Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,120
- 871,360
Mwanzoni kulikuwa na utaratibu mzuri kabisa! Kulikuwa na jukwaa la dini na si kila mtu aliruhusiwa kuingia huko! Hii ilisaidia kwa kiwango kikubwa kiwadhibiti hawa wapuuzi
Dini ni imani na ni jambo la kiroho lisilohitaji ithibati za kibinadamu
Dini jambo binafsi na kila mtu ana sababu zake za kuamini katika dini fulani
Dini ni njia ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu asiyeonekana kwa macho ya nyama
Dini ni tokeo la kibinadamu kutafuta asili yake, chanzo chake, uhalisia wake wa jana leo na kesho
Kama watu wasivyofanana dini haziwezi kamwe kufanana
Kama ilivyo tofauti kwenye mambo mengi dini nazo zina tofauti zake
Kama mwanadamu asivyo mkamilifu, chochote kinachozalishwa naye si kikamilifu
Haitakaa itokee dunia nzima iwe na dini moja
Wewe amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini
Elimu yako kwenye dini yako ni ya kuungaunga uliyofundishwa na wakufunzi wa kuungaunga, kutoka kwenye vitabu vilivyotokana na asili na tamaduni za wengine! Vena kukaa kimya
Bhavaghita waachie Wakrishna na ukiwa na lolote waone wao.. Maana ndio wenye msahafu wao
Biblia waachie wakristo wenyewe.. Hata kama ni malumbano waache walumbane wenyewe
Sutra waachie Mabudha maana wanaijua kuliko wewe.. Wanashinda nayo wanalala nayo
Quran vilevile.. Hakuna mjuzi wa Quran isipokuwa Muislam mwenyewe
Wenye imani zingine zikiwemo za asili na hata waabudu shetani.. Wapewe heshima yao
Kimbelenyuma kwenye imani za wengine ni ushamba, ni ujuha ni upuuzi kama upuuzi mwingine!
Huwezi kuyajua in deep ya w
Nyumba fulani kuliko wenye nyumba wenyewe!
Dini zenyewe zinazowafanya muwakashifu watu si zenyu wala hamna ufahamu za kutosha kuzijua.. Hata ukiulizwa undani wa dini yako utaishia kujibu yale uliyokaririshwa na si vinginevyo
Usitumie nguvu nyingi mpaka povu linakutoka mdomoni kutaka kuthibitisha kitu kisicho na ithibati za kisayansi
Amini unachoamini nami niache niamini ninachoamini.. Nitakuacha na mapungufu ya dini yako na ya kwangu niachie mwenyewe
Hakuna vita ya kidini iliwahi shinda.. Kinachoshinda siku zote ni ukimya