Hali ni mbaya sana, nazidi kudhoofika

Hali ni mbaya sana, nazidi kudhoofika

Ngoja kwanza mpaka wote tutumie akili kufikiria ndo tutajua kwamba wote tunaisoma namba
 
Hali ya sasa ya kimaisha hairidhishi hata kidogo. Kimbilio la vijana wengi lilikuwa ni viwandani ila kwa sasa hata huko viwandani kazi hakuna.

Viwanda vingi uzalishaji ni mdogo mno kiasi kwamba hata wale vibarua permanent nao hawapati nafasi ya kuingia kazini
Viwanda vingine navyo vimefungwa na haijulikani lini wataanza tena kufanya kazi.

Vile viwanda ambavyo miaka ya nyuma vilikuwa vikikimbiwa na watu kisa ugumu wa kazi navyo siku hizi hata ukienda hupati nafasi maana kumejaa

Mfano mzuri ni kiwanda cha nondo kilichopo Jeti siku hizi nafasi ni adimu mno. Viwanda vingine vibarua wazoefu hawataki kuachia nafasi wanaunga shift usiku na mchana hawataki kutoka.

Viwanda vingine hawakupokei mpaka uhonge au uwe na mtu anayekujua mf kiwanda cha Pepsi ,Jambo ,kiwanda cha kioo,serengeti nk

Viwanda vingi sana vimefungwa mf Kiwanda cha Jumbo,Murzah one.Murzah Two.

Vibarua wanakimbilia Murzah four napo kazi hakuna uzalishaji mdogo mno.

Kiwanda kingine ni kiwanda cha samaki ila napo wanachukua idadi ndogo mno haswa wale wazoefu na wanawake

Kiwanda cha rasta napo siku hizi pagumu mno.

Vijana tunakufa njaa
Kumbu kumbu zinaonesha huu uzi uliandikwa siku chacha kabla Mungu hajatenda
 
Back
Top Bottom