Hali ni mbaya sana ya mungano.

Hali ni mbaya sana ya mungano.

Vyovyote iamuliwe,lakini lazima tuwe na Tanganyika yetu, katiba yetu,na mambo yetu...!
 
ufe tuu ahh tumechoka
mi najiuliza sna kwanini wapemba hawataki mungano japo wanafanya biashara sana huku bara yani wapo tayari hatakupigana na huwa wanatukana sna
wakisikia mtu anautetea.sasa kwann tulazimishwe kuungana na hawa watu?
 
Watanzania bara wanaosema ngoja muungano uvunjike, Zanzibar mtakosa hiki na kile.
Tujiulize ni wao ndio wanautaka huo muungano? sisi Tanzania bara ndio tunang'ang'aniza usivunjike.

Tanzania visiwani wameshaonyesha nia ya kutoutaka, wachague kuuvunja tu. Kwani sisi woga wetu ni nini hasa?
Watabaki kuwa majirani kama wengine, mambo ya kung'ang'aniza Muungano na watu wasioutaka nafikiri kuna mifano mingi.
 
Teh teh teh zanzibar vunjeni basi huo muungano fasta muone kitakachofuata.chakula hamlimi hivyo mtalipa dola,umeme mtalipa dola, uraia fasta mtatulipa dola maana lazima mje kucheki msosi,vyuo vikuu mtakuja kusoma kwa dola, bila shaka askari wetu watakuja kulinda amani maana mnavyobaguana lazima mpigane hivyo makamanda wetu watalipwa dola,zile nafasi 1000 wanazopewa waznz katika vyuo vikuu watapewa watanganyika,lazima mtarudisha mashamba yote mnayomili huku bara yaani pesa yenu itakuwa ya mugabe.wembe mkali
Wewe unastahili kuitwa kolokoloni, mimi si muumini wa muungano, lkn hoja zako ni za kipuuzi, suala la kununua vyakula na bidhaa nyingine ni la kibiashara, si lazima wanunue kutoka kwetu tanganyika, wanaweza kuagiza kutoka china, india, na kwingineko ambako ni rahisi zaidi
 
Acheni hizo habari za kuvunja muungano....father mzanzibar wa kule pemba na mother ni mzigua wa pale tanga sasa mkiuvunja muungano ss wengine itakuwaje....
 
Waznz eti wanataka kuvunja muungano ili wawe matonya wa kujitegemea.....!! Teh teh teh teh umatonya sasa umeshaanza kuwa tatizo maana lazima kwanza muugubali ushoga na lazima mtaukubali tu maana hakuna cha kuzalisha znz useme mtajibu nyodo kwa hao wahisani. Ila msisahau kutengeneza sarafu yenu ili ty tujitengenezee dola chap chap. Mlitaka wenyewe chai iweje mnalalamika mnaungua?. Kwa kuwaonea huruma tu tunataka tanganyika yetu mkiendelea na kelele tunavunja kabisa muungano.
 
Jamani mnaozunguzia kuuvunja muungano nyinyi mlikuwepo kipindi nyerere na karume walivyoziunganisha hizo nchi mbili? Naamini kutokana na uchu wa madaraka kwa baadhi ya watu. Ukiona mambo yanazungumziwa saana ujue zaidi ni tamaa ya madaraka
Kwa taarifa yako Muungano uliosasisiwa kati ya Nyerere na Karume umeshavunjwa. Wao waliweka Muungano wa Nchi moja (Tanzania) kwa Serikali mbili {Tanzania bara (Tanganyika) serikali ya Muungano na Zanzibar serikali ya Mapinduzi}. Sasa hivi kuna Muungano wa serikali mbili kwa nchi mbili {Tanzania bara (Tanganyika) ile ya Muungano na Zanzibar serikali ya umoja wa kitaifa ambayo ina bendera yake (sina uhakika kuhusu wimbo wa Taifa). Kwa mantiki hiyo ili kuwe na usawa ndani ya Muungano serikali mbili haziepukiki.

Vinginevyo Zanzibar irudi kama awali tulipoungana (nchi moja serikali moja) na tujipange upya kimkakati wa kurekebisha kero za muungano au tuwe na serikali moja. Je hilo la mwisho linawezekana kwa hatua tuliyofifkia sasa hivi? Kama jibu ni itakuwa vigumu basi suluhisho ni serikali tatu.

Tufike sehemu tujiulize, Ni CCM haohao walioridhia Zanzibar kuwa nchi, kwa nini leo Tanganyika hawataki nayo iwe nchi? Hii sio "Double Standard"?
 
Back
Top Bottom