Halima Mdee: Hatujakata rufaa, muda bado upo

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
Mdee.jpg

Mhe. Halima Mdee na wabunge wenzake 18 wa Chadema waliopatikana kwa njia ya viti maalum wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kula kiapo jijini Dodoma hivi karibuni

Halima Mdee, alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) amesema yeye na wenzake 18 waliofukuzwa uanachama wa chama hicho baada ya kula kiapo cha ubunge wa viti maalumu bila ridhaa ya chama, bado wana muda wa kukata rufaa kupinga adhabu hiyo.

Akizungumza na gazeti hili, Mdee alisema hadi kufika leo wana siku 17 zaidi za kukata rufaa baraza kuu kupinga uamuzi wa kamati kuu ya chama hicho iliyowavua uanachama na nyadhifa zao zote.

Mbali na Mdee wengine ni Ester Bulaya, Ester Matiko, Agnesta Lambert, Grace Tendega, Salome Makamba, Jesca Kishoa , Nusrat Hanje, Tunza Malapo, Conchestar Rwamlaza.

Wengine ni Naghenjwa Kaboyoka, Hawa Mwaifunga, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Asia Mohammed, Sophia Mwakagenda, Cecilia Pareso na Felister Njau ambao walivuliwa uanachama na kamati kuu Novemba 26 baada ya kukiuka msimamo wa chama hicho.

Desemba mosi, Mdee aliwaeleza wanahabari kuwa hawana mpango wa kuondoka ndani ya chama hicho na kwamba wana mpango wa kukata rufaa baraza kuu ili haki itendeke dhidi yao.

Novemba 30 walipewa barua za uamuzi wa kufukuzwa uanachama na hivyo kuwa na fursa ya kukata rufaa wakitakiwa kufanya hivyo ndani ya siku 30 tangu kupokea barua hiyo.

“We have 30 days (tuna siku 30 tulizopewa) kwa ajili ya kukata rufaa. Sasa nashangaa hapa haya yanayoendelea hapa katikatika deadline ni Desemba mwishoni. Tutapeleka rufaa zetu kwa sababu bado tunakipenda Chadema. Watu wasitulazimishe tukate rufaa leo au juzi bado siku zipo,” alisema Mdee.

Katika rufaa hiyo, Mdee na wenzake wataeleze namna walivyokwenda kuapa wakati chama chao kikilumbana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu aliyewatuma waende, mtu aliyepeleka majina katika tume hiyo.

Wakati hayo yakijiri Chadema kilitangaza kuanza kutumia nguvu ya mahakama kupinga mchakato wa uteuzi wa wabunge hao 19 na mtu aliyesaini fomu zao kwa nafasi ya katibu mkuu.Hata hivyo kwa nyakati tofauti, Spika wa Bunge alisisitiza Mdee na wenzake ni wabunge halali na watekeleze majukumu yao ya kibunge popote walipo.

Chanzo:
Mwananchi 14 Desemba 2020.

Nyongeza ya Mama Amon:

Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema ya mwaka 2006 Toleo la 2019 na Kanuni zake, Kanuni ya 6.5.8 inasomeka kama ifuatavyo:

"Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu." (Katiba ndogo, uk. 99).
 
Hakuna haja ya kukataa rufaa, hawatakiwi kwenda bungeni kushiriki kwenye bunge la wezi wa kura na wamwaga damu fullstop.
Wangefaaa kama wangekubali kutengeneza kiki za kutishiwa iliwakaishi ugaibuni na kucahafua taifa. Sasa wamegomea huo mchezo mchafuu.
 
Yaani Halima James Mdee ndio Kiongozi mkuu wa akina mama wa Chadema!

Akajifunze utulivu kwa mama Sophia Simba wa CCM!
Inasikitisha sana kuona wenzetu wa cdm wamemwamini mwanamama "mcharuko" wa namna hii kuwaongoza wanawake wote wa cdm taifa. ☺
 
Mimi niwashauri tu wakae chini kama kweli wanafikiri wanataka kubaki wanachadema waache uasi waombe radhi maisha yaendelee ila wasitishe mpango wao ovu wa kuendelea kushiriki kwenye Bunge hovu kuwahi kutokea.
 
Anafikiri hao wengine waliowahi kufukuzwa CDM hawajui kuna kukata rufaa?

Anataka kujaribu ku-outshine the master?😁! Yaani washinde rufaa ili Mbowe aonekane kilaza mbele ya hao wanawake?

Akamsome Robert Greene kwanza.

Wakasujudu tu kwa jamaa labda awafikirie kuliko hii option ya kutaka kumtunishia misuli.
 
Mzee Halima Mdee na Covid-19 wenzio wote mmeshakua "ZILIPENDWA".

Kaeni chini mjitafakari na mjiKumbushe mlipotoka na mnapoelekea. kati ya "CCM" au "WANACHAMA WA UPINZANI"(Mlio Waasi) nani aliewapigania baada ya hii issue kutokea??? Mkalazwa hospitalini mkiwa "MAHUTUTI" na kutibiwa kwa "PESA ZA WANACHAMA WA UPINZANI na MAOMBI YA VIONGOZI WA DINI WAPENDA HAKI".

Leo hao wanachama wa upinzani pamoja na hao viongozi wa dini wanaopenda haki kwenu hawana maana, na mnajali matumbo yenu.

#Baada ya hapo, ndio mtajua mna roho za aina gani wewe na wenzako.

Hawajajistukia bado
 
Ukiwa Ccm Kila Kitu Sawa
Kinajipanga Tu, Halima Na Wenzake Wapo Juu Kama Mkungu Wa Ndizi
Watamu Kama Mcharo!!
😅😄😃😁😂🤣😅😄😄😃😀😁
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Back
Top Bottom