Hali katika Baraza la Uwakilishi Zanzibar sio Shwari juu ya Muungano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali katika Baraza la Uwakilishi Zanzibar sio Shwari juu ya Muungano.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 19, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Baraza la wawakilishi lafunguka: Tusilazimishane katika muungano huu. Watanganyika wanatuhadaa
  [​IMG]

  Mwakilishi wa Uzi Ibrahim Razawanabodi.
  Amini Usiamini UAMSHO sio UAMSHO tena. yaani Licha ya Vyombo vya habari kuripoti na kupotosha kuhusu UAMSHO. Ndani ya baraza la wawakilishi ni kinyume kabisa, hakuna mwakilishi anaejaribu kulizungumizia, na hata akijaribu kuligusa ni wazi unaweza ukahisi kama analiunga MKono japo sio moja kwa moja.

  Katika hali isiyotarajiwa na wengi. Leo hii Wazanibar wametoa madai mazito kuhusu muungano unavyoendeshwa huku Lawama za wazi wazi zikilekezwa kwa Watanganyika kwamba wanawahadaa wazanzibar

  Hoja zenyewe
  1)Mh Raza: Ilikuwa ni vigelegele, makofi na hata vicheko vilitanda kila kona barazani huku Spika na Mawaziri wa SMZ wakionekana wazi kupigwa na Butwaa.
  Nini Alisema Mh Raza:

  no1:
  "Mh Spika, nina nyaraka za makubaliano kati ya Serekali ya Awamu ya 3 ya Dk Salmini na Mh Mkapa kuhusu Zanzibar kujiunga OIC. Haya sio maneno ya Mitaani, ninazo nyaraka za makubaliano, na kama serekali ya sasa wanahizaji nitawapa ambazo wenzetu walisema Tanzania itajiunga OIC kwa manufaa ya Zanzibar. Lkn wenzetu wametuhada na wanaendelea kutuhadaa. huku wao wakiwa na UBALOZI wa vertican kwa manufaa yao.

  Hi ni hadaa kubwa tunayoendelewa kufanyiwa Zanzibar, Hatukubali tena tunasema hatukubali, kwa muungano wa aina hii " makofi ukumbi mzima.

  Eti tunaambiwa kupata uanachama wa OIC ni kazi kubwa, naiomba serekali hii kazi inepe mimi, ndani ya miezi 3 Tanzania itajiunga na OIC ili tutengezewe madaraja, barabara na vyuo vikuu kama baadhi ya nchi. Zanzibar tunanjaa wao kama Watanzania bara wameshiba waache washibe

  No2:
  "Mh Spika, niliwahi kusema huko Nyuma, itafika siku vyeti vya ndoa tutakiwa tuvifate Dodoma, nikapuuzwa. sasa unaona, waziri wa nishati wa Tanzania bara leo ndio anawakilisha Wazanzibar ktk jumuia ya Afrika Mashariki huku Waziri huyo akiwa mwisho wake ni CHUMBE tu. hii ni hadaa kubwa tunayohadaiwa wazanzibar huku viongozi wetu wakiwa sio wakweli , sijui nini wanachoogopahili tunasema Tunashachoka, hatulitaki litendeke

  No3: Mh spika, miaka 48 ya Muungano hadi kuna watu ndani ya tanganyika wanatuona Zanzibar hatuna maana, leo mawaziri wanakubaliana kutatua tatizo la Muunagno, kuna watu wenye nia mbaya na Zanzibar wanazuia. Muungano kama huu haufai, huu si Muungano, huu ni ulaghai" Makofi.

  Tumechoka kutanganywa na kufanyiwa ulahai na kuzarauliwa na wenzetu tulio ungana nao,hili swala linatuma sote sio viongozi wa SMZ wala wananchi wa kawaida Zanzibar ni nchi yetu wote na inatuma kila Mzanzibar.


  Mwakilishi wa Kitope
  "Mimi naona sasa hakuhitajiki viongozi wasomi kutatua matatizo ya Muungano, tuachaguliwe sisi wasio na Elimu wenye kutoa kauli. maana ndugu zetu hawataki kutusikia.

  KWA UFUPI KILA MWAKILISHI INAOENAKANA ANAKWERA NA MUUNGANO HUU UNAVYOENDESHWA licha ya waziri Aboud kudai watu wasubiri katiba mpya. Sio CCM SIO CUF
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Jee na huyu Mutasema ni Uamsho? ikiwa Seif ni Uamsho kutokana na kusema kuhusu Muungano jee na huyu nae Kada mpevu wa ccm na aliwahi kuwa Waziri wa Michezo Zanzibar nae ni Uamsho .

  Kwani Uamsho ni Watu wa Nchi kani isio na wenyewe?
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sioni connection kati ya kuwa na ubalozi VATICAN na Znz kujiunga na OIC.
  Ivi hajui kuwa Vatican ni nchi na sio jumuia like OIC!
  Tz akumbuke kuwa haina dini!
   
 4. j

  joely JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Nimekumbuka wimbo ndoa ndoano wa msondo ngoma
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,463
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Na wanasahau Saudi Arabia ni nchi sawa na Vatican?
   
 6. s

  swrc JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yanapoelekea, majibu yake ni dhahiri.:llama:
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,132
  Trophy Points: 280
  Huu muungano uvunjwe tu, maana tunakoelekea siko..
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Naye ni Uamsho, kwani huuoni uarabu wa Oman huo?
   
 9. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kura ya maoni ndio suluhisho.
   
 10. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kula tano mkuu,

  bila kusahau IRAN, ila tofauti hapa ni Saudi Sunni, Iran Shia.
  Maoni yangu, kwa wale watanzania wanaojiaminisha kupita ufahamu kwamba wao ni wazanzibari na wana haki kuwa na nchi yao sawa, wadai haki hiyo, ila sio kwa vigezo dhaifu kama hiki cha Vatican etc.
  Bora waseme wakiwa wachache ni rahisi kupata misaada na kijitawala (hii inapiga kengele ya sera ya majimbo kichwani mwangu !!!!!!!!!).
  Ila kwa sasa nchi ni moja, na inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
  Ukweli ndio huo, japo inawauma baadhi, Pinda was RIGHT kwa hili.

  Respect !!!
   
 11. A

  Abdalla Khamis Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika hili kwanza nampongeza Mh.Raza ,na aina hii ya viongozi ndio tunayoihitaji kwa sasa, Mimi binafsi naona tatizo lililopo ni woga tu, hakuna nchi iliyonaviongozi woga kama zanzibar na sijui wanachokiogopa ninini.

  Hivi ni nani leo atathubutu kusema kuwa wazanzibari tunafaidika na muungano,namtakatuelezane kupitia hapa hapa.maana kama kuna mtu alitakiwa kujua zaidi faida za muungano alikuwa ni waziri husika na mpaka tarehe 16/6/2012, akiwa katika mkutano mkoani Morogoro katika viwanja vya kichangani aliueleza umma kuwa faida ya muungano nipamoja na watanganyika kujua kupika urojo.

  Kilichopo Zanziba ni woga tu wa viongozi basi,na wafahamu kuwa kuna leo kuna na kesho kwa Mungu.

  Aidha wanatakiwa wasome alama za nyakati.
   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mimi ni kristo mkatoliki, hivi kuna dhambi gabi Tanzania ikijiunga OIC kwani nakumbuka kuwa tayari tume mbali mbali zilitumwa huko na kugundua kuwa hakuna uabay wowote. Kuna ubaya gani akiwepo Kadhi Mkuu ka ajili ya kushughulikia mambo ya dini ya Kiislamu kama wenyee wanataka? Kwanini waingiliwe? Naomba mtu anifafanulie ubaya wa mabao haya mawili.

  kwa hakika sioni ugumu wa mambo haya na mabao ambayo CCM wanatufanyia kuban hiki na kile ili mradi tu tukose uhuru.
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kichwa cha habari hii kinaoonyesha kuwa mwandishi wa thread tayari una ajenda yako mfukoni. Kama mtu kachaguliwa kuwakilisha maoni ya wananchi anaotoa maoni na kama unavyosema anaungwa mkono na na nwawakilishi wenzie wewe unasema hali sio shwari katika barza la wawakilishi kwanini sio shwari? Yaani hali kuwa shwari ni pale wahafidhina wachache mtakapokuwa mna maintain status quo na mnaendelea kufaidi raslimali za nchi hii?
   
 14. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuendako sasa ni kubaya zaidi kuliko tulikotoka. Mengi sasa yanadhihirika ila Mwalimu alisha tuasa sana. Hivi Vatican ni jumuiya ya kikristo au maana ndugu yetu hapa kapotoka waziri mzima kaenda chaka hapa.
   
 15. doup

  doup JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Nisingependa kodi yangu nayolipa kila mwezi, na kwakununua bidhaa ikaendeshe injili wa mihadhara.
  ya kaisali apewe kaisali na ya mungu ntapeleka hukohuko kanisani.
   
 16. A

  Abdalla Khamis Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana kwanza rafiki yangu,kwanza unaposema Tanzania haina dini huu ni uongo tu uliomo ndani ya katiba,wewe unaelimu kiasi gani ya kumshinda Dr. SIVALON?,yeye aliionesha dini ya Tanzania katika kitabu chake alichokiita"THE DARK SIDE OF NYERERE LEGACY",Tokea zama za Nyerere dini ya Tanzania ni UKRISTO,Ila sikulaumu inawezekana huelewi nini maana ya dini, tafsiri zifuatazo huenda ukaona uongo wa katiba(1)"The word religion comes from Latin word "RELIGARE"which means put together"Hii ni maana ya dini kilugha,(2)Rligion reffers to an institution with recognized body of communicate wher peoples come together regarly for warshipping(3),Religion is an out ward actsor form by which men indicate theirrecognitionto the existance of God/gods having power over tghe destiny(4),Religion is a total way of the life . nadhani kwa kiasi kikubwa umefahamu maana ya dini na kwa mnasaba huu dini Tanzania ipo na ni UKRISTO.Na dini hii ya ukristo kwa Tanzania kwa mujibu wa Dr. Sivalon ni matokeo ya juhudi za Nyerere na ha ta dhulma za muungano ni matokeo ya Nyerere.Kwa upande mwengine kusema kuwa huoni connection kati ya VATICAN na OIC, pia niukosefu wa kuelewa am kuamua tu kw chuki zako kutoelewa,hoja ya msingi hapa ni Muungano na Mh.alitaka kuonesha nikwa jinsi gani Tanganyika inaihujumu Zanzibar na ndiop maana akakuletea mfano wa Zanzibar kujiunga na OIC, sio haelewi ninini VATICAN,anaelewa sana ,tatizo shule tu ndio maana hujamfahamu.Jiulize kitu kimoja inakuwaje muungano huu wa nhi mbili huru,kutaka kujiunga na asasi za kimataifa mpaka tanganyike iridhie? na mbona wao hawaishauru zanzibar katika manufaa yao?,Kwa ufahamu Zaidi soma "KWA HERI UKOLONI KWAHERI UHURU" cha Dr. Mohammed Said, THE DARK SIDE OF NYERERE LEGACY" cha MCHUNGAJI Dr.SIVALON na hata MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHYD SYKES. any complain you are welcome.THANKS. NIKO TAYARI KUKUSAIDIA KWAHILI MIMI NI MWANAFUNZI WA COMPARATIVE RELIGION, SHAHADA YA KWANZA KWA UWANJA HUU NINALO LA KUKUSAIDIA.
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyu ni Mhindi. Hujui Wahindi walikuwa wadau wakubwa katika serikali ya sultani?
   
 18. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  angalau mwana jf mwenzangu hilo umeliona maana watu wanasashau kuwa Vatican ni nchi huru kama ilivyotanzania kwa kusikia makao makuu ya Wakatoliki wao hudhani kuwa siyo nchi. Raza amefirisika kimtazamo yeye ni nambari one katika watu wanaoona Muungano un amzuia biashara zake haramu ambazo mwisho wake ni kuolewa na sultan. Raza fanya kazi usitegemee misaada toka Uarabuni baba
   
 19. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kudanganyika ni kubaya sana. Yaani kumbe mmehaidiwa kujengewa barabara na vyuo vikuu ndo maana mnataka "nchi" yenu baadae mjiunge OIC. Yaani hadi leo kuna wanaume wazima wanasima na kuongea ***** kama huu wa kujengewa madaraja na wanaume wenzao? There is nothing free in this world. Hao waarabu si kwamba wanatupenda sana hadi waje kutujengea madaraja. Wakifanya hivyo lazima kuna kitu na wao wanakitarajia kukipata kutoka zanzibar. Wenye akili tunajua wanachokitaka. Ni muhimu tutafute namna ya kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali zetu kuliko kukaa na kupiga kelele eti wanaume wengine waje kutujengea barabara kana kwamba wao huko kwao wana hela za kuchezea tu
   
 20. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,599
  Likes Received: 2,983
  Trophy Points: 280
  Katika hayo uliyoyasema, majibu yake ni kama ifuatavyo:

  -Jumuiya yoyote huendeshwa na nia na madhumuni; dhumuni mojawapo la OIC ni kuhakikisha waislam wanashika nafasi zote za juu za utawala wa nchi. Huu ni udini, katiba yetu inakataa. Mtu atashika uongozi kutokana na uwezo na maamuzi ya wananchi, na siyo dini yake.

  -Mahakama ya kadhi, hakuna mtu anayewazuia waislam kuwa na mahakama hiyo. Kinacholeta tatizo ni kutaka mahakama hiyo ianzishwe na serikali na gharama zote za uendeshaji zilipwe na serikali wakati mahakama za dini nyingine kama vile za wakatoliki zimeanzishwa na kanisa lenyewe na zinagharamiwa na kanisa lenyewe. Waislam wanaruhusiwa kuanzisha mahakama yao, kwa namna waipendayo, na wawahukumu wale watakaopenda kuitumia mahakama hiyo ila hawataruhusiwa kuwakataa wevi mikono au kuwapiga mawe wazinzi mpaka wafe. Hiyo itakuwa ni kukiuka katiba ya nchi yetu. Tukikubali mahakama hiyo ifanye kazi kwa waislam kama ilivyo huko Iran, mjue hatutakuwa na viongozi waislam kwenye serikali kwa muda mfupi sana, 90% watakuwa wameuawa ndani ya mwezi mmoja. Wakristo watabakia siyo kwa sababu labda wao siyo wazinzi bali kwa vile wao hawatahusika na hiyo sharia.
   
Loading...