Hali halisi ya mimba zisizopangwa (unplanned pregnancies) na watoto wasiopangwa ikoje katika nchi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,607
46,245
Takwimu zikoje kuhusu wanawake wanaopata mimba nchini na wanaume wanaowapa mimba wanawake nchini pamoja na watoto wanaozaliwa bila kupanga?

Je, wengi humu JF na wengine nchini walizaliwa kwa wazazi wao kupanga au ilikuwa ni bahati mbaya kwa wazazi wao?

Je, wenye watoto, walipanga kuwazaa wote au baadhi yao ilikuwa ni bahati mbaya kutegwa ili waoe au kushawishiwa na ndugu jamaa na marafiki?

Ili tufikirie kuwa na mipango ya miaka 20 au 30 kuna mambo, hulka na tabia za jamii za kuzitizama kwa makini ili kuweza kufanikisha hilo.
 
Nina mtoto mmoja sikuplan kumpata ilitokea tu na nikakubali matokeo.
 
Takwimu zikoje kuhusu wanawake wanaopata mimba nchini na wanaume wanaowapa mimba wanawake nchini pamoja na watoto wanaozaliwa bila kupanga?

Je, wengi humu JF na wengine nchini walizaliwa kwa wazazi wao kupanga au ilikuwa ni bahati mbaya kwa wazazi wao?

Je, wenye watoto, walipanga kuwazaa wote au baadhi yao ilikuwa ni bahati mbaya kutegwa ili waoe au kushawishiwa na ndugu jamaa na marafiki?

Ili tufikirie kuwa na mipango ya miaka 20 au 30 kuna mambo, hulka na tabia za jamii za kuzitizama kwa makini ili kuweza kufanikisha hilo.
Wajinga hawa watakwambia chakula kipo cha kutosha acha waendelee kufyatua ,kama Yule kichwa ubuyu WA chato alivyokuwa anawadanganya
 
Kuna dada anauza karanga akalala na jamaa apate kodi lakini bahati mbaya akapata mimba na ana mtoto wa miezi 4 aisee sijwahi ona mwanamke akilia na kutia hutuma kiasi hiki.
Alisahauje mbinu za kivita wakati anajua anaenda vitani.
 
Kuna takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya abortion ni kwa watu walio kwenye ndoa au mahusiano.
 
Kiukweli kwa Tanzania hapa kwa sasa watu wengi sana wanazaa bila kupanga. Na hii ndio inaongeza idadi ya watu kwa kasi sana, na sio kuongeza tu idadi ya watu, inaongeza idadi ya masikini pia kwa sababu watu wengi wanazaliwa kwenye mazingira magumu ambayo hata kupata elimu na malezi bora wanashindwa, matokeo yake inakuja kuwawia ugumu pia kutengeneza maisha yao
 
Hili ni jambo linalopaswa kuwaamsha watunga sera wa elimu na huduma za uzazi wa mpango.
Kuna takwimu zinaonesha asilimia kubwa ya abortion ni kwa watu walio kwenye ndoa au mahusiano.
 
Waswahili wana msemo wao kwamba "Kila mtoto anakuja na sahani yake"!

Back
Top Bottom