Halafu mnasema eti tusiguse simu zao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halafu mnasema eti tusiguse simu zao!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, May 17, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Aliyeaga kwenda misa ya kwanza Kristo Mfalme akutwa akizini Send to a friend Sunday, 16 May 2010 20:09 0diggsdigg

  Daniel Mjema, Moshi

  MJI wa Moshi na vitongoji vyake, jana ulizizima baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amemuaga mumewe kuwa anakwenda misa ya kwanza kanisa la Kristo Mfalme kufumwa akifanya mapenzi na kijana mmoja mbeba mizigo.

  Tukio hilo ambalo lilivuta hisia za wananchi wengi ambao walifurika kituo kidogo cha polisi cha Kiborlon kushuhudia, lilitokea saa 1.00 asubuhi katika nyumba ya kulala wageni (inahifadhiwa) iliyoko eneo la Majengo mjini hapa.

  Habari zilizowakariri mashuhuda wa tukio hilo na baadhi ya maofisa wa polisi zilidai kuwa kilichomponza mwanamke huyo ni ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) aliotumiwa na hawara yake huyo akimtaka wakutane hiyo jana asubuhi.

  “Jana (juzi) huyo kijana mbeba mizigo hapa Kiborlon alimtumia SMS huyo mke wa mtu, lakini kumbe mume wake aliiona na kujikausha kuwa hajaiona na ndipo leo (jana) alipotoka tu mumewe alianza kumfuatilia,” kilidai chanzo hicho.

  Habari hizo zinadai kuwa baada ya mwanamke huyo kumuaga mumewe anaenda misa ya kwanza na kuondoka, mumewe alimfuatilia ambapo mke alipanda daladala maarufu kama Hiace na mumewe akakodisha Taxi.

  “Mumewe aliendelea kuifuatilia hiyo Hiace kila inaposimama kwenye kituo naye anasimama kwa mbali hadi ilipofika karibu na daraja ambapo kuna kituo yule mwanamke akashuka kuelekea kwenye nyumba ya kulala wageni ,” kimefafanua chanzo hicho.

  Huko ndiko mwanamke huyo mdogo kiumri alipokutana na mbeba mizigo huyo na kwenda moja kwa moja chumbani ambako mumewe baada ya kufika hapo na kuulizia alielekezwa namba ya chumba walichokuwa wameingia.

  Akimkariri mume wa mwanamke huyo, polisi mmoja alilidokeza Mwananchi kuwa baada ya kuona hivyo, mume wa mwanamke huyo alirudi tena hadi eneo la Kiborlon na kuchukua vijana wengine wanne wa miraba minne.

  “Walipofika pale ‘guest’ aliagiza kinywaji aina ya Konyagi na kuanza kunywa lakini walikuwa wanatazama mlango wa chumba na baada ya muda alitoka yule kijana akiwa amefuatana na mke wake,”alifafanua.

  Kutokana na mshituko alioupata baada ya kumuona mumewe, mwanamke huyo alianguka ghafla na kupoteza fahamu kwa muda na alipozinduka walichukuwa pamoja na hawara yake hadi nyumba moja iliyopo Kiborloni.

  Katika nyumba hiyo, mwanamme huyo alipatiwa kipigo cha nguvu kwa kutumia minyororo huku mwanamke akishuhudia na saa 2:40 waliwapeleka wote wawili kituo cha polisi, lakini mwanamme alikuwa ameumizwa vibaya.

  Mwananchi mmoja wa Kiborlon aliyekuwa nje ya kituo cha polisi Kiborlon pamoja na mamia ya wananchi, Charles John maarufu kama King alisema mwanamme aliyefumaniwa alikuwa ameumizwa na alikuwa akitembea kwa shida.

  Mume wa mwanamke huyo alisikika akifoka kwa hasira kituoni hapo kuwa alikuwa anataka kuachana na mwanamke huyo hapohapo kituoni, lakini polisi wakamshauri suala hilo wakalizungumze na wazazi wa pande mbili.

  Baadaye polisi walimwachia mwanamke huyo ambapo alichukuliwa na mumewe na kuingizwa kwenye Taxi na mumewe alisikika akisema anamrejesha kwa wazazi wake huko Kibosho na hana mpango wa kuishi naye tena.

  Mume wa mwanamke huyo ni mfanyabiashara wakati mkewe alikuwa akiuza duka la mabegi alilofunguliwa na mumewe katika eneo hilohilo la Kiborlon ambalo zamani lilikuwa ni maarufu kwa uuzaji wa nguo za mitumba.

  Mnamo saa 4:30 asubuhi, Mwananchi lilishuhudia gari la kituo cha polisi Majengo aina ya Toyota Landcruiser likifika kituo cha Kiborlon na kumchukua mwanamme aliyekuwa amefumaniwa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa , alipoulizwa jana alisema alikuwa hajapata taarifa hizo, lakini ofisa mmoja wa polisi alisema wameamua kuwaachia mwanamke na hawara kwa sababu fumanizi sio kosa la jinai kisheria na kwamba waliwahifadhi pale kwa muda kwa sababu za kiusalama.

  Ya Kwangu:

  Wanaume ishini na wake/wanawake zenu kwa akili. Akili ya kuambiwa (eti usichunguze vya mwenza wako), changanya na ya kwako


  Send to a friend
   
 2. Mapondela

  Mapondela JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna mtu anatakiwa kuchukua hatua mkononi. Huyu mume ana kesi ya kujibu ya kujeruhi.
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aisee Kingi, kumbe uliyekuwa unahojiwa na gazeti hili pale ni wewe?
   
 4. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Kusudio la mleta maada kuchunguza ma kutokuchunguza!

  @ Kingi; rejea majadilaino ya nyuma kuna maada kama hii tuliizungumzia kwa kirefu!
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nimeiona hiyo mada wakuu, ila tatizo langu ni hawa wadada wa humu jamvini kutetea simu zao kutoguswa. Wanaume pia hawataki simu zao ziguswe. Kwa hiyo huyo mzinzi angerudh hom bila hofu akipretend kutoka ibadani. Mi ni mkosefu ila linapokuja suala la Mungu huwa nina hofu sana. Ilikuwa ni haki kupewa kichapo
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kweli, mkuu. Nilikuwa eneo la tukio.
   
 7. a

  arasululu Senior Member

  #7
  May 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  She was my wife
   
 8. R

  Ramos JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lakini kimbelembele chake cha kushika cm ya mkewe kimemsababisha ameachana nae. Asingegusa hiyo cm wangekuwa wanaishi raha mustarehe hadi leo....
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ramos; umeoa weye?
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Nitasema hata nikiamshwa usingizini, hiizi simu ni mashokolo mageni (vitu vipya tu) na tunaiga jinsi ya kuzitumia; kwa hiyo ziwe kwenye free trade zone na wapenzi wawe huru kuzigusa wakati wowote wakipenda. Huyu mama angejua simu yake inaweza kuguswa na mume wake 24/7 asingeruhusu huyo fisadi wa ngono atume ujumbe wake wa hovyo. Wangepanga na kumalizana bila kujidai kutumia simu wakidhani ni siri. Simu ziwe huru lakini muhimu zaidi ni kwa wapenzi kutulia na kuridhika na wenzi wao. Waache kutanga tanga kama mbayuwayu!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  May 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Duuu..Habari ndio hiyo.
   
Loading...