Halima Mdee na wenzake 18 watatoboa Mahakamani kwa kutumia hoja hizi?

I agree with your observations. I, even myself, wonder how the Court reached to a yesterday's reported order. But, I was not in Court and did not see all documents submitted thereto for the order to be given. My belief is: there were more documents and submission we did not witness in Court.
Mahakama za mchongo hizi, amini tu.hakuna.doc zingine
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Kama ilivyo ada yangu, nianze kwa kutamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania au kwingineko. Daima, nimekuwa nikijenga hoja; kukosoa kwa staha; kushauri au kuunga mkono hoja yoyote ya kisiasa au ya kitaifa kumhusu yeyote yule. Sibagui chama chochote au mtu yeyote wa kumhusisha na hoja yangu. Pamoja na yote yanayojulikana kwenye sakata zima za akina Halima Mdee, nawiwa kusema neno katika maeneo mawili: ubunge wao na taratibu za kinidhamu zilizofuatwa dhidi yao.

Nikiri kuwa nimeziona na kuzisoma nyaraka zilizowasilishwa na akina Halima Mdee Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la kutekelezwa kwa uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA dhidi yao pamoja na kuondolewa kwa ubunge wao. Sitaki na wala siko tayari kujadili kwa kina kuhusu nyaraka husika (kwakuwa si sahihi na hairuhusiwi kujadili jambo ambalo liko mahakamani). Mpira uko kwa Jaji Mgeta kwasasa na yeye anaucheza katika kutoa haki kwa anayestahili. Unaweza kuziona hapa: Nyaraka za kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wabunge wenzake dhidi ya CHADEMA

Hatahivyo, nisamehewe kwa kufanya hivyo, nitatumia kauli mbili za kwenye Kiapo cha Halima James Mdee alichokiwasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania katika shauri lao. Aya husika ni ya 2 na 18 ya Kiapo hicho. Kwanini ni Halima Mdee? Ndiye anayetajwa na kuonekana kama kiongozi wa wahusika 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA. Hata kesi yao imeanza na jina lake. Kwanini Kiapo? Kisheria na kiuhalisia, Kiapo ni ushahidi. Katika Kipo tajwa kunapatikana mambo yangu mawili.

Kuhusu ubunge wao, Halima Mdee (kwenye aya ya 2 ya Kiapo chake) anasema kuwa wao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kudhaminiwa na CHADEMA. Yaweza kuwa makusudi au bahati mbaya, Mdee amekwepa kusema kuwa walipendekezwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kwakuwa wao wanaamini kuwa ni Wabunge halali wa VIti Maalum wa CHADEMA, walipaswa kupendekezwa na kudhaminiwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kuacha hoja hii ya kupendekezwa na CHADEMA kama takwa la kikatiba na kisheria, ni kuuteteresha ukuta wao wa kuwakinga.

Kuhusu taratibu za kinidhamu zilizofuatwa kwenye kufukuzwa kwao uanachama na CHADEMA, kwenye aya ya 18 ya kiapo chake, Halima Mdee analeta hoja ya kuwa wanachama ambao pia ni 'Wabunge' wana taratibu za kipekee katika kushughulikiwa kinidhamu tofauti na wanachama wa kawaida. Tena, taratibu hizo za kipekee kwa wanachama walio 'Wabunge' hazikufuatwa. Yawezekana ni kwa makusudi au bahati mbaya, Halima Mdee hakuelewa mantiki ya hoja yake mwenyewe na hoja ya CHADEMA katika jambo lao-la jinsi walivyoteuliwa kuwa Wabunge.

Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.

Taarifa ya kufukuzwa uanachama imewasilishwa Bungeni ili kuwaondoa kwenye Ubunge wote wanaotajwa kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalum. Kutokana na hayo mambo mawili na mengineyo, nauona ukuta wanaoutumia akina Halima Mdee kujikinga na kuhalalisha ubunge wao kama dhaifu na usio na msaada kwao. Lakini, kwakuwa jambo hili lipo mahakamani, tusubiri matokeo yake. Haya yabaki kama maoni yangu tu.

Nadhani upo sahihi sana,lakini tuiachie mahakama kwa uamuzi wa haki.
 
Nimesoma hoja za Kibatala na Mtobesya naona kama ni hojo nzuri..lakini kwa nini huwa nashindwa kwenye mapingamizi anayoweka? mahakama huwa zinafanya kusudi au ni kweli huwa na hoja dhaifu kisheria?
Mahamaka huwa zinafanya kusufi tu zingekuwa huru wala wasingethubutu hata kufungua hio kesi mahakamani maana wagejua fioa wataangukia pua tu.

Kwakuwa wana mdhamini wao serikalini na mahakama ni serikali unaweza kuta wanashinda kifala sana hadi unashanga huyu jaji vipi kapitiwa au kalewa.

Imasikitisha sana
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Kama ilivyo ada yangu, nianze kwa kutamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania au kwingineko. Daima, nimekuwa nikijenga hoja; kukosoa kwa staha; kushauri au kuunga mkono hoja yoyote ya kisiasa au ya kitaifa kumhusu yeyote yule. Sibagui chama chochote au mtu yeyote wa kumhusisha na hoja yangu. Pamoja na yote yanayojulikana kwenye sakata zima za akina Halima Mdee, nawiwa kusema neno katika maeneo mawili: ubunge wao na taratibu za kinidhamu zilizofuatwa dhidi yao.

Nikiri kuwa nimeziona na kuzisoma nyaraka zilizowasilishwa na akina Halima Mdee Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la kutekelezwa kwa uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA dhidi yao pamoja na kuondolewa kwa ubunge wao. Sitaki na wala siko tayari kujadili kwa kina kuhusu nyaraka husika (kwakuwa si sahihi na hairuhusiwi kujadili jambo ambalo liko mahakamani). Mpira uko kwa Jaji Mgeta kwasasa na yeye anaucheza katika kutoa haki kwa anayestahili. Unaweza kuziona hapa: Nyaraka za kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wabunge wenzake dhidi ya CHADEMA

Hatahivyo, nisamehewe kwa kufanya hivyo, nitatumia kauli mbili za kwenye Kiapo cha Halima James Mdee alichokiwasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania katika shauri lao. Aya husika ni ya 2 na 18 ya Kiapo hicho. Kwanini ni Halima Mdee? Ndiye anayetajwa na kuonekana kama kiongozi wa wahusika 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA. Hata kesi yao imeanza na jina lake. Kwanini Kiapo? Kisheria na kiuhalisia, Kiapo ni ushahidi. Katika Kipo tajwa kunapatikana mambo yangu mawili.

Kuhusu ubunge wao, Halima Mdee (kwenye aya ya 2 ya Kiapo chake) anasema kuwa wao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kudhaminiwa na CHADEMA. Yaweza kuwa makusudi au bahati mbaya, Mdee amekwepa kusema kuwa walipendekezwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kwakuwa wao wanaamini kuwa ni Wabunge halali wa VIti Maalum wa CHADEMA, walipaswa kupendekezwa na kudhaminiwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kuacha hoja hii ya kupendekezwa na CHADEMA kama takwa la kikatiba na kisheria, ni kuuteteresha ukuta wao wa kuwakinga.

Kuhusu taratibu za kinidhamu zilizofuatwa kwenye kufukuzwa kwao uanachama na CHADEMA, kwenye aya ya 18 ya kiapo chake, Halima Mdee analeta hoja ya kuwa wanachama ambao pia ni 'Wabunge' wana taratibu za kipekee katika kushughulikiwa kinidhamu tofauti na wanachama wa kawaida. Tena, taratibu hizo za kipekee kwa wanachama walio 'Wabunge' hazikufuatwa. Yawezekana ni kwa makusudi au bahati mbaya, Halima Mdee hakuelewa mantiki ya hoja yake mwenyewe na hoja ya CHADEMA katika jambo lao-la jinsi walivyoteuliwa kuwa Wabunge.

Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.

Taarifa ya kufukuzwa uanachama imewasilishwa Bungeni ili kuwaondoa kwenye Ubunge wote wanaotajwa kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalum. Kutokana na hayo mambo mawili na mengineyo, nauona ukuta wanaoutumia akina Halima Mdee kujikinga na kuhalalisha ubunge wao kama dhaifu na usio na msaada kwao. Lakini, kwakuwa jambo hili lipo mahakamani, tusubiri matokeo yake. Haya yabaki kama maoni yangu tu.
wametumwa na maccm hao pia mahakama ni tawi la ccm hakuna haki wataipata chadema
 
Nadhani wanacheza "delay technique" ili watafute muwafaka wa jambo lao, wao wana haki ya kwenda mahakamani, CHADEMA wana haki ya kuwafukuza wanachama wao kwa taratibu zao na bunge nalo lina taratibu zake kwa wabunge wake. Tatizo kubwa la Chadema lililolifanya na vyama vytote vya upinzani baada ya uchaguzi kufanyika wao hawajakubaliana na matokeo kwa kuwa uchaguzi ulugubikwa na dhulma na figisu nyingi tu, hivyo hakuna aliyekwenda mahakamani hata ya kwamba wanajua hakuna haki itatendeka, kwenye nchi zetu haki huwa inachelewa lakini itafika kwani KARMA haijawahi kumuacha mtu salama.
 
Petro, hakuna Cha kutoboa, Mgeta ana maelwkezo tayari ya kuamua kuwa 1+1=4 katika natural mathematics. Sawa na Jaji wa Mbowe walivyokuwa wanafanya vioja vya kihanithi!
 
Hakuna mahakama hapa we ongea tu maana hukumu tayari imeshaandikwa
 
Nadhani wanacheza "delay technique" ili watafute muwafaka wa jambo lao, wao wana haki ya kwenda mahakamani, CHADEMA wana haki ya kuwafukuza wanachama wao kwa taratibu zao na bunge nalo lina taratibu zake kwa wabunge wake. Tatizo kubwa la Chadema lililolifanya na vyama vytote vya upinzani baada ya uchaguzi kufanyika wao hawajakubaliana na matokeo kwa kuwa uchaguzi ulugubikwa na dhulma na figisu nyingi tu, hivyo hakuna aliyekwenda mahakamani hata ya kwamba wanajua hakuna haki itatendeka, kwenye nchi zetu haki huwa inachelewa lakini itafika kwani KARMA haijawahi kumuacha mtu salama.
Utakwenda mahakama ipi na wewe? Ya Ibrahim Juma? Be serious please
 
Nakubaliana na wewe

Hata CCM hupendekeza majina zaidi y 100 halafu NEC huteuwa kulngana na idadi inayohitajika.

Cha ajabu Chadema walipeleka exactly.majina 19!
Chadema kumbe ni zaidi tunavyoisikia kuwa chama cha siasa,kinamanguvu yakupenya hadi magerezani kuwatoa watuhumiwa.
 
NEC wakimteua vipi bila kupokea majina kutoka CHADEMA? ulitaka aseme NEC walipewa majina na CHADEMA kwani ye inamhusu? NEC watajibu waliyatoa wapi majina ndo sababu na wenyewe ni washtakiwa kwenye kesi hii.
Simba wa Yuda alipeleka,sasa hayupo.
Kibatala unaswali.
Jaji naona simba wa Yuda alikuwa sahihi kwa maslahi ya mikopo japo Nchi hii nitajiri nitajiri nitajiri,tumechezewa sana.
 
BROTHER... Nikukumbushe tu halima mdee alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA, ni member wa CC na anajua in and out ya mchakato husika.

Halima siyo mpumbavu anapose.a kuwa wao ni wabunge halali wa CHADEMA kwa kuwa ni wazi anaujua mchakato wote ulivyofanyika

Lakini pia halima hawezi kuwa mpumbavu kiasi cha kusema hadharani kuwa kulikuwa na uhuni ktk maamuzi dhidi yao.

Umesema wewe si mwanachama wa chama chochote lakin mbona hoja zako haziko neutral?yani umebase upande mmoja wa kuwakandia wabunge 19 na kukibeba CHADEMA? Obviously wewe ni CHADEMA na huna sababu ya kujificha

mwisho: Binafsi nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa halima na wenzake walifoji barua ya CHADEMA ya kwenda tume ya uchaguzi kwa sababu kama kweli wangekuwa wamefoji basi CHADEMA zamani sana ingekuwa imeshawashitaki wabunge hao.

tusubiri maamuzi ya mahakama na ukweli utajulikana.. haya mengine ni blah blah tu
Yule manzi aliekuwa mahabusu akatolewa usiku usiku asubuhi yake akaenda kula kiapo gereji napo unasemaje?
 
CDM hawakupeleka hayo majina hata Halima Mdee mwenyewe anakiri hilo. Kasema waliteuliwa na NEC na kudhaminiwa na CDM, yaani kaeleza njisi alivyoaanza kuvaa sketi/suruali kabla hajavaa taiti
Hapo kuna technical issue iliyotumika kama alivyosema mtoa mada, hiyo inatupa mpira kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwani majina yanayopendekezwa huwasilishwa tume ya uchaguzi, na si lazima mhusika ufahamu, wakishafanya mchakato wa kuchuja ndio yanapelekwa Bungeni na Spika anayapokea kama wabunge halali.kwa kifupi Mbunge huteuliwa na Tume ya uchaguzi baada ya kupokea majina kutoka kwenye chama. So hapo wanaruka kiunzi na kuiachia NEC ndio ijibu cross examination.So hoja ya Petro Mselewa inamantiki kabisa.Tuiachie mahakama
 
(Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.)

Kwa hiyo unawafukuza uanachama kwa kosa gani mpaka hapo ??????
Kwa hiyo kosa lao hujaliona tu?
 
Wewe umeshatoa hukumu tayari maana hata bandiko lako limeegemea upande mmoja, kama CHADEMA haiwatambui Halima Mdee na wenzake kama Wabunge basi wanalo deni kwa Watanzania, warudishe Ruzuku waliyopewa na Serikali kupitia Wabunge 19 maana hawakustahili kuichukua hiyo Ruzuku ambayo ni kodi zetu Wavuja jasho.
Yaani mijitu mingine sijui mkoje! Unaambiwa hawajawahi kuchukua ruzuku
 
Ubishi mwingine ni wa kijinga. CHADEMA wapeleke majina ya Halima na wenzie NEC halafu baadae wakatae, wawavue uanachama...? Kwa nini walipeleka hayo majina sasa? Tusipotezeane muda. Hii siyo rocket science hata kidogo. Wala hahitaji mtu kuwa mwanachama wa chama fulani kujua. Nchi imejaa uhuni hadi kwa Rais mwenyewe. Wote tulikuwepo October 2020. Tunajua kilichotokea. Kama haukuwepo, uliza.
Umesema wewe si mwanachama wa chama chochote lakin mbona hoja zako haziko neutral?yani umebase upande mmoja wa kuwakandia wabunge 19 na kukibeba CHADEMA? Obviously wewe ni CHADEMA na huna sababu ya kujificha
 
Utakwenda mahakama ipi na wewe? Ya Ibrahim Juma? Be serious please
Mahakama ni ya nchi, Ibrahim Juma hana mahakama yeye ni mtumishi kama walivyowatumishi wengine wa mahakama. Yaani ufe kwa kiu kwa kuwa huwezi kwenda kuchota maji mtoni sababu kuna mamba?
 
Nakubaliana na wewe

Hata CCM hupendekeza majina zaidi y 100 halafu NEC huteuwa kulngana na idadi inayohitajika.

Cha ajabu Chadema walipeleka exactly.majina 19!
Cha ajabu yani CDM wakapeleka na jina la mwanachama aliyeko gerezani...

Hauhitaji kuwa na ubongo ili uwe fisiem
 
Back
Top Bottom