Maendeleo ya Kilimanjaro hayakuja bila involvement ya serikali, ama ya kikoloni au baada ya ukoloni. Kuendelea kwa Kilimanjaro haina maana kuwa Kigoma hawana maendeleo, tofauti ni kasi ya maendeleo na kukosekana kwa miundo msingi huko Kigoma. Miundo msingi popote pale ni jukumu la serikali, miundo msingi ndio kichocheo cha maendeleo ktk sehemu husika, miundomsingi haiwekwi na watu binafsi bali serikali.
Kigoma hawana barabara ya lami kuwaunganisha na mikoa mingine ili hali wanazalisha chakula cha kutosha na ziada, Kigoma wanategemea reli ya Mjerumani ambayo imechoka kwa ajili ya kusafirisha watu na bidhaa wanazozalisha (hapo treni ikikosekana bila shaka utawataka wanunue vichwa vya treni, mabehewa na kuwataka waikarabati reli!), Kigoma hata hiyo reli ya SGR wamenyimwa (kumbuka hawana barabara za lami na treni isipokuwa ndege tu ambayo usiku haiwezi kutua!)
Lakini najiuliza, bidhaa gani ambazo sio za viwansani zinazalishwa Kilimanjaro na kuwaongezea kipato ambazo Kigoma hawana? Mazao yote ambayo Kilimanjaro wanayo, Kigoma pia yapo! Sasa jiulize: kwa nini saruji inayouzwa Tsh. 14,000/- Kilimanjaro, Kigoma inauzwa kwa Tsh. 19,000/-? Kwa nini mabati yanayouzwa Kimanjaro Tsh. 20,000/-, Kigoma wananunua kwa Tsh. 24,000/-? Hata dizeli na petroli Kigoma inauzwa bei kubwa kuliko sehemu yoyote Tanzania! Sukari, Kilimanjaro mnanunua Tsh.1,400/- wenzenu Kigoma wanauziwa 1,800/.-Kila bidhaa ya kiwandani Kigoma inauzwa kwa bei kubwa kuliko sehemu yoyote Tanzania wakati kiwango cha mishahara ya waalimu waliopo Kigoma kinalingana na waalimu walipo Kilimanjaro na kwa mshahara huo huo unategemea mwalimu aliyeko Kigoma ajenge nyumba nzuri kama ya mwalimu aliyepo Kilimanjaro na unamshutumu mwalimu aliyeko Kigoma kuwa mzembe. Jaribu kuwa objective ndugu yangu.
Vv
Vv