Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Baada ya Mwananchi kupitia JamiiForums.com kueleza kushangazwa na hali ya uchafu ya vyoo vya Stendi Kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda, kutokana na kujaa maji taka na hivyo kuweka rehani afya za watumiaji ambao wanaweza kupata magonjwa mbalimbali kama UTI, Mamlaka imetoaufafanuzi.
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Natamani Viongozi wa Wilaya na Mkoa Katavi wangekuwa wanatumia Vyoo vya Stendi ya Mizengo Pinda labda wangevijali
==================================
UFAFANUZI JUU YA VYOO VYA STENDI KUU YA MABASI YA MIZENGO PINDA
17/07/2025
Ipo taarifa iliyochapishwa na mtandao wa kijamii wa "Jamii Forum" unaoonesha hali ya uchakavu wa Miundombinu ya vyoo katika stendi kuu ya mabasi ya Mizengo Pinda.
Stendi kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda ina vyoo 5 vyenye jumla ya matundu 38.
Picha ya matundu ya vyoo iliyochapishwa kupitia mtandao wa Jamii forum ni matundu 3 ya vyoo vilivyofungwa ambavyo havitumiki kwa sasa ambavyo viliziba kutokana na matumizi yasiyo sahihi yalitokana na watumiaji kutupa kwenye matundu ya vyoo vitu kama mabunzi, nguo, makopo na pampasi.
Aidha Kufuatia kuziba kwa matundu 3 ya vyoo hivyo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imefunga matundu hayo na kuchukua hatua nyingine za haraka ambazo ní:-
1. Kuanza kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo.
2. Kufungua matundu 8 ya vyoo ambayo hayajawahi kutumika yaliyopo jengo kuu upande wa chini.
Aidha halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa abiria juu ya matumizi sahihi ya vyoo.
Imetolewa na:-
Donald Pius
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda
Hali ya Vyoo ilivyo kaa ilivyolalamikiwa na Mdau.
Alichosema Mkuu wa Mkoa ~ RC Katavi asema "Mkurugenzi asipotekeleza agizo la usafi Stendi ya Mizengo Pinda nitaona cha kufanya"