Halima Mdee amchana Pinda live Bungeni Ardhi ya Mpanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halima Mdee amchana Pinda live Bungeni Ardhi ya Mpanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 17, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri Mkuu Pinda Na Mbunge Halima Mdee Bungeni
  Wakijadili Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Ardhi

  Mdee aonya machafuko kugombea ardhi


  Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee aliitahadharisha Serikali kuwa kuipuuza sekta ya ardhi kutasababisha watu wa taifa hili kuchinjana."Sekta ya ardhi ndiyo uhai wa nchi hii. Sekta hii tukiipuuza... na ninaiambia Serikali tukiipuuza watoto wetu, wajukuu wetu watakuja kuchinjana na hatutaki kutengeneza Tanzania ya kuchinjana katika kipindi," alisema Mdee.

  Akizungumzia kuhusiana na Kampuni ya Agri Soil ambayo imepewa eneo la uwekezaji katika Wilaya ya Mpanda, Mdee alisema mbali na upungufu wake imekiuka sheria."Imekiuka sheria ya nchi, sheria zetu zote ziko wazi na hili namwambia Mheshimiwa Waziri Mkuu asiposhughulikia vizuri anaweza akaanguka nalo kabisa kwa sababu kuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa ofisi yake ilihusika tutumie busara tuokoe nchi," alisema.

  Mdee alisema sheria inasema kama kuna ushirikiano unamhusu raia na kwamba sheria ya uraia haijatambua halmashauri na kuhoji kuwa Serikali iwaambie wabunge ni raia gani anamiliki hekta zaidi ya 200?

  Mgogoro wa shamba hilo uliibukia kwa mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Pudenciana Kikwembe ambaye aliitaka serikali kutoa asilimia 25 ya hisa katika shamba hilo kwa wazawa na kwa sababu madiwani walishirikishwa katika suala la Agro Soil basi waamue gawio la faida litakwenda katika mradi gani.

  Mwananchi

  Halima Mdee, Serukamba jino kwa jino

  MBUNGE wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, amemponda Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) kuwa ni muongo na anapeleka siasa uchwara bungeni.

  Mdee amemjibu Serukamba kwa kumweleza kuwa, anamuonea huruma kwa kuwa hajui kama mwaka 2015 Mbunge huyo atarudi bungeni.

  Serukamba alisema, wabunge waache kutafuta umaarufu kwa kusema uongo bungeni na kwamba, wananchi wa Kigoma ndiyo wanaofahamu hali halisi ya mambo yao. "Huo uzalendo uchwara unaoletwa leo hatuutaki Kigoma, tunataka maendeleo' amesema Serukamba alipoomba kutoa taarifa wakati Mdee anachangia bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  Mdee amesema, hatafuti umaarufu kwa kuwa yeye tayari ni maarufu, anataka kufanya kazi. Mbunge huyo amesema, hazungumzi kitu ambacho hana ushahidi nacho hawafanyi uchochezi. " Hatutafuti umaarufu wa kisiasa, upo tayari, tunataka kuijenga nchi yetu" amesema Mbunge huyo kijana, Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  Amemtahadharisha Waziri Mkuu awe makini katika kushughulikia mkataba unaodaiwa kummilikisha mwekezaji eneo kubwa la ardhi mkoani Rukwa, kwa kuwa inadaiwa kuwa ofisi yake imehusika. Kwa mujibu wa Mdee, mkataba huo umekiuka sheria za nchi na kwamba, Pinda asipokuwa makini ‘ataanguka nalo'. Amewataka wabunge waache ushabiki, hilo ni tatizo kubwa.

  Baada ya Mdee kusema hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu aliomba kutoa taarifa, akasema, hakuna sheria iliyovunjwa Rukwa, na hakuna mwekezaji aliyemilikishwa ardhi mkoani humo.

  Mdee amesema bungeni kuwa haitaki taarifa ya Nagu, na anashangaa kuona kuwa wanaopaswa kutekeleza sheria wanatetea uhalifu. Mbunge huyo amesema, anataka haki itendeke kwa wananchi wa Kwembe na Mabwepande mkoani Dar es Salaam na atakuwa na wananchi hao hadi mwisho. "Sisi tutakufa na wananchi wetu, liwe jua, iwe mvua"amesema Mbunge huyo na kusema, Serikali inapaswa kuweka utu kwanza, iache siasa zifanywe na vyama.

  Ameiomba Serikali itumie busara kushughulikia mgogoro wa ardhi eneo la Chesimba, na amewatuhumu baadhi ya wenyeviti wa mitaa na madiwani wasio waaminifu kuwa wanauza maeneo. Amedai kuwa, maeneo ya wazi yakiwemo yakiwemo yaliyotengwa kwa shughuli maalum yanauzwa, na kwamba, wakubwa wanajenga ‘mabangaloo'. Amesema, ardhi ndiyo mhimili wa nchi na kwamba, sekta hiyo ikipuuzwa baadaye wananchi watachinjana.

  "Sekta hii ikipuuzwa Watoto wetu, wajukuu wetu watakuja kuchinjana, hatutaki kutengeneza Tanzania ya Watanzania kuja kuchinjana" amesema Mdee.


  Source Habari Leo.

   
 2. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Pinda kaishasema yuko tayari kutetea hii kitu hata kama itammaliza
  tuna waziri mkuu kweli?
   
 3. p

  plawala JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichangia vizuri kama kawaida yake,kina Pinda hawawezi kutenda tofauti na kinachofanyika,ardhi kibao ziko mikononi mwa wazawa au wawekezaji bila kufuata sheria kikamilifu
   
 4. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi...
  Hofu yangu isije ikaonekana kuwa CDM ndiyo
  wameleta vurugu pindi zitakapotokea
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nadhani Mnyika awahishe Hoja binafsi ya kutokuwa na IMAN nae. Kama wabunge wa magamba watampitisha atuletee uraiani hiyo hoja. Nguvu ya umma itumike. PM anaboa. Kila kitu anapotosha
   
 6. d

  dorry Senior Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Achilia mbali kuchanwa hata wakipasuliwa live hawaelewi chochote hawa wana roho ngumu kama paka mwitu. Dhuluma kibaoooo.
   
 7. G

  GAGAGIGIKOKO Senior Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,627
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Tanzania haina rais,waziri mkuu wala serikali, kuna genge la wahalifu wanajiita serikali na mwisho wao hauko mbali. Huyu Pinda ni dhaifu sana kama bosi wake.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  KWani PInda siyo CCM??? wale wenzake tu?>? yeye je??
   
 10. G

  GAGAGIGIKOKO Senior Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii serikali na watendaji wake inanikumbusha ka msemo haka'KENGE HASIKII MPAKA DAMU ZIMTOKE MASIKIONI" Huyu waziri mkuu mpaka aone nguvu ya umma ndo atajua kumbe enzi za unyapara zimepita
   
 11. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Watu wa Nape wako wapi JF jamani? Naona mijadala inapita tu bila kupingwa make wale watu nao wana umuhimu wao kwa kuchangamsha genge.

  Kina MS, FF na wenzake siwaoni na ninawamiss.
   
 12. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Pinda ni msanii tu, anadai yeye ni mtoto wa mkulima lakini hao wakulima wenyewe ndo anawasaliti kila uchao
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,627
  Likes Received: 4,731
  Trophy Points: 280
  Nape anawabania sana anadai anawalipa mamilioni kumbe anajishibisha mwenyewe sasa wamesusa mpaka fungu liongezeke, magamba bwana kwa kuzimiana taa,wamekubuhu.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwakuwa taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba uongozi mzima wa wilaya kuanzia kwa mkurugenzi hadi madiwani walilipiwa trip ya kwenda marekani na huyo 'mwekezaji',katika mazingira kama hayo tusitarajie jambo ama kauli tofauti na hiyo ya pinda.
  Mtoto wa mkulima keshasema hii ndo awamu ya mwisho kuwania ubunge,sasa kwanini ahangaikie maslahi ya watu wengine hadi akose muda wa kujiandaa kuwa muwekezaji. Tumesikia mawaziri wakuu kadhaa waliomtangulia wanavyowekeza kwa kuhodhi mahekari ya ardhi huku wananchi wa maeneo husika wakitaabika.
  Kinachozidi kudhihirika kila mara ni kwamba wanamagamba wote wanafanana, kama alivyowahi kusema baba wa taifa; wanamagamba wote 'manzi ga nyanja' muda wote wao wanatekeleza sera yao ya chukua chako mapema.
  Hata wale wanamagamba wachache waliokuwa wanaaminiwa na wananchi japo kidogo lakini nao wameanza kuwakatisha tamaa.
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  itammaliza kweli,hata baada ya miaka 50,tusubiri muda tuu
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na huyo Serukamba ni samsingi ya yule mdosi fisadi aliyesukumwa korongoni mwezi uliopita. Kila siku alikuwa akishinda katika outer office ya RA (caspian) utadhani alikuwa mlinzi wake.

  Halafu nyie watu wa Kigoma vipi mnamchagua huyu Mrundi kuwa Mbunge wenu?
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wameishiwa nyimbo -- walifikiri chejo???
   
 18. B

  Bazil Tweve Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli pinda ni kichwa cha mwendawazimu hana mwelekeo
   
 19. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyu PM AKILI ZAKE ZIMEPINDA KAMA LILIVYO JINA LAKE
   
 20. G

  GAGAGIGIKOKO Senior Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ya pinda tumwachie pinda ayapindue ili apinduke nayo.Ndo maana ukimwangalia usoni amejaa matuta utafikiri ngiri ajuza sababu ya unafiki wake
   
Loading...