Halima Mdee na wenzake 18 watatoboa Mahakamani kwa kutumia hoja hizi?

Hao ni SAwa na mtu kumpeleka mpenzi wake mahakamani eti kisa kamuacha. Hao wanalindwa na serikali lengo kuwahadaa wafadhili, hio kesi itaenda hadi October 2025 wakati wa uchaguzi, Ili wamalizie ubunge wao.
Wangekuwa wana maanisha wangewasimamishia ubunge kwanza hadi kesi iishe. Covid-19 ni michezo Kati ya Mbowe, CCM na serikali, Mbowe KILA siku anaitwa ikulu, na ikulu ni CCM. Na CCM ni adui wa Chadema, wewe shika jembe kalime.
 
Kusema ni uhuni tu haitoshi inabidi kuthibitisha ni uhuni gani?

Kura ya siri ingeweza kuleta mzozo kwamba kuna 'forgery' Kura ya wazi ndiyo hiyo inaitwa Uhuni

Walipokata rufaa walijua CC ilikuwa na uhalali.

Hivi kuna uhuni zaidi ya wao kutoeleza nani kawapa barua? Hivi kuna uhuni kuliko ule wa kumtoa Nusrat Magereza usiku bila ' Nolle' mahakamani! Hivi kuna uhuni zaidi ya ule wa kuapa kwenye banda la uani la Bunge!
Uhuni ni pamoja na kutozingatia utaratibu wa kikatiba wa kuwafukuza wanachama

Uhuni ni kuwazushia wamefoji barua wakati kimsingi barua ni orijino eti kwa sababu tu wamegoma kupelekeshwa😀
 
Nawasalimu waungwana wa JF,

Kama ilivyo ada yangu, nianze kwa kutamka kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania au kwingineko. Daima, nimekuwa nikijenga hoja; kukosoa kwa staha; kushauri au kuunga mkono hoja yoyote ya kisiasa au ya kitaifa kumhusu yeyote yule. Sibagui chama chochote au mtu yeyote wa kumhusisha na hoja yangu. Pamoja na yote yanayojulikana kwenye sakata zima za akina Halima Mdee, nawiwa kusema neno katika maeneo mawili: ubunge wao na taratibu za kinidhamu zilizofuatwa dhidi yao.

Nikiri kuwa nimeziona na kuzisoma nyaraka zilizowasilishwa na akina Halima Mdee Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la kutekelezwa kwa uamuzi wa Baraza Kuu la CHADEMA dhidi yao pamoja na kuondolewa kwa ubunge wao. Sitaki na wala siko tayari kujadili kwa kina kuhusu nyaraka husika (kwakuwa si sahihi na hairuhusiwi kujadili jambo ambalo liko mahakamani). Mpira uko kwa Jaji Mgeta kwasasa na yeye anaucheza katika kutoa haki kwa anayestahili. Unaweza kuziona hapa: Nyaraka za kesi iliyofunguliwa na Halima Mdee na Wabunge wenzake dhidi ya CHADEMA

Hatahivyo, nisamehewe kwa kufanya hivyo, nitatumia kauli mbili za kwenye Kiapo cha Halima James Mdee alichokiwasilisha Mahakama Kuu ya Tanzania katika shauri lao. Aya husika ni ya 2 na 18 ya Kiapo hicho. Kwanini ni Halima Mdee? Ndiye anayetajwa na kuonekana kama kiongozi wa wahusika 19 waliofukuzwa uanachama na CHADEMA. Hata kesi yao imeanza na jina lake. Kwanini Kiapo? Kisheria na kiuhalisia, Kiapo ni ushahidi. Katika Kipo tajwa kunapatikana mambo yangu mawili.

Kuhusu ubunge wao, Halima Mdee (kwenye aya ya 2 ya Kiapo chake) anasema kuwa wao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kudhaminiwa na CHADEMA. Yaweza kuwa makusudi au bahati mbaya, Mdee amekwepa kusema kuwa walipendekezwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kwakuwa wao wanaamini kuwa ni Wabunge halali wa VIti Maalum wa CHADEMA, walipaswa kupendekezwa na kudhaminiwa na CHADEMA kabla ya kuteuliwa na NEC. Kuacha hoja hii ya kupendekezwa na CHADEMA kama takwa la kikatiba na kisheria, ni kuuteteresha ukuta wao wa kuwakinga.

Kuhusu taratibu za kinidhamu zilizofuatwa kwenye kufukuzwa kwao uanachama na CHADEMA, kwenye aya ya 18 ya kiapo chake, Halima Mdee analeta hoja ya kuwa wanachama ambao pia ni 'Wabunge' wana taratibu za kipekee katika kushughulikiwa kinidhamu tofauti na wanachama wa kawaida. Tena, taratibu hizo za kipekee kwa wanachama walio 'Wabunge' hazikufuatwa. Yawezekana ni kwa makusudi au bahati mbaya, Halima Mdee hakuelewa mantiki ya hoja yake mwenyewe na hoja ya CHADEMA katika jambo lao-la jinsi walivyoteuliwa kuwa Wabunge.

Tangu mwanzo, CHADEMA imekuwa inapinga uhalali wa kuteuliwa kwa akina Halima Mdee. Kwakuwa wamekuwa wakipinga uhalali wa kuteuliwa kwao, ni wazi kuwa CHADEMA haikuwahi kuwatambua akina Mdee kama Wabunge wao wa Viti Maalum baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Hivyobasi, akina Halima Mdee walishughulikiwa kinidhamu kama wanachama wengine wa kawaida na hakukuwa na sababu za kushughulikiwa kama 'Wabunge' kwakuwa wao si 'Wabunge' kwenye macho ya CHADEMA. Ndiyo kusema, taratibu za kipekee za kuwashughulikia kinidhamu wanachama walio Wabunge za CHADEMA 'hazikuwahusu akina Halima Mdee.

Taarifa ya kufukuzwa uanachama imewasilishwa Bungeni ili kuwaondoa kwenye Ubunge wote wanaotajwa kama Wabunge wa CHADEMA wa Viti Maalum. Kutokana na hayo mambo mawili na mengineyo, nauona ukuta wanaoutumia akina Halima Mdee kujikinga na kuhalalisha ubunge wao kama dhaifu na usio na msaada kwao. Lakini, kwakuwa jambo hili lipo mahakamani, tusubiri matokeo yake. Haya yabaki kama maoni yangu tu.
Yametimia...Mkuu GT
 
Uhuni ni pamoja na kutozingatia utaratibu wa kikatiba wa kuwafukuza wanachama

Uhuni ni kuwazushia wamefoji barua wakati kimsingi barua ni orijino eti kwa sababu tu wamegoma kupelekeshwa😀
Sasa huo uhuni na huu utetezi wako, nenda kawasaidie mahakamani!
 
Hawa ndio wasomi w taifa hili kweli safari bado ndefu. Naona kakimbia uzi wake.
 
Nilifikiri kuna la maana umeandika ndio maana nimesoma najuta!
 
Ipo siku wanaodhamini huu uhuni watalipa fedha wanazowalipa.hakuna kitu kinauma kuwa na msururu wa matozo afu wanalipwa covid 19 .hii dharau itazaa laana.
 
Back
Top Bottom