Hali ni tete

Victor MG

Member
May 25, 2023
48
70
Hali yangu sio shwari. Kazi ndio hivyo najaribu kuomba hata vibarua lakini ni za manati.

Nasubiri tu vibarua vya kulima vikianza nijitose sina namna. Muda mwingine nakosa hata hela ya vocha kweli?

Najutia sana ile bidii niliyoweka huko kwenye elimu ningewekeza hata kwenye skills zingine ningekuwa mbali sana. Nakatiza mtaa au sometimes sitoki home kabisa.

Maana hata kampani yenyew ya vijana wenzangu hapa mtaa sio kabisa kutokana na matukio ya ulevi , wizi wa bike, bangi n.K.

Wanayo engage nayo Sikutegemea kwamba nitakuja kuishi maisha ya stress na dhiki kiasi hiki.

Simwombei mtu akose kazi maana joto lake nalionja. Na nishasema kuomba msaada kwa ndugu never.

Nimesimangwa sana kwa kweli inatosha.
 
Huwaga yanapita,ila uwe na mvimilivu tu maana inaweza chukua muda mrefu kupitia hapo...Ila kumbuka hapo ndio unatengenezwa kuwa Bora zaidi.

Hapo ndio unajifunza watu sahihi kwako, hapo ndio unatengenezwa kuheshimu kila mtu, hapo ndio unatengezwa kuwa hard worker.

usichoke kupapasia,fanya kama upo kwenye chumba chenye giza endelea kupapasa utakutana na ufa siku Moja unaingiza mwanga,hiyo ndio break through yako....Yesu akutunze
 
Pole sana ndugu katika kipindi hiki cha mpito.
Counselling ingekufaa zaidi
shukrani sana maana dah. Hata wale niliowapiga tafu kwa namna moja au nyingine. Nikiwacheki wanipige jeki nao wana majukumu ya kifamilia . Wengine ndio hivyo wamepandisha vioo.

Nikaona ntazidi kujichoresha kwa watu tu yaani nimeamua kusubiri wakati wa mungu sina ujanja kwa kweli.
 
shukrani sana maana dah. Hata wale niliowapiga tafu kwa namna moja au nyingine. Nikiwacheki wanipige jeki nao wana majukumu ya kifamilia . Wengine ndio hivyo wamepandisha vioo. Nikaona ntazidi kujichoresha kwa watu tu yaani nimeamua kusubiri wakati wa mungu sina ujanja kwa kweli.
Shukrani sana be blessed kwa counseling.
 
Ukimaliza chuo hicho ni kipindi huwa kipo tu akiepukiki usione watu wanangaa road huko ukazani hawajapitia hayo maisha uliyonayo ni siri tu mkuu, wewe jishikilie na usimame kiume mambo yatajiset fresh kikubwa toka ndani usilale, na kukata tamaa take it easy.
Lakini pia usikomae na professional yako nenda hata kwenye mahotel makubwa omba kazi huko unaweza pata hata usafi au zaidi

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu, ungoje wakati wa Mungu huku ukiomba bila kuchoka, ukiamini na ukiwa na matumaini kwamba it’s just a matter of time.

Wanasema hakuna usiku usiyokuwa na asubuhi. Keep on keeping on.
 
Ukimaliza chuo hicho ni kipindi huwa kipo tu akiepukiki usione watu wanangaa road huko ukazani hawajapitia hayo maisha uliyonayo ni siri tu mkuu, wewe jishikilie na usimame kiume mambo yatajiset fresh kikubwa toka ndani usilale, na kukata tamaa take it easy.
Lakini pia usikomae na professional yako nenda hata kwenye mahotel makubwa omba kazi huko unaweza pata hata usafi au zaidi

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
naam nimekuelewa
 
Hali yangu sio shwari. Kazi ndio hivyo najaribu kuomba hata vibarua lakini ni za manati. Nasubiri tu vibarua vya kulima vikianza nijitose sina namna. Muda mwingine nakosa hata hela ya vocha kweli? Najutia sana ile bidii niliyoweka huko kwenye elimu ningewekeza hata kwenye skills zingine ningekuwa mbali sana. Nakatiza mtaa au sometimes sitoki home kabisa.Maana hata kampani yenyew ya vijana wenzangu hapa mtaa sio kabisa kutokana na matukio ya ulevi , wizi wa bike ,bangi n.K. Wanayo engage nayo Sikutegemea kwamba nitakuja kuishi maisha ya stress na dhiki kiasi hiki. Simwombei mtu akose kazi maana joto lake nalionja. Na nishasema kuomba msaada kwa ndugu never. Nimesimangwa sana kwa kweli inatosha.
Mkuu mtu kama wewe ndo wa kuja ulaya hasa Norway na Denmark. Tatizo waliopata iyo fursa hawapendi kufanya kazi. Kina kazi nyingii sana huku. Kuna dogo kaja huku mwaka jana yeye kulala. Mimi nina miaka 15 huku napiga mzigo sichagui kazi. Mwezi wa tano nilifanya kazi masaa 500. Dogo yani analala tu hela iko njenje. Kuna mzee ni besti yangu ana gerej toka 1970s anatoa vibarua na kukulipa cash in hand baada ya kazi kama elfu 70-80 kwa saa. Dogo nikampeleka kufanya yani masaa mawili tu kachoka anatoroka anaenda kulala. Halafu mizinga sasa ameanza kuishi kijanja visa ilishaisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom