Hali ni mbaya

mseseve

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
511
88
Nadiriki kusema hali ni mbaya sana kwa Taifa letu huko tunakoelekea ni wapi? Watu sasa hivi hawawaogopi tena viongozi wao wanafikia hatua ya kujaribu hata kumpiga mkuu wa wilaya?

Uko wapi utu wetu na heshima yetu kama watanzania! Kwa kweli kilichotokea Igunga mimi binafsi ijaunga mkono na hata sintosita kutofautiana na mtu yeyote yule anayediriki kumdhalilisha kiongozi yeyote hata kama ni wa ngazi ya chini.

Ndiyo basi natuseme ni kiongozi wa wilaya wameweza kumdhalilisha huyo watashindwa je huko tuendako kuja hata kumfanyia vivyo hivyo mkuu wetu wa nchi?mimi binafsi siungi mkono kile alichotaka kufanya likini sio kujichukulia sheria mkononi kumdhalilisha mkuu wetu wa wilaya tena mbele ya watoto wake.

JAMANI TULIANGALIE HILI LA MAADILI TUNAELEKEA WAPI?

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Ndugu yangu uhuru wa kidemkrasia uliotolewa umeangukia mikononi mwa wahuni ambao sasa wanautumia vibaya. Hakika vitendo hivi vikichekewa kesho tutasikia Waziri Mkuu au Rais amevamiwa na kudhalilishwa.

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,272
4,663
Wewe ni mnafiki, kwani DC alitaka kufanya nini?, umesahau kuwa alikuwa ktk kazi zake za kawaida?, - hili tuna ushahidi nalo na kama unajingine tujuze.
Nadiriki kusema hali ni mbaya sana kwa Taifa letu huko tunakoelekea ni wapi? Watu sasa hivi hawawaogopi tena viongozi wao wanafikia hatua ya kujaribu hata kumpiga mkuu wa wilaya?

Uko wapi utu wetu na heshima yetu kama watanzania! Kwa kweli kilichotokea Igunga mimi binafsi ijaunga mkono na hata sintosita kutofautiana na mtu yeyote yule anayediriki kumdhalilisha kiongozi yeyote hata kama ni wa ngazi ya chini.

Ndiyo basi natuseme ni kiongozi wa wilaya wameweza kumdhalilisha huyo watashindwa je huko tuendako kuja hata kumfanyia vivyo hivyo mkuu wetu wa nchi?mimi binafsi siungi mkono kile alichotaka kufanya likini sio kujichukulia sheria mkononi kumdhalilisha mkuu wetu wa wilaya tena mbele ya watoto wake.

JAMANI TULIANGALIE HILI LA MAADILI TUNAELEKEA WAPI?

Mwendabure

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,138
1,030
Ni wazi wimbo wa nidhamu umekosa muitikiaji, kwa kuwa muimbaji hana nidhamu kwa waitikiaji... Imegundulika!

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,881
1,124
We msesewe wa kuchachusha mbege,hili tumeshalisemea sana hapa kuwa bomu walilolitega viongozi wa nchi hii litajulipukia wote,nchi imekuwa haina uongozi ni kama kambale kila mmoja sharubu.walitupa miiko ya uongozi leo rais anabangaiza biashara ikulu.vyama vya siasa havina heshima kwa rais na viongozi waandamizi wa serikali sasa ukikimbilia kulaumu vyma ni kosa.
Kuna usemi wetu unasema ukikuta mtoto anatoa matusi barabarani ujue wazazi wake wako hivyo.mbopo nae anashabiki kuangalia mahali tunapo angukia badala ya tulipojikwaa.sishabikii kiongozi yeyote yule kudhalilishwa ila sitaki ubaguzi haki itendeke akidhalilishwa mbunge wa cuf tupinge kwani ni mwakilishi wa wananchi,tuache ushabiki wa vyama kwani vyama vingine vimeshazeeka vinataka kujifia tuviweke pembeni vipumzike kama vimejiwekea pensheni viitumie kama vilichezea maisha visubiri hukumu ya wananchi.

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
28,386
26,776
Nidhamu gani unayozungumzia wewe?
Nifhamu haitakiwi kua ya upande mmoja tu,
Huyo bibi na aliemuweka wote wayayushaji tu, unategemea wapewe nidhamu ili iweje?
Au unazungumzia nidhamu ya uoga?
Anza kwanza wewe kuwaheshimu wanajamii hapa kwa kutoleta tuhuma za kizushi zisizo na kichwa wala miguu!!

Dr Kingu

Senior Member
Jun 13, 2011
154
43
Mkubwa jiheshimu na mdogo atakuheshimu. Viongozi wetu wa nchi hawana maadili ya uongozi, je wanaoongozwa wafanyeje? Hivi huyo Dc kaanza kuvuruga mkutano wa cdm kumbe wamchekee tu? Wote wana makosa. Hivi mbowe,slaa, tundu lisu au lema wakichaniwa nguo na polisi wakiwa wanapakizwa kwenye lori tena wakiwa wanafanya mikutano halali mbona mnafurahia? Kwani hao sio binadamu ambao utu wao inapaswa kuheshimiwa? Hao viongozi vilaza wakiongea upupu lazima tuwazomee kuonyesha tumechoshwa na ufisadi wao. Unajua hata kama tembo kakukanyaga sisimizi ukipiga kelele atajua kumbe naye anajua kuwa namkandamiza.

0 Reactions
Reply
Top Bottom