Hakuna wa kufuta historia ya CUF

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
20220327_105014.jpg
 
CUF Hakiiiiiiiiii......wachukucha wachukuchaaa huku unapandisha mabega kidogo
 
Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimemteua Hamad Masoud Hamad kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Haroub Mohamed Shamis.

Masoud ameteuliwa kushika wadhifa huo, akitokea Chama cha ACT Wazalendo alikokuwa akilalamika kuchezewa rafu katika uchaguzi aliogombea nafasi ya Mwenyekiti, ambapo Juma Haji Duni ndiye aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo.

Baraza hilo pia limewateua Kona Vuai Haji na Juma Shaaban Nkumbi kuwa wajumbe wa baraza kuu huku nafasi nyingine zilizo wazi zikipangwa kujazwa katika kikao kijacho cha baraza kuu.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 28 jijini hapa na Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa kutangaza maazimio ya ajenda 14 zilizotokana na mkutano wa baraza hilo, ikiwamo mabadiliko ya uongozi, hali ya ngumu ya maisha, vita vya Urusi na Ukraine na hali ya kisiasa.

“Baraza Kuu limemshukuru Haroub Mohamed Shamis kwa kazi kubwa aliyofanya kama Katibu Mkuu katika kipindi kigumu baada ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, hayati Khalifa Suleiman Khalifa na kukiwezesha chama hicho kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu wa 2020,” amesema Lipumba.

Azimio lingine la baraza hilo ni pampoja na kuweka kando masharti ya Ibara ya 116 kifungu kidogo cha 6 yaliyopo kwenye Katiba ya chama hicho ya mwaka 1992 Toleo la 2019, yanayozuia mwanachama mpya kugombea nafasi ya uongozi hadi atakapokuwa ametimiza miezi sita.

Baraza hilo pia limeondoa kikwazo hicho ili kuhakikisha wanachama wanaorejea ndani ya chama hicho kushiriki katika ujenzi wa chama hicho huku likitangaza kuanza kwa uchaguzi wa ndani kati ya Mei 14 mwaka huu hadi Oktoba 2023.
 
Magufuli kawafuta kibwege sana. Ni hostoria iliokwenda na CUF. Lipumba na Kambaya wamepiga hela sana.

Nawahurumia sana wazanzibar wamekua watu wakubakwa, kuuliwa na kuuzwa na MADALALI wa SIASA kina Zitto.
Ni suala la muda tu itaibuka tena kwa nguvu zaidi. Kama mpaka leo Fatwa, Islamic jihad na brotherhood bado vipo! Ni ngumu sana kushindana na philosophy ni hii ndiyo silaha ya chadema
 
CUF ndicho Chama pekee Cha Upinzani chenye itikadi.

Wazanzibar wanebugi kuingia ACT Wazalendo ya Zito Cabwe mtu mbinafsi na mbaguzi wa kiwango Cha juu sana. ACT ni kama CCM ni Chama Cha Kijamaa kinachoongozwa na mabepari na watu wenye ubinafsi na walafi.

CUF kina itikadi inayojali haki na usawa Kwa watu wote.

Wakati CUF ilipokua inapigania haki sawa wapinzani wengi na CCM waliona kama haiwahusu wao ,Leo kila Mtanzania anasema habari ya haki sawa Kwa wote.

Wazanzibari ni wakati wa kujitafakari kubaki ndani ya vyama vya kimaslahi kama CCM A na B ( ACT) au kurudi kwenye Chama walichokipigania Kwa Mali,nafsi zao na muda wao yaani CUF wakidai haki sawa Kwa wote.
Zito Hana itikadi zaidi ya Tamaa ya kutaka siku Moja kuwa Bilionea kama Mbowe na Lowasa. Bila kujua kuwa Mbowe ni mtoto wa Bilionea tangu enzi za Ukoloni . Mbowe hajatajirika Kwa sababu ya siasa zaidi ameporwa Mali zake Kwa sababu ya siasa.
Zito ana tamaa sana ya Mali. Mjamaa mnafiki ,mbinafsi na mwenye roho mbaya ya kuona wengine wanapata. Zito ni CCM Kwa tabia na matendo yake japo Kwa maneno anajiita Mpinzani.

CUF kinipange upya ili kilete ushindani wa kweli wenye kujipanbanua Kwa sera na itikadi dhidi ya CCM
 
Ni suala la muda tu itaibuka tena kwa nguvu zaidi. Kama mpaka leo Fatwa, Islamic jihad na brotherhood bado vipo! Ni ngumu sana kushindana na philosophy ni hii ndiyo silaha ya chadema

CUF imeshakufa mkuu, Viongozi na wafuasi wake wote waliobaki walijiunga na ACT, chama kimebakiwa na wasaka tonge tu
 
CUF imeshakufa mkuu, Viongozi na wafuasi wake wote waliobaki walijiunga na ACT, chama kimebakiwa na wasaka tonge tu
Soma vizuri historia ya zanzibar. Afu utajua kwamba hisbu ilikuwa au ndiyo ilikuja kuwa CUF?
 
Back
Top Bottom