Mkuu mtu kama wewe ndo wa kuja ulaya hasa Norway na Denmark. Tatizo waliopata iyo fursa hawapendi kufanya kazi. Kina kazi nyingii sana huku. Kuna dogo kaja huku mwaka jana yeye kulala. Mimi nina miaka 15 huku napiga mzigo sichagui kazi. Mwezi wa tano nilifanya kazi masaa 500. Dogo yani analala tu hela iko njenje. Kuna mzee ni besti yangu ana gerej toka 1970s anatoa vibarua na kukulipa cash in hand baada ya kazi kama elfu 70-80 kwa saa. Dogo nikampeleka kufanya yani masaa mawili tu kachoka anatoroka anaenda kulala. Halafu mizinga sasa ameanza kuishi kijanja visa ilishaisha.