Hali ya Barabara Didia – Solwa eneo la Ndagwa, Kijiji cha Kasingili, Kata ya Ilola inaumiza Wananchi

Hali ya Barabara Didia – Solwa eneo la Ndagwa, Kijiji cha Kasingili, Kata ya Ilola inaumiza Wananchi

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
161
Reaction score
200
Screenshot 2026-02-20 191055.jpg

Screenshot 2026-02-20 191027.jpg
Screenshot 2026-02-20 191007.jpg

Diwani wa Kata ya ILOLA, KISENA FRED KISENA amelazimika kuchelewa kwenda kwenye hitimisho la ziara ndani ya kata kutokana na ubovu wa miundombinu ambapo ilimlazimu kuanza kuvusha watoto wa shule kwenye maji ambao walihofia kusombwa na maji ndipo akaanza jukumu la kuwavusha kwenye maji kwa kutumia pikipiki.

Barabara hii ya Didia - Solwa imekatika kwa maji na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hii.

Lakini pia wakati akiendelea kuvusha watoto wa shure ilimlazimu kuanza kusaidiana na wananchi kukwamua bajaji zilizokuwa zimekwama kwenye dimbwi hilo kwa kuingia kwenye maji hayo na kuanza kusukuma pamoja na wananchi na kuzivusha bajaji hizo zilizokuwa zimebeba mpunga kuelekea Didia mahala ambapo kuwa viwanda vya kuchakata mpunga.

Akizungumzia jambo hilo, ametoa wito kwa TARURA kuliangalia dibwi hilo kwa jicho la pekee huku akishauri kuwa hatua zichukuliwe kuweka daraja katika eneo hilo ili kutoathiri shughuri za uchumi kwa wafanyabiashara kwa kuwa barabara hiyo ya Didia - Solwa ni muhimu sana kwa uchumi wa Wilaya ya Shinyanga DC.

 
Ilola kwa akina Mwanamembo, Hiyo njia inafaa sana iwekwe Mkeka iende hadi salawe misasi then Misungwi
 
Back
Top Bottom