KwetuKwanza
Senior Member
- Mar 13, 2023
- 121
- 218
Kuna vitu vinafanywa na serikali ukiviangalia vinaumiza, vinatia watu hasira, na hata hakuna anayejali, au kuumia kama ambavyo Wananchi tunaumia.
Hapo juu kuna picha nne, ingawa nimeziunganisha ili zikae sehemu moja, ni picha ya gari la taka, nyingine la kukusanya uchafu na nyingine ni mashine ya kuchonga Barabara na kukusanya uchafu pia.
Hivyo, vifaa na magari vilinunuliwa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, viligharimu pesa nyingi, nadhani hapo hata Bilioni moja zilifika kama sikosei.
Hizo pesa ni kodi za wananchi, ni miaka kama mitatu hivi tangu vinunuliwe, leo vimepakiwa vyote pale kwenye uzio wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi (Somanda) Karibu kabisa na Jengo la Mochwari, havifanyi kazi.
Magari yote hayo na mashine hiyo vimeharibika, havifanyi kazi ni Mwaka mmoja sasa vimewekwa hapo, hakuna Kiongozi, mtumishi au Mtendaji yeyote ambaye anahurumia kodi hizo za Wananchi, wamevitelekeza, kama hawakununua hivi, kama walipewa bure hivi, kama siyo Kodi za wananchi, hakuna mtu yeyote ambaye anajali.
Ukiangalia hivyo vifaa vyote, vilinunuliwa kwa ajili ya suala la usafi kwenye Mji wa Bariadi hasa, leo Mji ni mchafu kweli kweli, kila sehemu ukipitia uchafu umejaa.
Kwa muda wa zaidi ya miezi sita hivi, Mji wa Bariadi hakuna gari la kusomba uchafu kwenye makazi ya watu, uchafu umejaa mpaka basi, kila sehemu ukipita hali ni mbaya, uchafu umerundikwa Barabarani kwenye makazi ya watu mpaka kero na harufu Kali.
Hilo gari la maji taka lilikuja Ili kusaidia Wananchi, lilikuja kupunguza gharama ambapo awali gari lilitoka Mkoani Mwanza, tangu limeharibika changamoto zimerudi pale pale, vyoo vinajaa gari la kuchukua uchafu kulipata ni shida.
Shida zimerudi palepale, Kodi za Wananchi, Kodi zetu zinateketea. Viongozi wa Juu, tunawaomba mukamulike Halmashauri ya Mji wa Bariadi, mulikeni hizi Kodi zinazoteketea, mziokoe.
Waziri Mkuu Mwiguli Mchemba, tunakuomba wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi uje umulike hii Hali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Kodi zetu zinateketea.
Tunakuomba uje uangalie wananchi wako tunavyoteseka na Wakati Kodi zetu zinateketea.