Hali ya Vijijini ni mbaya sana

Hali ya Vijijini ni mbaya sana

Bila kupoteza muda,hali ya amani katika Vijijini vyetu ni ya kusikitisha sana,Serikali wekeni umakini katika hili
Kuna tukio limetokea hivi karibuni,katika Kijiji cha Magoza kata ya Kuparang'anda.

Binti mlemavu wa masikio,macho na bubu,amebakwa mchana kweupe, ni hili la kubaka, ni jambo la kawaida sana Vijijini,na Hawana njia ya kutatua.

Kadhalika,jambo la kutiana mimba hususan kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi,imekuwa kawaida mno,adhabu anayopewa Mtia mimba,ni kupeleka kiroba cha sembe kilo Tano kila wiki.

Tatizo
Katika Vijiji vingi,hakuna vituo vya polisi,hakuna lolote lile ambalo wananchi wanaweza kukimbilia
Ifike Wakati, Serikali iweke angalau Kituo kimoja katika Kijiji au Kitongoji,kupunguza uhalifu na kuweka amani

Unaweza kusema
Serikali ipo Mjini tu, Kijijini hakuna Serikali
sio vijijini tu hata mijini watu wanabakwa wanafunzi mimba nje nje.... juzi kati nimetoka mkoa nikamkumbuka jiran yangu wa vijibweni nilikaa nae vizuri sana nikasema nimpelekee mazaga ya njiani nikapita darajani nikala nunge pale nikaitafuta vijibwax nilipofika wakanipokea nikatoa mazaga wakati napiga stor na bro akaletewa mtoto amshike nikapa hongera ndio ananiambia fatuma katuletea mjukuu nilishangaa kinoma maana huyo fatuma ni mtoto mdogo kajifungua mwaka jana mtoto kashasogea now anaanza kutembea.
nikauliza mazingira nikaambiwa mimba ni ya mwanafunzi wa form 3 nilichoka kabisa ila wazazi hawana time ya kupelekana polisi swala limeisha kifamilia kwahyo hapo sioni nguvu ya serikali.

liniagana na bro ila sio siri jambo lile lilinikera japo sio mwanangu na ishatokea sijui hatma ya fatuma ila kwa familia yake naona kabisa hakuna tena kusoma inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom