Hali ni mbaya sana, nazidi kudhoofika

Hali ni mbaya sana, nazidi kudhoofika

Ndo maana natafuta kazi za viwandani nipate mtaji nijiajiri japo mpaka nipate mtaji itabidi nifanye kazi si chini ya miezi sita mbaya zaidi hata huko viwandani tunapotegemea tujichange tupate mtaji napo pagumu.
Unahitaji kiasi gani cha mtaji?
 
Uza hio simu unayotumia hela utakayopata fungua genge la mboga mboga.
 
Mitano tena.. chagua magugu kazi iendelee
 
Mkuu ajira milioni 6 hukupata 🤣

Kuna miradi mingi ya Maendeleo kama Flyover, Stigler's gorge, SGR, bomba mafuta n.k huko kote ajira kibaooooo.

Anyway tuko UCHUMI WA KATI. Nchi inapaa kuzidi "URAYA" au ulikuwa mpiga deal.
Alisema milioni 8 na viwanda elfu 10 wamejenga
 
Hali ya sasa ya kimaisha haiiridhishi hata kidogo.
Kimbilio la vijana wengi lilikuwa ni viwandani ila kwa sasa hata huko viwandani kazi hakuna.

Viwanda vingi uzalishaji ni mdogo mno kiasi kwamba hata wale vibarua permanent nao hawapati nafasi ya kuingia kazini
Viwanda vingine navyo vimefungwa na haijulikani lini wataanza tena kufanya kazi.

Vile viwanda ambavyo miaka ya nyuma vilikuwa vikikimbiwa na watu kisa ugumu wa kazi navyo siku hizi hata ukienda hupati nafasi maana kumejaa

Mfano mzuri ni kiwanda cha nondo kilichopo Jeti siku hizi nafasi ni adimu mno .
Viwanda vingine vibarua wazoefu hawataki kuachia nafasi wanaunga shift usiku na mchana hawataki kutoka.

Viwanda vingine hawakupokei mpaka uhonge au uwe na mtu anayekujua mf kiwanda cha Pepsi ,Jambo ,kiwanda cha kioo,serengeti nk

Viwanda vingi sana vimefungwa mf Kiwanda cha Jumbo,Murzah one.Murzah Two.

Vibarua wanakimbilia Murzah four napo kazi hakuna uzalishaji mdogo mno.

Kiwanda kingine ni kiwanda cha samaki ila napo wanachukua idadi ndogo mno haswa wale wazoefu na wanawake

Kiwanda cha rasta napo siku hizi pagumu mno
Vijana tunakufa njaa

Awamu ya 5 iangalie jinsi ya kuokoa sector ya viwanda.
 
Hakika. Nakuelewa sana hasa kama ww ni mkaka kwa kweli huwa napata huruma sana. Maana hapo kuna ka demu unakafukuzia na unajua kabisa sound bila mpunga unaweza usieleweke. Au kama unafamilia unajua kabisa majukumu ya baba ni yapi. Dah kwangu mm nawaonea huruma sana wakaka

Sina hamu ya kuwa na mpenzi nitanyanyasika tu bure
 
Back
Top Bottom