Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

Wengi wenu ni halal yenu! Mnafika kazini saa 4 halafu dk 10 zikipita eti mnaenda kunywa chai..mkitoka huko kazi ya kwanza ni kusoma magazeti kabla hamjaanza mishemishe za lanchi. Toeni upuuzi wenu hapa, ala!
 
Kuna jamaa humu ndani asiyependa lugha ya serikali imefilisika.. Labda angeshauri lugha gani itumike. Kama una shughuli zako za kimaendeleo.Mfano,saluni,mgahawa,stationery,n.k.Na una wafanyakazi kama 9 wa kuwalipa kila mwezi.Tena umejipangia kila siku ama tarehe ya mwisho ya kila mwezi ndipo unawalipa. Ikatokea ukachelewa kwa siku 2 au 3,ndipo unalipa wafanyakazi wako,nao hawana tabu wanajua watalipwa. Sasa siku itokee ucheleweshe kwa siku 10,nina hakika siku ya 5 tu watakugongea kukuuliza kulikoni....Hivi jibu la kawaida la kutuliza munkari huwa ni lipi? Si utasema,mambo SI MAZURI,ila mtapata mishahara yenu?! Maana kama uwezo unao ungelipa tu.. Kifupi serikali inachacha kutokana na kutokuwa na vipaumbele sahihi..
 
Kwa mawazo uliyo nayo, kamwe hutaweza kuona kitu kizima hivi ambacho ndicho serikali. TRA ni kama TCRA. Je TRA pia inapokea ruzuku kutoka serikalini? Kwa taarifa yako ukusanyaji mapato kwenye kampuni za simu siyo kitu rahisi kama vile kulipa kodi ya pango TRA. Kunahitajika utaalamu wa hali ya juu na watu wenye wataalamu na vyombo vya kudhibiti mianya ya kukwepa kodi ni TCRA. Upo?
Huo ndiyo upuuzi wetu waafrika. Eti ''utaalam wa hali ya juu''!! Wa hali ya juu unatoka sayari gani? Mbona nchi zingine zimeweza!! Ndiyo maana akina Camerun wameamua kutufundisha adabu. Hela zipo mikononi mwetu lakini tunashindwa kuzikusanya na kutumia.
 
Wengi wenu ni halal yenu! Mnafika kazini saa 4 halafu dk 10 zikipita eti mnaenda kunywa chai..mkitoka huko kazi ya kwanza ni kusoma magazeti kabla hamjaanza mishemishe za lanchi. Toeni upuuzi wenu hapa, ala!

Sasa tatizo hilo ni la in charge,supervisor,HR officer,MD,DED,yaani ni usimamizi mbovu wa hiyo ofisi husika. Utamlaumu vp kila mtumishi wa serikali?
 
Sasa tatizo hilo ni la in charge,supervisor,HR officer,MD,DED,yaani ni usimamizi mbovu wa hiyo ofisi husika. Utamlaumu vp kila mtumishi wa serikali?
Ukweli ni kwamba pool ya labor force ya Tz ni kituko. Output hamna. Nod maana wawekezaji wengine wapo radhi kumpa mkenya mshahara wa 5 mil kwa mwezi kuliko kumpa mbongo laki 5 kwa same job description, maana anajua mbongo ataharibu. Wengi wenu ni wavivu na wazembe halafu ndio wa kwanza kudai chenji.
 
hakuchaguliwa, aliteuliwa na tume ya uchaguzi na usalama wa taifa kupitia process iliyokuja julikana kama chakachua-gate

Mliimchagua wenyewe huyo JK last year, subirini mnae huyo hadi 2015. Mtavuna mlichopanda
 
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!

Huku sekata binafsi ukiacha makampuni ya kihindi na family business; makampuni mengi hutoa mishahara ijumaa ya mwisho ya kila mwezi. Mfano hapa kwangu walipata jana tarehe 25.11.2011

 
Dr Dr Dr Dr Dr Dr Dr Lieutenant Jakaya Mrisho Kikwete! a.ka Baba Riz1 wala hana tatizo wafanyakazi nyie subirieni tu mtapata ila nawashauri mkicheleweshewa sana gomeni kwani mtakuwa hamna nauli za kuwapeleka maofifi kwenu etc.
 
Mkiambiwa muwe wajasiriamali hamtaki sasa mtajuta kumfhamu kikwete, wanacho fanya kwa sasa ni kutoroshea nje ma trilioni ya fedha kabla mambo hayajawa mabaya
 
tatizo kubwa la serikali yetu ni kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi wenye tija ndogo,kwanza kuchelewa kazini saa 3.5 halafu kwenda kwenye supu 4 kazi kidogo na miseni town nyingi,usishangae jairo anabeba wafanyakazi zaidi ya 200 kwenda dodoma kupitisha budge ya wizara yake ndogo.kwa mfano kuna mamlaka moja iko chini ya wizara nyeti ina wafanyakazi wengi kwenye karakana zake ambao hawafanyi kazi zozote,kila gari au mtambo wa serekali ukipelekwa hapo huishia kwenye karakana binafsi, wafanyakazi wana ripoti na kwenda kwenye shughuli zao binafsi,kama mataifa tajiri kama marekani yanajaribu kupunguza ukubwa wa serikali zao kwanini tanzania isifanye hivyo???kumbuka mkono mtupu haulambwi
 
Nakubaliana na wewe kwamba kufilisika ni mchakato!!! Hata hivyo, point yangu ni kwamba, mimi nimeshahusika sana na suala hili la mishahara wakati nipo benki fulani miaka michache iliyopita. Fluctuation ya tarehe za kulipa mishahara haijaanza leo, hivyo ikiwa fluctuation hiyo ndio dalili ya kufilisika basi ingekuwa tumeshafilisika zamani. Mkuu, asikuambie mtu; kufilisika sio kitu rahisi kiac hicho. Inawezekana, lakini ktk mazingira ya sasa bado sana na hakuna indicator ya kufilisika.....suala la kuchelewa mishahara wiki moja au mbili bado sio kigezo cha kufilisika.Kuna wakati fulani nilikuwa nahusika na posting ya mishahara ya TAZARA, ilifikia wakati una-post mshahara November kumbe ndo mshahara wa September huo!!!!! Je, sisi (kwa maana ya TZ gvt) tumekaribia huko?!

Mkuu, kama unadhani indicator ya serikali kufilisika si kucheleweshewa mishahara watumishi wa umma basi kwako ni kigezo gani? Tatizo hapa si fluctuation ya mishahara, bali hoja ya kufilisika inachagizwa na serikali kukopa fedha TCRA, Stanbic, CRDB na kwingineko ili kulipa mishahara. Kama kweli hivyo ndivyo, those are indicators of a collapsing govt financially, which may lead to bankrupcy. Hoja ni kwanini serikali ikope kwa ajili ya kulipa mishahara?
 
Wengi wenu ni halal yenu! Mnafika kazini saa 4 halafu dk 10 zikipita eti mnaenda kunywa chai..mkitoka huko kazi ya kwanza ni kusoma magazeti kabla hamjaanza mishemishe za lanchi. Toeni upuuzi wenu hapa, ala!

Sidhani kama umetumia busara kuzungumza maneno hayo! hao uliowaona wanafanya hivyo si justification ya Watumishi wote wa umma ndivyo walivyo. Kwa taarifa yako kuna watumishi obedient ambao wanajua saa ya kuingia kazini tu, saa ya kutoka hawaijuwi! wanafanya kazi isiyolingana na mishahara yao tena kwenye mazingira magumu. Waangalie madaktari, manesi, madereva, waalimu etc... kuna wafanyakazi wa umma ambao wana miezi kadhaa hawajalipwa stahili zao kama vile likizo, uhamisho n.k. Unaongea kama unaishi sayari nyingine? yet mtumishi wa umma ndiye mlipa kodi mkubwa wa nchi hii, maana anakatwa juu kwa juu kodi yake ya 20% atake asitake! tofauti na wafanyabiashara wenye kuingiza mabilioni ya fedha huku wakikwepa kodi na kushirikiana na mamlaka husika kukwepa kodi, au kupata exemption lkn ukweli wanaiibia serikali. Wahurumie wafanyakazi wa umma ktk halmashauri mbalimbali ambao mishahara yao hucheleweshwa na pengine kukatwa kiholela. Please, think big!
 
Lakini mbona jeshini hakuna upuuzi wa kucheleweshewa mishahara?. Sijui polisi na magereza lakini JWTZ hakuna upuuzi huo kabisa.
 
Back
Top Bottom