Hali ya uchumi nchini: CAG alia na ukata

Hali ya uchumi nchini: CAG alia na ukata

Kama nimeelewa vizuri andiko, naona kama CAG analalamikia hela ya maendeleo tu ya ofc yake, kwasababu kama waliomba 18b na kati ya hizo 8b ni zamaendeleo, ili afanye kazi zake kwa ufanisi anahitaji 10b ambapo anasema mwezi mmoja baada ya badget alipewa 2b then 5b, na mwisho 4b ambazo zinafanya jumla ya 11b, sasa hapo atashindwaje kuzifikia halmashauri zote na kumaliza hata kama ni kwa kuchelea kidogo ukulinganisha na muda waliojiwekea?
Msaada please....
 
Naomba uniache mkuu nile mshahara wa bure,hakuna kazi ya kufanya

Siku hizi tunasema 'Kituo cha mshahara' hatusemi tena kazini hapa kwetu hata wale wanoko wamekua na akili timamu siku hizi wanatuuliza michongo ya mtaani inapigwaje.
 
Mku
Hana nidhamu hata ukimtazama tu akiwa na JPM huwa hasimami kinidhamu.

Aliulizwa na Tido Mhando tofauti ya Jk na Magufuli akasema Jk alikuwa anatoa hela ya kazi na hafanyii Kazi Mapendelezo ya CAG lakini Huyu hatoi hela halafu anategema tufanye kazi ya kukagua mpaka ngazi ya Kata na kila sehemu anataka tukafanye Special Audit wakat budget kaikata kwa 60%![/QUOT

.

Mkuu kwa hiyo hapa shida ni ya CAG na uko fair kweli kwa hilo? Ni nani huyo anayetarajia audit ifanyike mpk level ya Kata pasipo pesa? Hapo kwenye kusimama kinidhamu siwezi kutoa hukumu kwani sifahamu kusimama kupi ni kwa kinidhamu na kupi si kwa kinidhamu
 
Anaweza kumteua tu kumfukuza hawezi!mfukuzaji anaweza kuanzisha mchakato wa kumfukuza kama Cag atakiuka maadili ya viongozi,lakini ni lazima iundwe tume ya kijaji kuchunguza tuhuma hizo na kushauri,majaji hao ni lazima wawe ni majaji wa mahamakama kuu kutoka nchi mwanachama wa common wealth.jaji yupi wa hovyo kati yao anawaza kuweka rehani weledi kumfurahisha mtu?
Umeivaa kaka katika career hii..hasa kweny auditn subject mana umetoa clarification nzuri
 
Anaweza kumteua tu kumfukuza hawezi!mfukuzaji anaweza kuanzisha mchakato wa kumfukuza kama Cag atakiuka maadili ya viongozi,lakini ni lazima iundwe tume ya kijaji kuchunguza tuhuma hizo na kushauri,majaji hao ni lazima wawe ni majaji wa mahamakama kuu kutoka nchi mwanachama wa common wealth.jaji yupi wa hovyo kati yao anawaza kuweka rehani weledi kumfurahisha mtu?
Unapotoa povu kumsafisha Lowasa waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond,usisahau pia kuwa Mh.Lowasa kazungukwa na Rostam,Karamagi na Chenge.CVs za hawa watu zinajulikana!Kwa hiyo ndugu msafishaji kumsafisha Lowasa tu haitoshi,una jukumu zito kuendelea kusafisha pia watajwa hapo juu.Tujikumbushe kidogo kauli ya baba wa taifa kuwa huwezi kuwa msafi na unazungukwa na watu wa ajabu ajabu
 
Professor Assad Atafukuzwa Muda si mrefu ana amini katika Professionalism sana.
CAG hafukuzwi kiurahisi kama unavyodhani wewe! Tupende kusoma ili tujue hata basics jamani sio kushangilia shangilia tuuuu
 
Sasa kama CAG hapewi pesa za kumwezesha kufanya kazi mafisadi si ndio watasherekea? Watakomba zo-o-te wakijua mpaka wafikiwe watakuwa wameshapata nafasi ya kuharibu nyaraka zote. Hata ukaguzi ukija kuanzwa baadaye nyaraka za kumkamata mtu hazitapatikana
 
..serikali dhalimu hii...pesa hawana wamekula hadi hela za maafa..wanajificha na kivuli cha uhakiki vyeti wakati wanawakumbatia wezi wa vyeti kina bashite...

..hela hawana wamebaki wanakimbizana na wapinzani...maana ndicho wa naweza...

..wamewakopa watumishi stahiki zao na sasa naskia wanataka kuwapa mikataba mipya watumishi walioahama...
.....aibu yao maana wamedanganya wameishiwa...na sasa wanaumbuka...hata bajeti yao waliyopitisha kwa mbwembwe wameshindwa kuitekeleza hata robo..mwaka unaisha sasa.....
 
Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imekiri kukabiliwa na ukosefu wa fedha, hali inayoathiri utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Khatibu Kazungu, wakati akijibu hotuba ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad, kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

“Ukosefu wa fedha haupo kwenu (CAG) tu, upo serikalini kote; nikubaliane na ushauri wa Prof. (Assad), kwamba tunatakiwa kujiongeza kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya serikali na kusimamia vizuri makusanyo yake,” alisema Kazungu.
Prof. Assad, alisema ofisi yake inakabiliwa na wakati mgumu kiutendaji, kutokana na serikali kuchelewa au kutoipelekea fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwenye bajeti hivyo kufanya kazi ya ukaguzi wa fedha kwenye halmashauri kuwa ngumu.

Alitoa mfano wa bajeti ya ofisi hiyo katika fungu la OC kwa Mwaka 2016/17, kwamba ilikuwa Shilingi Bilioni 18 lakini mpaka Agosti mwaka jana kiasi kilichokuwa kimepokewa hakikuzidi Shilingi Bilioni 2.

“Nililazimika kuzungumza na Mheshimiwa mwenyewe (Rais John Magufuli), kwamb bila kupata Shilingi Bilioni 10 wataalamu wasingeenda kufanya ukaguzi, akaahidi kulishughulikia
,” alieleza.

Prof. Assad, aliongeza kwamba Mwezi Septemba walipatiwa Shilingi Bilioni 5 na baadaye Oktoba wakapatiwa Shilingi Bilioni 4, ambapo wataalamu walianza ukaguzi kwenye halmashauri mbalimbali mwezi Novemba 2016. CAG ameweka bayana kuwa mpaka Februari mwaka huu baadhi yao walikuwa hawajamaliza kazi hiyo, hali ambayo ni tofauti na kawaida, ambapo Desemba hutakiwa wote wawe wamerejea kutoka kwenye maeneo ya ukaguzi, ili waandae taarifa ambayo huwasilishwa kwenye Bunge la Bajeti.

Prof Assad amesema kuwa mikoa na halmashauri zinazokaguliwa na CAG zimekuwa zikiongezeka; kutoka mikoa 25 hadi 26 na halmashauri 170 hadi 173. Pia bajeti inayowasilishwa na ofisi ya CAG Bungeni imekuwa ikiongezeka lakini kiasi ambacho amekuwa akipitishiwa na kupewa kimekuwa kikishuka kila mwaka.

Prof Assad ameweka bayana kuwa miaka mitatu iliyopita, ofisi yake ilianzisha utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wataalamu wake ili waendane na matakwa ya kimataifa, lakini sasa utaratibu huo umekwama kwa ukosefu wa fedha.
“Tumeomba msaada kwa baadhi ya nchi, ikiwemo China, zimekubali kutusaidia kusomesha wataalamu wetu kwa awamu, angalau watano watano lakini ikumbukwe hata kusafirisha mtu mpaka China na kuishi huko kuna gharama, bado serikali imeshindwa kumudu gharama hizo,” alieleza Prof. Assad
Alibainisha kuwa hata watumishi 129 walioajiriwa na ofisi hiyo, hawajapatiwa mafunzo elekezi, hali inayosababisha kufanya kazi bila ufahamu wa hakika wa taratibu za kazi zao.

Miradi ya gesi na mafuta inayoendelea kutekelezwa nchini, pia haiwezi kunufaisha taifa kwa kiwango cha kutosha kutokana na taifa kutokuwa na wataalamu waliobobea katika ukaguzi wa rasilimali hizo.

Prof Assad pia ameiomba Hazina ipeleke fedha kwa wazabuni wanaoidai serikali. Bila kutaja majina ya wazabuni wala kiasi wanachodai, Prof. Assad alisema, “Naomba Hazina mpeleke fedha zinazotakiwa kupelekwa ofisini kwetu, hawa watu walipwe na sitegemei baada ya kutoa kauli hii, nipigiwe simu au nifuatwe tena na wazabuni hawa.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Prof. Assad, mmoja kati ya wadai amesema akilipwa ndani ya mwezi huu (Machi) atapokea kiasi anachodai lakini zaidi ya muda huo, ataanza kutoza riba ya asilimia 15 ya deni hilo kwa kila mwezi.

Alisema wameshaandika barua tatu Hazina, kuhusu madai hayo bila kujibiwa; huku fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ofisi hiyo, Sh. Bilioni 8, haijapekwa hata Shilingi moja.

Chanzo: Dodoma: Serikali yakubali kukabiliwa na ukata, hali ni mbaya kiuchumi
 
Mikwala Mingi, Kauli za kibabe, kubeza waliotangulia ktongoza, mwisho wameingia Mkenge yaani kudondokea pua.
 
Back
Top Bottom