Hali ya uchumi nchini: CAG alia na ukata

Hali ya uchumi nchini: CAG alia na ukata

kubana kote matumizi pesa zinaenda wapi???
 
Naomba uniache mkuu nile mshahara wa bure,hakuna kazi ya kufanya
Hii NDIYO Hali serikalini watu wanakula mishahara ya bure kabisa, OC hakuna, fedha za maendeleo hakuna sasa mtafanya kazi gani??

Na Kwa taarifa yenu mapato ya serikali ya awamu ya tano inavunja record kabisa kila kukicha ili hali mambo serikalini hayaendi

Endeleeni kupongeza kuongezeka Kwa mapato muda NDIYO msema kweli.
 
Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imekiri kukabiliwa na ukosefu wa fedha, hali inayoathiri utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Khatibu Kazungu, wakati akijibu hotuba ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad, kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

“Ukosefu wa fedha haupo kwenu (CAG) tu, upo serikalini kote; nikubaliane na ushauri wa Prof. (Assad), kwamba tunatakiwa kujiongeza kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya serikali na kusimamia vizuri makusanyo yake,” alisema Kazungu.

Prof. Assad, alisema ofisi yake inakabiliwa na wakati mgumu kiutendaji, kutokana na serikali kuchelewa au kutoipelekea fedha zinazoidhinishwa na Bunge kwenye bajeti hivyo kufanya kazi ya ukaguzi wa fedha kwenye halmashauri kuwa ngumu.

Alitoa mfano wa bajeti ya ofisi hiyo katika fungu la OC kwa Mwaka 2016/17, kwamba ilikuwa Shilingi Bilioni 18 lakini mpaka Agosti mwaka jana kiasi kilichokuwa kimepokewa hakikuzidi Shilingi Bilioni 2.

“Nililazimika kuzungumza na Mheshimiwa mwenyewe (Rais John Magufuli), kwamb bila kupata Shilingi Bilioni 10 wataalamu wasingeenda kufanya ukaguzi, akaahidi kulishughulikia,” alieleza.

Prof. Assad, aliongeza kwamba Mwezi Septemba walipatiwa Shilingi Bilioni 5 na baadaye Oktoba wakapatiwa Shilingi Bilioni 4, ambapo wataalamu walianza ukaguzi kwenye halmashauri mbalimbali mwezi Novemba 2016. CAG ameweka bayana kuwa mpaka Februari mwaka huu baadhi yao walikuwa hawajamaliza kazi hiyo, hali ambayo ni tofauti na kawaida, ambapo Desemba hutakiwa wote wawe wamerejea kutoka kwenye maeneo ya ukaguzi, ili waandae taarifa ambayo huwasilishwa kwenye Bunge la Bajeti.

Prof Assad amesema kuwa mikoa na halmashauri zinazokaguliwa na CAG zimekuwa zikiongezeka; kutoka mikoa 25 hadi 26 na halmashauri 170 hadi 173. Pia bajeti inayowasilishwa na ofisi ya CAG Bungeni imekuwa ikiongezeka lakini kiasi ambacho amekuwa akipitishiwa na kupewa kimekuwa kikishuka kila mwaka.

Prof Assad ameweka bayana kuwa miaka mitatu iliyopita, ofisi yake ilianzisha utaratibu wa kuwaongezea ujuzi wataalamu wake ili waendane na matakwa ya kimataifa, lakini sasa utaratibu huo umekwama kwa ukosefu wa fedha.

“Tumeomba msaada kwa baadhi ya nchi, ikiwemo China, zimekubali kutusaidia kusomesha wataalamu wetu kwa awamu, angalau watano watano lakini ikumbukwe hata kusafirisha mtu mpaka China na kuishi huko kuna gharama, bado serikali imeshindwa kumudu gharama hizo,” alieleza Prof. Assad

Alibainisha kuwa hata watumishi 129 walioajiriwa na ofisi hiyo, hawajapatiwa mafunzo elekezi, hali inayosababisha kufanya kazi bila ufahamu wa hakika wa taratibu za kazi zao.

Miradi ya gesi na mafuta inayoendelea kutekelezwa nchini, pia haiwezi kunufaisha taifa kwa kiwango cha kutosha kutokana na taifa kutokuwa na wataalamu waliobobea katika ukaguzi wa rasilimali hizo.

Prof Assad pia ameiomba Hazina ipeleke fedha kwa wazabuni wanaoidai serikali. Bila kutaja majina ya wazabuni wala kiasi wanachodai, Prof. Assad alisema, “Naomba Hazina mpeleke fedha zinazotakiwa kupelekwa ofisini kwetu, hawa watu walipwe na sitegemei baada ya kutoa kauli hii, nipigiwe simu au nifuatwe tena na wazabuni hawa.”

Kwa mujibu wa maelezo ya Prof. Assad, mmoja kati ya wadai amesema akilipwa ndani ya mwezi huu (Machi) atapokea kiasi anachodai lakini zaidi ya muda huo, ataanza kutoza riba ya asilimia 15 ya deni hilo kwa kila mwezi.

Alisema wameshaandika barua tatu Hazina, kuhusu madai hayo bila kujibiwa; huku fedha zilizoidhinishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ofisi hiyo, Sh. Bilioni 8, haijapekwa hata Shilingi moja.


Chanzo: Dodoma: Serikali yakubali kukabiliwa na ukata, hali ni mbaya kiuchumi
Naibu Katibu Mkuu ni mpiga DILI mirija yake ya ufisadi imekatwa ndio maana anamwaga Povu
Ukweli nikwamba Mapato yameongeza sana
 
kubana kote matumizi pesa zinaenda wapi???
Itakuwa wanagawana Hawa wezi


J

Je CAG hataingiliwa majukumu yake na hule muhimili korofi? But ni vyema prof Asad afuate nyayo za mtangulizi wake Bw Utto L kwa heshima yake na taifa, hii ni kwa sababu kumekuwa na kuingiliwa utendaji wa taasisi za serikali hili kuficha ufisadi na uhalifu wa uchumi wa nchi
 
Namba Zinasomeka Vizuri.

[HASHTAG]#AsirudieKosa2020[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Afaa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#DaudiBashite[/HASHTAG]
 
Daaah magufuli huwa nakussuport saana ila kwa apa cjaelewa maan mapato yameongezeka sas hawa jamaa mbona wanalia pesa hawapati ya kazi..hvi bila ya hawa jamaa utajuaje sasa kam sehemu flani kuna ufisadi umefanyika.?kumchleweshea CAG pesa ya kazi tunaweza jikuta tunapoteza zaid ya hiyo tuliyochelewesha
Na wee unaaminigi zile report za TRAaaa???[emoji1] [emoji3]
 
Asihofu kuna Nchi ya Asali na Maziwa inajengwa huko Chato ikiisha hela zitaletwa kwingine.
 
Kama nimeelewa vizuri andiko, naona kama CAG analalamikia hela ya maendeleo tu ya ofc yake, kwasababu kama waliomba 18b na kati ya hizo 8b ni zamaendeleo, ili afanye kazi zake kwa ufanisi anahitaji 10b ambapo anasema mwezi mmoja baada ya badget alipewa 2b then 5b, na mwisho 4b ambazo zinafanya jumla ya 11b, sasa hapo atashindwaje kuzifikia halmashauri zote na kumaliza hata kama ni kwa kuchelea kidogo ukulinganisha na muda waliojiwekea?
Msaada please....
Hayo sio mahitaji halisi ya ofisi yake,hizo 18bill ni 40% ya bajeti alioomba maana anasema imekatwa by 60%.
 
Halafu eti anasifiwa kwa mapambano dhidi ya "RUshwa" nchi ina maigizo hii!! Unafahamuje paliopooza kwa Rushwa bila CAG kufanya kazi yake au anatumia darubini ya babu wa Koromije kupitia msukule Bashite? CCM hili janga mliliokota wapi?
 
Professor Assad Atafukuzwa Muda si mrefu ana amini katika Professionalism sana.
Kama utani hivi lakini ndio ukweli huu. Kama huna PhD ya "maganda ya korosho" na vyeti kama vya Bashite huwezi kuendana na "kasi" ya baba Killaza.
 
Siyo rahisi kama unavyofikiria!
Unafatilia Stori za Vijiweni Nimesoma katiba na anaweza kutengenezewa zengwe akang'olewa katika haijaeleza kua Controller and Auditor General ataacha/Kustaafu kazi kwa kujiamulia.
 
Ni aibu CAG kukosa fedha
www.ippmedia.com/sw/maoni-ya-mhariri/ni-aibu-cag-kukosa-fedha

Ni aibu kwa kuwa jukumu la msingi la ofisi hiyo ni kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya fedha za umma kisha kuweka taarifa hadharani.

Kwa hiyo kama haipewi fedha za kutosha na kwa wakati, maana yake ni kuwa hakuna shughuli zitakazofanyika za kudhibiti matumizi ya fedha za walipakodi.

Hayo yalibainishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad, juzi mjini Dodoma wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo.

Alisema ofisi yake huhitaji Sh. bilioni 10 kwa ajili ya uendeshaji, lakini haijapata licha ya kupeleka maombi serikalini.

Kwa mujibu wa Profesa Assad, Sh. bilioni nane huhitajika kwa matumizi ya kawaida ya kila mwaka, ikiwamo kuwapeleka wakaguzi kwenye mafunzo ya ukaguzi ya kimataifa.

Alisema kutokana na kutopatiwa fedha hizo hadi sasa, kazi zao za kila siku zimelala, ikiwamo kushindwa kuendelea na ujenzi wa ofisi zake katika mikoa kadhaa.

Kadhalika, ofisi hiyo imeshindwa hata kupeleka wakaguzi katika mafunzo ya ukaguzi wa kimataifa, kutokana na ukata huku akieleza faida za mafunzo hayo kwa wakaguzi kuwa ni kuepuka kudanganywa kila uchao kwa kuwa watakuwa na wakaguzi wa kimataifa kutoka nchini.

Tunakubaliana na kuunga mkono jitihada za serikali za kubana matumizi yake, lakini tunaona kuwa kutokana na umuhimu mkubwa wa Ofisi ya CAG, ipewe kipaumbele kwa kupewa bajeti ya kutosha na kwa wakati mwafaka ili itekeleze makukumu yake ya kila siku kwa tija na ufanisi.

Ukweli ni kwamba Ofisi ya CAG ina majukumu mengi kila siku lengo likiwa kutoa huduma bora za ukaguzi zenye kuleta tija kwa nia ya kuimarisha uwajibikaji ili kupata thamani ya fedha katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma.

Ofisi hiyo imekuwa ikifanya ukaguzi wa taarifa za fedha kwa kipindi chote cha mwaka unaoishia kila Juni 30 katika taasisi za serikali zaidi ya 400 na mamlaka za Serikali za Mitaa hususani halmashauri 185 yakiwamo majiji 5, manispaa 21, miji 22 na wilaya 137.

Hii ni kazi kubwa na yenye changamoto kubwa inayohitaji rasilimali watu na fedha za kutosha, hivyo anachokisema Profesa Assad kina ukweli kwa asilimia 100.

Umuhimu wa ripoti ya CAG ulianza kuonekana kwa watu wengi katika miaka ya karibuni kuanzia uongozi wa Ludovick Utouh, kutokana na kubainisha madudu mengi ya kifisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma. Ripoti hiyo ilichangia kuwang’oa mawaziri kadhaa mwaka 2012.

Mbali na ukaguzi wa CAG kuibua wizi wa fedha taslimu, lakini pia umekuwa ukitumika kubaini kama miradi ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa inatekelezwa kwa kutumia fedha halisi (value for money.

Kwa kuwa serikali ya Rais John Magufuli inajipambanua kwa kupambana na rushwa na ufisadi, haitakuwa sahihi kama itatekeleza majukumu yake bila kuipatia Ofisi ya CAG fedha za kutosha na kwa wakati. Bila hivyo itashindwa kumsaidia kufuatilia matumizi ya fedha za umma na matokeo yake ajenda ya serikali itakwama.

Sisi tunaona kwamba siyo vizuri CAG kulalamikia ukata hadharani, badala yake serikali iwapatie haraka fedha wanazozihitaji ili waanze kugharamia vitu ambavyo vina uhitaji wa haraka, vinginevyo itakuwa aibu kwa chombo hicho kukwama kutekeleza majukumu yake kutokana na ukata.
 
Magu hawezi kumpa CAG bil 10 halafu aumbuke kwamba matumizi yake hayazingatii bajeti.
 
Back
Top Bottom