Hali Ikiendelea hivi, Nitamuunga Mkono Rais Magufuli

Teuzi inatafutwa.

mkuu huyo Rais atateua wangapi?

Nilishawahi Kumkemea kipindi kile akiomba kura aliposema, wasipomchagua hata leta maendeleo,
Nikamwambia asitishe watu, awaachie uhuru watu, yeye sio Mungu, tunaweza tusimchague na bado tukaishi,

Hayo ya teuzi ni akili ya watu wajinga wanaomtegemea mtu mmoja kama wehu
 
Huwa nasoma sana mabandiko yako, haupo upande wowote na kama muandishi wa makala unafanya vizuri sana. Wale wanaotaka uponde kila siku, au wanaotaka usifu kila siku nadhani wanaumia.

Magu anazingua mengi, naamini anaharibu uchumi pia coz ni kweli kuwa purchasing power ya wengi imeshuka mno, biashara nyingi mi haziendi.

Ni kweli na hii ni kwa sababu anataka kufuta umasikini kwa kuwanyonya watu wake, huwezi kufukuza umasikini bila kujua utaupeleka wapi.

Uundwe mkakati wa kuondoa umasikini ndani ya taifa kwa kuvamia nchi zingine, iwe kiutamaduni, kijamii, kiuchumi, kisiasa au kijeshi, ila sharti nchi zingine zivamiwe.

Vinginevyo tutalipana mishahara midogo miaka nenda rudi, tutaua biashara za watu wetu miaka nenda rudi, wapewe vijana passport, wapewe mitaji, wapewe elimu ya uzalendo na kujitambua, nchi isijiwekee mipaka linapokuja suala la maendeleo.
 
Mtu yoyote anayetamani kuminywa kwa demokrasia hajapita kadhia ya kukosa demokrasia ndani ya familia na nje ya familia. Ukikutana nayo kadhia ya kukosa uhuru wa kufanya maamuzi hutatamani jambo hili liwepo .
Demokrasia ni jambo muhimu kwenye mustakabali wa maendeleo. Kama maendeleo yananihusu mimi kwanini nisishirikishwe kwenye maamuzi yake?
Kiongozi asiyependa demokrasia achie ngazi kwakuwa ameshindwa kutuongoza. Na badala yake wenye kufuata demokrasia wapewe nafasi hiyo. Tangu tuwe na mfumo wa demokrasia nchini tumeweza kupata maendeleo makubwa sana nchi nzima
Kama **ujenzi wa shule nchi nzima, maabara nchi nzima, utitiri wa benki zinazotoa mikopo nchi nzima barabara za lami kuunganisha mikoa na wilaya, ajira za kutosha kila mwaka, pembejeo mfano mbolea bure kila kijiji.
 
nchi masikini na yenye wajinga wengi ili iendeee inahitaji mabavu, uliona wapi masikinina mjinga akapewa uhuru
Masikini mjinga ni wewe labda.Yeye anayejigeuza katiba hao alioshirikiana nao kugawana majumba ya serikali ndio waliofilisi hii nchi kiasi cha kuita wengine ambao hawajala keki ya taifa wananchi wanyonge. Nchi masikini wakati miaka yote inaongozwa na majambazi wa ccm! Awanyang'anye mali walizoiba kwanza na sio kuwanyang'anya mashamba akina Sumaye kisa wamehama chama au kuvunja jengo la umma la iliyokuwa Billcanas ili kumkomoa Mbowe kwa chuki za kijinga za kisiasa ambazo haziwasaidii wanaowaita wanyonge.
 
Ungelijua namna watu wa usalama wanavyohaingaika kulinda usalama wa nchi wala usingehaika, hao wanaotekwa wengi wao wanatumika na maadui kurisk usalama wa taifa, kwa kua watu wa usalama hutekeleza majukum yao kwa siri mtu wa kawaida ni rahisi kudhani wahusika wanaonewa.
 
Mwambie tunataka Tume huru ya uchaguzi - kama Rais mzuri na mwema kwako kwa nini anachekelea uminywaji wa HAKI hasa hii ya kuchagua na kuchaguliwa - tunavyoongea muda huu Makada na wagombea wa Ubunge na Udiwani wanasota magelezani kwa kesi zisizo na dhamana - hii ni DHAMBI kubwa mno...

Yaani unamyima mtu haki yake anayostahili kikatiba, afu bado unamtocha kwa adhabu kali.... hii dhambi kubwa mno!!

Akirekebisha haya kwa 100% na kufanya siasa ni utani badaal ya uadui (Vita) basi hata mimi nitamuunga mkono.
 
Mimi ni Mkweli
Nilishasema simmpigii Kura Magufuli na sikumpigia.

Nikimsema Magufuli kuna vimtu vipuuzi vinanifuata inbox na vingine kunipigia simu vikinitisha, wengne wakinipongeza.

Ninachojaribu kusema, mimi sio mfuasi wa yeyote, sio mtumwa wa Yeyote, sina chama, dini, club ya mpira, au mfuasi wa kundi lolote. Mimi ni tu huru, nafurahishwa na yeyote akifanya vizuri, na nachukizwa na yeyote anayefanya vibaya. Hilo pekee linanifanya nijivunie
Hapo kwenye Club nakataa, labda useme sio mpenzi wa michezo yeyote.

Kitendo cha kua mpenzi wa mchezo wowote, lazima kuna kundi (club) ambayo utaiunga mkono.
 
Kazi zake ni nyingi Mkuu.

Mimi ni mwandishi wa Makala, waandishi wanajua umuhimu wa mawasiliano.

Mawasiliano ni biashara
Mawasiliano ni kazi
Mawasiliano ni Connection
Mawasiliano ni elimu
Mawasiliano na Utatuzi wa migogoro n.k

Hizo hoja zinamaelezo yake na ndio sababu ya watu wote unaowaona wakiacha mawasiliano kwenye maandishi wayaandikao.

Nafikiri nimekujibu
Kwa hiyo unaandika hpa upate ajira

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom