Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM(NEC) imeridhia ombi la Ndg. Abdulrahman Kinana kustaafu wadhifa wa Katibu Mkuu wa chama

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Leo May 28 .2018 ni jumatatu ya mnyukano CCM kwenye kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) baada ya report ya wabadhirifu kutua kwa Mh. Rais JPM.

Vigogo wa CCM wote wametua Jijini Dsm kuhudhuria kikao hicho kitakachojadiri hatma ya wabadhirifu wa mali za chama. Kitaongozwa na Mwenyekiti CCM Taifa Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

Mubashara tujuzane!

Updates

DeRkbsGWsAAyyz4.jpg


DeRlPb3XUAAlF0n.jpg
Wajumbe Wapya wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM, Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere wakiingia katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) muda huu


Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM(NEC) imeridhia ombi la Ndg. Abdulrahman Kinana kustaafu wadhifa wa Katibu Mkuu wa chama

Rais Magufuli - ''Napenda kumshukuru ndugu Kinana kwa utumishi wake katika Chama cha Mapinduzi (CCM), na CCM itaendelea kutumia uzoefu wake katika majukumu mbalimbali ya chama kwa kadiri itakavyohitajika''

ccm1.jpg
ccm2.jpg
 
Vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Kamati kuu (CC) vinaanza leo Jijini Dar es Salaam ambapo Halmashauri Kuu (NEC) itajaza nafasi za wajumbe wake ziiizokuwa wazi, tayari Mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt. John Magufuli amewateua Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne, Mizengo kayanza Peter Pinda na Makongoro Nyerere kuwa Wajumbe wa NEC

Jambo lingine ambalo taarifa za kuaminika zinaeleza kutokea ni kuwasilishwa kwa ripoti ya Uhakiki wa Mali za Chama mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC)

Hata hivyo taarifa inayosubiriwa kwa hamu ni ukweli kuhusu kujiuzulu kwa Katibu Mkuu , Comred Abdulrahman Kinana.

Nitaendelea kutoa Updates za vikao.
 
Ukichunguza sanaaaaa, utagundua mwenye kaya anafuta siasa za Rais Wa china..

Ile tunaita " personalized system of rulling"

Kimahesabu ,watu wengi waweza msifaham kwann Ukaguzi wa mali??? Kwann kile???

Hii sio miujiza,bali nimahesabu makali sana yalopigwa namtu wa hesabu

Matokeo yake, nikuwafanya waonekane wasofaaa ,wezi na wachafu wale ambao mkuu anawaona km wanachama ambao wanaushawishi mkubwa!!

Baada ya kuwakata haoo, ambapo wengi watasamehewa kwasababu ya Uchama , watalazimika kunyamaza ,namwishoooooo Mkuu ndio ataonekana mtu pekee sahihi wakuendesha chama...

Sishangai sana ,ni maandalizi
 
Back
Top Bottom