China na Japana au Germany kuwa zimefanikiwa sababu ya kutumia Lugha yao.

Mimi sikubaliani na huo upotoshaji mkubwa unafanywa ama ka makusudi au kwa kutokuwa na uelewa wa kutosha. Hakuna utafiti wowote wa kitaalam uliofanyika na kubainisha kwamba hizo ndiyo sababu za watanzania wengi kumaliza vyuo bila kuelimika vizuri. Sababu zangu za kutokukubaliana ni kama zifuatazo:-

1. Elimu hii hii inayotolewa kwa kiingereza ndiyo walivyofundishwa wazazi wetu wakaelimika vizuri sana kulitumikia hili taifa siku za nyuma hasa serikali ya awamu ya kwanza wasomi wengi walikuwa wazuri hakuna anayebisha hilo, hadi sasa ndiyo wasomi wanaendelea kuheshimika sana hapa nchini.

2. Watu wengi wanaokwenda kwenye kozi za ualimu hasa ngazi ya primairi ni wale waliofeli shuleni na kushindwa kazi zingine ndo wamekuwa wakipelekwa kusomea kozi za ualimu kama vile ualimu ni kazi inayotakiwa kufanywa na wajinga.

3. Mazingira ya shule nyingi kuanzia primary sekondari ni duni sana kiasi kwamba hayawezi kuleta matokeo chanya ya wanafunzi kujifunza na kueleimika vizuri. Chukulia mfano shule nyingi za Dar es salaam ambazo ni za day wanafunzi wanakutana na changamoto kubwa usafiri na pia mchana hakuna chakula shuleni hivyo ni vigumu katika mazingira hayo wanafunzi kupata elimu nzuri.

4. Kazi ya ualimu haionekani kuwa na umuhimu wowote katika jamii yetu hivyo walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu hakuna utaratibu wa kuhakikisha walimu wanapata huduma bora za mahitaji yao ili waweze kuwa na uwezo na kujituma katika kutimiza wajibu wao.

5. Wapo wataalam mbali mbali ambao wamekwenda nje ya nchi kusoma kama urusi, India, uingereza, marekani, ujerumani na kwengineko ambako elimu haifundishwi kwa kiswahili na wamefundishika wakaellimika na ni wataalam wetu wakubwa tunao wategemea katika taasisi mbali mbali hapa nchini.

Hivyo siyo jambo zuri kuacha kutatua matatizo yaliyosababisha elimu yetu kushuka na badala yake kujificha kwenye lugha ya kiswahili.

Ni vema tukajiuliza, hivi mtu akiwa amekifahamu vizuri sana kiswahili anaweza kwenda kufundisha kiswahili marekani kama hajuwi kingereza. Kwanini tunadhania kuacha kutumia kingereza kufundishia kutatusaidia kupanga kiswahili nje ya nchi. Ni lazima uwe unajuwa lugha ya hiyo nchi ndipo uweze kufundisha kiswahili chako.

Ni vema tukaachana na siasa badala yake tutatue tatizo la kushuka kwa elimu yetu kwa kuanza na kuthamini kazi ya ualimu kwa kuwalipa vizuri ikiwezekana kuliko kazi nyingine yoyote ili wanafunzi wanaofaulu vizuri ndio waende kwenye vyuo vya ualimu kwa kufanya hivyo kutasaidia kuboresha kiwango cha elimu kwa kutumia hii hii lugha ya kiingereza kufundishia.

Kama kuna wanafunzi ambao hawaelewi kingereza wanapofundoshwa hao ni wajinga sawa na wajinga wengine ambao hawaelewi kiswahili wanapofundoshwa hivyo tusitumie ujinga wa baadhi ya wanafunzi kutokuelewa na kusema tatizo ni lugha ya kufundishia.

Karibuni kwa maoni yenu wana bodi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom