Hali ya Vijijini ni mbaya sana

Hali ya Vijijini ni mbaya sana

Bila kupoteza muda,hali ya amani katika Vijijini vyetu ni ya kusikitisha sana,Serikali wekeni umakini katika hili
Kuna tukio limetokea hivi karibuni,katika Kijiji cha Magoza kata ya Kuparang'anda,Binti mlemavu wa masikio,macho na bubu,amebakwa mchana kweupe,Ni hili la kubaka,ni jambo la kawaida sana Vijijini,na Hawana njia ya kutatua,
Kadhalika,jambo la kutiana mimba hususan kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi,imekuwa kawaida mno,adhabu anayopewa Mtia mimba,ni kupeleka kiroba cha sembe kilo Tano kila wiki....
Tatizo
Katika Vijiji vingi,hakuna vituo vya polisi,hakuna lolote lile ambalo wananchi wanaweza kukimbilia
Ifike Wakati,Serikali iweke angalau Kituo kimoja katika Kijiji au Kitongoji,kupunguza uhalifu na kuweka amani

Unaweza kusema
Serikali ipo Mjini tu,Kijijini hakuna Serikali
Kuna Kijiji Fulani kijana akitaka kuoa anamuapproach Binti. Binti alikubali ponepone yake. Akikataa basi, kijana ana organize vijana wenzake.
Basi hiyo Binti asitoke hata kwenda dukani, amekamatwa Kwa nguvu na kubebwa Hadi geto la mchizi.
Wakati huo wazazi wa muoaji feki pia wamepangwa.
Ikihakikishwa Binti kuwepo geto, basi wazazi hao huamka asubuhi na mapema kwenda kiwaambia wazazi wa Binti kwamba Binti yao wanae.
Kisha hufanyika makubaliano kati ya hao wazazi na hatimaye Binti huolewa atake asitake.
 
Kwa wasukuma huko shinyanga bado wazee wanauwawa sana wanapigwa mapanga siyo mchezo hasa wabibi, basi tu imefika hatua hayaripotiwi tena kwenye vyombo vya habari
Safari ni ndefu sana wale viumbe hadi kubadilika
 
Back
Top Bottom