Mwanakijiji,
Nadhani ipo haja kubwa ya kumhoji tena huyu Wangwe..
Zipo sehemu za kumbana tupate ukweli maanake tumeyasikia mengi sana humu ambayo yanagongana na madai ya wangwe.. Kitu kimoja tu usitake kujua maisha yake mwenyewe isipokuwa issues... madai yake!
Mkandara nawe! Naona unamkwepesha mambo yake binafsi. Lakini kama PM amemtuhumu humu kwa wizi na kughushi kwanini asiulizwe?
Huyu jamaa alisimamishwa baada ya mjadala wa taarifa ya Kamati ya Wazee kutokana na utovu wake wa nidhamu. Badala ya kujitokeza na kuzungumza hilo yeye ametoka na kusema amesimamishwa kwa kuwa alitaka ruzuku ipelekwe wilayani wakati Mbowe alikuwa hataki, akasema kuwa amesimamishwa kwa kuwa alikuwa anapiga vita ukabila kwenye masuala ya viti maalumu, duh! Ama kweli kuna watu wanajua visingizio!
Umuulize:
1. Unapinga matumizi ya Helikopta- wewe si ulikuwa mjumbe wa Baraza Kuu na uliunga mkono matumizi ya helikopta kwa maneno yako mwenyewe kabisa mwaka 2006? Iweje leo umebadilika?
2. Muulize yeye alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu 2006 wakati suala la Viti Maalum 2005 linajadiliwa. Mbona hakupinga chochote? Mkumbushe kuwa mkutano Mkuu Agosti 2006 si ulifunga huu mjadala wa viti maalumu kwa pamoja na mambo mengine kuamua kuunda Baraza la Wanawake wa CHADEMA na kulipa jukumu la kuteua viti maalum kuanzia uchaguzi wa 2010 na kuendelea? Iweje yeye asema kuna ubaguzi?
3. Muulize, amesema kuna wabunge watano wa viti maalumu wachagga, ni wakina nani hao? Akikutajia na Mama Komu na Halima muulize yeye ndiye aliyemzaa mama Komu mngazija na baadaye kumbadili kuwa mchagga? Kabila linabadilika?
4. Muulize amesema kwamba kati ya wakurugenzi 10 waCHADEMA wachagga ni wanne. Mwambie awataje hao wachagga ni wakina nani? Amesema kuwa hao wanne wachagga ni pamoja na Mnyika. Muulize toka lini Mnyika amebadili kabila kutoka Msukuma mpaka mchagga?
5. Alisema ruzuku haipelekwi wilayani. Sasa baada ya wilaya za Tarime, Temeke, wilaya zote za kigoma nk kusema kwamba zinapokea ruzuku kila mwezi ana lipi la kusema?
6. Je, anajua kuwa kukaimu kwake kumekoma Julai kwa mujibu wa katiba? Ana maoni gani kuhusu hilo?
7. Je, ni kweli kwamba yeye ni mbinafsi kama alivyosema Profesa Baregu na kwamba anazungumza lugha chafu vikaoni? Je, ni mgomvi kama Makani alivyosema kwenye Mtanzania na alitaka kumpiga Tundu Lissu kikaoni kama Lissu Mwenyewe alivyokiri kwenye gazeti la Mwanahalisi?
8. Je, ni ukweli anatumiwa na Rostam Aziz kama alivyosema PM?Ni kweli alikutana nae faragha Kempinski Hoteli? Kama hapana, ni kwanini kila kukicha waliomstari wa mbele kufanya mahojiano naye ni Mtanzania na Rai?Kuna ndoa gani kati yake na wao?
Nadhani kuna haja ya kutengeneza hapa maswali ya kutosha mwanakijiji au mwandishi wa habari mwingine kumwuliza huyu jamaa.
Asha