Emanuel Makofia
JF-Expert Member
- Jan 5, 2010
- 3,832
- 631
baada ya kutoridhishwa na bajeti ya nishati na madini vurugu zimeshaanza mitaa ya Magomeni, Soko kuu na Coco beach Pande za mtwara ....
nimetulia ndani naskizia mabomu yanavurumishwa ...
for more updates stay tuned ....
Nahisi kama mapinduzi ya ukombozi wa nchi hii yataanzia Mtwara!
wengi
wenu mnaowapa sapoti watu wa Mtwara wala hamuishi Mt,yaani mpo nje ya
Mtwara,sasa nyie wanamtwara jidanganyeni tu eti mnaandamana mkidhani mpo
wengi!kwanza wengi wenu mna comment mkiwa ndani ya nyumba zenu,ndio
isitoke kweli?HAMUNA AKILI NYIE.
hv mnashindwa hata kujiuliza,ni sehemu gani Tanzania raia waliwazidi
askari ktk mapambano?..KUMBE MNAFANYA MIZAHA NA SMG,Madhara yake
mutayajua kesho kwenye misiba mtakapoo waona watoto wanalalamika kufiwa
na wazazi wao,nani atawalea?
acha utoto,
nguvu ya umma siku zote hailinganishwi na askari. Asikari wenyewe
hawafiki hata laki mbili wa majeshi yote. Je utalinganisha na raia zaidi
ya milion 30 wenye uwezo wa kupigana? nyie ndo mnawapa watu hasira na
baadae watu wakiamua kufanya kweli mnabakia kuwayawaya Unafikiri misri,
tunisia na kwingineko kulikuwa hakuna askari ? jifunze busara na si
zarau za kitoto hizo zinazoweza kuleta
madhara makubwa .
Nimehabarishwa jengo la CCM Wilaya ya Mtwara linateketezwa kwa moto.
Sababu za vurugu:
1) Kukatishwa kwa Matangazo ya TBC 1 ili watu washindwe kuona Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Hiyo ilitokana na vipeperushi vilivyokuwa vinasambazwa mkoani Mtwara vya kuhamasishana watu wasiende makazini ili kuangalia Bajeti ya Wizara hiyo ikisomwa siku ya leo.
2) Wananchi wanalalamika ya kuwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo haina faida kwao kwani haijaonyehsa kutatua matatizo ya gesi mkoani Mtwara.
Je, TBC 1 mna maana gani kukatisha matangazo kwa watu wa Mtwara?
Mmefanya hivyi ili iweje? Je, wananchi wa Mtwara hawana haki ya kuona matangazo ya Televisheni?
Kuna siri gani kwenye Hotuba ya Wizara ya Nishati?Tuwe waangalifu..TV ni ya Umma na si ya watu wachache.
Na inaendeshwa kwa kodi za Watanzania.
Nawasilisha.
kwa jinsi wana mtwara walivyodanganyika, hata kama serikali itaamua kumjenge nyumba kila mtu na kumpa mtaji wa biashara, hawatakubali. wamedanganyika kweli. hivi kwa ile speech ya leo ya waziri wa nishati na madini kulikuwa na sababu kweli ya wana mtwara kuleta fujo? au kwa vile ndo hawajaisikiaSerikali Mtwara haipo kwa sababu mkuu wa mkoa angejitokeza na wananchi wakakaa kwenye uwanja wa wazi wasikilize wote hotuba ya waziri wa nishati na madini ,ili kwa pamoja weka usalama wa mtwara sasa serikali mtwara imejificha imeacha jeshi la polisi wameteka mji wanadhani wananchi watakubali hawawezi kukubali
Unashangaa hilo mbona Masasi walichoma ofisi ya Halmashauri, magari yaliyokuwepo mpaka jengo walilokuwa wanatumia manesi wanafunzi kama hosteli. Haya na manesi wanahusika vipi hapo?kwa nini sasa jengo la ccm lichomwe moto? hawa watu wana malengo gani?
kwa nini sasa jengo la ccm lichomwe moto? hawa watu wana malengo gani?