Hali ya kiasiasa joto na mvuke katika mchakato wa uchaguzi 2024-2025

Kisesetusese

Senior Member
Sep 12, 2022
173
242
Nielekee kwenye mada.

Naona mambo yanaendelea na joto linaendelea kukolea. Katika chama cha Mapinduzi kile kiitwavyo uhuru wa kugombea utaleta doa kwa wale wasiokubaliana na Mama. Wanauhuru kugombea na Mama lakini haiwezekani kujitokeza hadharani.

Hawa watafukia vichwa vyao ardhini hadi 2030. Mvuke hautawaacha wataonesha vichwa vyao kunako 2029 pale watakapo ona Mama hana nia ya kuendelea na kwa kuwa Mh Mama yetu ni Muumini na Mfano kwetu hatapenda tena mivutano. Atatulia. Japo hataacha kuwa na wa kumuandaa.

Turejee 2025. Wabunge, madiwani nakadhalika wanachuana sana. Joto litakuwa kali sana Mama hatataka ushenzi. Vijana waliobebwa 2020 wataanguka sana. Naibu Mwana fa hatarudi, ni mfano mdg tu, kama ambavyo majina ya Boss wa Diamond watakavyopotezwa.

Ni imani kwamba bunge litajaa vijana wapambanaji Mama atapata safu cream 2025. Atapata mawaziri mfano wa waziri wa tamisemi hana mbambambai. Na hapo nchi itakuwa na mvuke tu. Wale waliotumbukiza vichwa ardhini wataendelea kuviacha huko japo tutaishi nao kimwili wakisubiri 2029.

Ni watu wabaya sana. Wanamchezea Mama. Waziri wa fedha inakuaje sukari inaadimika. Wewe kama waziri na waziri wa viwanda mnajitenga wapi kujua uzalishaji taifa kubwa hili sukari ipotee. Are you waziri listeto yourself???

Umeme unakatikaje wakati mvua zinanyesha? Kwa nn maji mabomba yamekauka. Hivi wewe waziri wa maji unajielewa.? Au unamkataba na wauza maji magari yanaposhana mtaani?? Mulimtua Mama ndoo sasa mmeirejesha??

Waziri wa elimu, hivi inakuaje awamu zote hazija ufumua mtaala, mnaufumua leo mnatafuta nini

Tuendelee kusubiri Joto likipanda
 
Joto lipande kwa mazingiya haya ya katiba mbovu na tume inayoteuliwa na mwenyekiti wa ccm. Uchafuzi wa 2020 ulikuja kuweka mipaka ya wananchi wengi kuendelea kushiriki kwenye chaguzi za kihayawani. Hakuna tume huru ya uchaguzi, hakuna anayejitambua ataendelea kushiriki huo ushenzi uitwao uchaguzi.
 
Joto lipande kwa mazingiya haya ya katiba mbovu na tume inayoteuliwa na mwenyekiti wa ccm. Uchafuzi wa 2020 ulikuja kuweka mipaka ya wananchi wengi kuendelea kushiriki kwenye chaguzi za kihayawani. Hakuna tume huru ya uchaguzi, hakuna anayejitambua ataendelea kushiriki huo ushenzi uitwao uchaguzi.
Kwa sasa hata makonda ana afadhari
 
Joto gani wakati uporaji wa Uchafuzi umeshaandaliwa.

Joto liko kwenye CHAGUZI HURU NA HAKI.
 
Back
Top Bottom