"Hakuna ukabila wala ubadhirifu CHADEMA"-Chacha Wangwe

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Leo nawakumbusha maneno ya Chacha Wangwe mara baada ya kuchaguliwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Alifanya mkutano na waandishi wa habari pale makao makuu ya CHADEMA ambapo pamoja na mambo mengine alisema- hakuna ukabila CHADEMA, wala hakuna matumizi mabaya ya ruzuku. Alisema pia anakubaliana na maamuzi ya kutumia helikopta. Alisema yanayosemwa kuwa amesema ni uchonganishi wa magazeti. Wakati huo tamko lake liliandikwa na magazeti ya Mtanzania, Habari leo na mengineyo. Kuna mtu anaweza kutuletea vile vipande vyake?

Sehemu ya maneno yake ilinukuliwa na Tanzania Affairs hapa:

Meanwhile CHADEMA itself was not without its problems. According to the Swahili press the leadership had to deny that there were differences within the party. Tarime MP and deputy chairperson Chacha Wangwe, told the press that there was no row within the party, and he had never accused the leadership of misuse of funds or of ethnic bias. Party Leader Freeman Mbowe said “We are as united as ever, but the pro-CCM media has been trying to smear us.” Wangwe was elected party deputy chairperson by 56 votes to 38 after a heated debate. He will hold the office for one year, and, according to the media, might then try to replace Mbowe. Some CHADEMA members were reported to consider Wangwe an ‘unguided missile’ and others baptised him ‘the Jacob Zuma of CHADEMA’ – Mtanzania

Chanzo: http://www.tzaffairs.org/?p=264

Swali la kujiuliza: Je, Chacha ameamua kuyakana maneno yake mwenyewe?
 
kaazi kweli kweli
 
That is why i dont want to be a pilitician.wakati mwingine unaweza kukubali hata jambo usilolitaka na la ovyo ila baadaye unaweza kugeuka ulichokisema..
 
Wacha Kuspin Ukweli Hajawahi Kusema Hivyo Na Hajawahi Kukana Maneno Yake Ila Chaga Group Imemuassessinate
 
Hii KALI.
Lakini safi...Ni hatua ya mwanzo!
Lakini itachukuwa kamuda kwa wananchi kumwamini tena.
Inategemea na jinsi VITA HII YA UFISADI ITAKAVYOKWENDA.
 
That is why i dont want to be a pilitician.wakati mwingine unaweza kukubali hata jambo usilolitaka na la ovyo ila baadaye unaweza kugeuka ulichokisema..

Gembe

Mi ningekuwa mwandishi wa habari ningemfuata Chacha na kumuuliza: Mbona ulikanusha kuwa CHADEMA hakuna ukabila wala ubadhirifu wa ruzuku? Kwanini leo unasema vinginevyo ndani ya kipindi kifupi? Nimsikie angesemaje!

Asha
 
Hiki kichwa cha habari hakina tofauti na ile statement ya polisi juu ya ushirikina wa Chenge;

Hakuna cha Kamera, wala ushirikina - Polisi
 
Kuhisiana na Wangwe No DOUBT ana matatizo na pengine naweza sema kuna mkono wa mtu.. I have dismissed him longtime isipokuwa tu Je, kweli kuna UKABILA!..Kama HAKUNA tupo pamoja!
Kama UPO, ni swala linalotaka maelezo na ufumbuzi..
 
Gembe

Mi ningekuwa mwandishi wa habari ningemfuata Chacha na kumuuliza: Mbona ulikanusha kuwa CHADEMA hakuna ukabila wala ubadhirifu wa ruzuku? Kwanini leo unasema vinginevyo ndani ya kipindi kifupi? Nimsikie angesemaje!

Asha

Unakumbuka kwenye gazeti nadhani lilikuwa Busara lile au Sani kulikuwa na feature moja inasema "Swali moja majibu Kem Kem"

Swali: Mheshimwa Wangwe baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu wa Chadema ulisema kuwa hujawahi kutoa madai ya ukabila na matumizi mabaya ya ruzuku na ya kuwa hayo yote ni maneno ya vyombo vya habari. Mbona leo umesikika tena TBC ukisema madai hayo hayo; unaweza kuelezea vipi msimamo wako baada ya uchaguzi?

Majibu:

- Wewe ni mkabila na nina uhakika fedha unazozipata kama ruzuku unazitumia vibaya.

- Watu waliokutuma kuniuliza swali hilo wanatoka kanda moja ya magharibi hivyo siwezi kukuamini.

- Kwa vile nataka kugombea nafasi ya Uenyekiti ndio sababu unaniuliza siyo?

- Nililazimishwa na wanachama wenzangu, walinishikilia bunduki!

- Kwani mtu kubadili msimamo ni vibaya, hata kesho naweza kugeuka tena nikiwa Mwenyekiti utaniuliza tena?

- Nadhani una wivu na mimi kama wengine walivyo na wivu.

- Ukabila nani kasema ukabila? vyombo vya habari ndivyo ambavyo vimekuwa vikinasa sauti yangu vibaya.

....
 
Aisee, we mwanaume umenichekesha kweli kweli! Sasa kwa nini usifanye nae tena mahojiano au gazeti makini kama Mwananchi lisimhoji tena kuanika uzandiki na ukigeu geu wake?

Asha
 
Mwanakijiji,
Nadhani ipo haja kubwa ya kumhoji tena huyu Wangwe..
Zipo sehemu za kumbana tupate ukweli maanake tumeyasikia mengi sana humu ambayo yanagongana na madai ya wangwe.. Kitu kimoja tu usitake kujua maisha yake mwenyewe isipokuwa issues... madai yake!
 
Mkandara nawe! Naona unamkwepesha mambo yake binafsi. Lakini kama PM amemtuhumu humu kwa wizi na kughushi kwanini asiulizwe?

Huyu jamaa alisimamishwa baada ya mjadala wa taarifa ya Kamati ya Wazee kutokana na utovu wake wa nidhamu. Badala ya kujitokeza na kuzungumza hilo yeye ametoka na kusema amesimamishwa kwa kuwa alitaka ruzuku ipelekwe wilayani wakati Mbowe alikuwa hataki, akasema kuwa amesimamishwa kwa kuwa alikuwa anapiga vita ukabila kwenye masuala ya viti maalumu, duh! Ama kweli kuna watu wanajua visingizio!

Umuulize:

1. Unapinga matumizi ya Helikopta- wewe si ulikuwa mjumbe wa Baraza Kuu na uliunga mkono matumizi ya helikopta kwa maneno yako mwenyewe kabisa mwaka 2006? Iweje leo umebadilika?

2. Muulize yeye alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu 2006 wakati suala la Viti Maalum 2005 linajadiliwa. Mbona hakupinga chochote? Mkumbushe kuwa mkutano Mkuu Agosti 2006 si ulifunga huu mjadala wa viti maalumu kwa pamoja na mambo mengine kuamua kuunda Baraza la Wanawake wa CHADEMA na kulipa jukumu la kuteua viti maalum kuanzia uchaguzi wa 2010 na kuendelea? Iweje yeye asema kuna ubaguzi?

3. Muulize, amesema kuna wabunge watano wa viti maalumu wachagga, ni wakina nani hao? Akikutajia na Mama Komu na Halima muulize yeye ndiye aliyemzaa mama Komu mngazija na baadaye kumbadili kuwa mchagga? Kabila linabadilika?

4. Muulize amesema kwamba kati ya wakurugenzi 10 waCHADEMA wachagga ni wanne. Mwambie awataje hao wachagga ni wakina nani? Amesema kuwa hao wanne wachagga ni pamoja na Mnyika. Muulize toka lini Mnyika amebadili kabila kutoka Msukuma mpaka mchagga?

5. Alisema ruzuku haipelekwi wilayani. Sasa baada ya wilaya za Tarime, Temeke, wilaya zote za kigoma nk kusema kwamba zinapokea ruzuku kila mwezi ana lipi la kusema?

6. Je, anajua kuwa kukaimu kwake kumekoma Julai kwa mujibu wa katiba? Ana maoni gani kuhusu hilo?

7. Je, ni kweli kwamba yeye ni mbinafsi kama alivyosema Profesa Baregu na kwamba anazungumza lugha chafu vikaoni? Je, ni mgomvi kama Makani alivyosema kwenye Mtanzania na alitaka kumpiga Tundu Lissu kikaoni kama Lissu Mwenyewe alivyokiri kwenye gazeti la Mwanahalisi?

8. Je, ni ukweli anatumiwa na Rostam Aziz kama alivyosema PM?Ni kweli alikutana nae faragha Kempinski Hoteli? Kama hapana, ni kwanini kila kukicha waliomstari wa mbele kufanya mahojiano naye ni Mtanzania na Rai?Kuna ndoa gani kati yake na wao?

Nadhani kuna haja ya kutengeneza hapa maswali ya kutosha mwanakijiji au mwandishi wa habari mwingine kumwuliza huyu jamaa.

Asha
 
Asha Abdala,
Hapana dada yangu, mimi siamini mpango wa character assassination kuwa ndio suluhisho.. Ukizungumzia issues wananchi watakuelewa zaidi ya kumzungumzia mtu kwani sio yeye wanayemtarajia isipokuwa chama - Chadema. Na wataanza kuamini kuna Ufitini baina ya wahusika...
Mimi naamini kabisa kwamba Wangwe is nothing kwetu akiondoka watakuja kina Wangwe wengine lakini kama Chadema kitapakwa mavi bila kujisafisha kikafa basi tumekwisha!
 
chadema si chama ni kikundi cha wahuni wachache kwa maslahi ya matumbo yao na vizazi vyao

huwatumia wananchi na viongozi wasiona mbali ili kutimiza malengo yao/.

wakiamka huanza kumtafutia sababu, kama vile ukitaka kuuua paka wewe sema mwizi basi na wengine bila ya kusubiri wanajumuika kumrushia mawe

ila mwaka huu ndio mwaka wa kufa kifo cha mende miguu juu, hizo ruzuku zisikufitinisheni 2010 tunakupumzisheni ili chama kife na kuzaliwa chama cha ukweli chenye nia ya kuleta mageuzi

mageuzi hayaletwi na wahuni na kamwe watanzania wasizaniwe hawana akili kwa kutowapa nchi wapinzani wamewajaribu 1995 kwa kuwapa viti vingi bungeni wakaona walivyofanya wakapunguza 2005 ili watazame watairekebisha wapi ndio wengine wakafanya ufisadi hadi wa kughushi wa kuwapa wasomali pasi za taifa letu tanzania

wakaona wawapunguze zaidi matokeo ndio hayo fitna na choko choko

sasa wananchi wameona kuwa wapinzani ni machelema na wanastahiki kupumzishwa tena nje ya bunge na watabakia wachache sana kwenye serikali za mitaa
 
Unakumbuka kwenye gazeti nadhani lilikuwa Busara lile au Sani kulikuwa na feature moja inasema "Swali moja majibu Kem Kem"

Swali: Mheshimwa Wangwe baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu wa Chadema ulisema kuwa hujawahi kutoa madai ya ukabila na matumizi mabaya ya ruzuku na ya kuwa hayo yote ni maneno ya vyombo vya habari. Mbona leo umesikika tena TBC ukisema madai hayo hayo; unaweza kuelezea vipi msimamo wako baada ya uchaguzi?

Majibu:

- Wewe ni mkabila na nina uhakika fedha unazozipata kama ruzuku unazitumia vibaya.

- Watu waliokutuma kuniuliza swali hilo wanatoka kanda moja ya magharibi hivyo siwezi kukuamini.

- Kwa vile nataka kugombea nafasi ya Uenyekiti ndio sababu unaniuliza siyo?

- Nililazimishwa na wanachama wenzangu, walinishikilia bunduki!

- Kwani mtu kubadili msimamo ni vibaya, hata kesho naweza kugeuka tena nikiwa Mwenyekiti utaniuliza tena?

- Nadhani una wivu na mimi kama wengine walivyo na wivu.

- Ukabila nani kasema ukabila? vyombo vya habari ndivyo ambavyo vimekuwa vikinasa sauti yangu vibaya.

....

MMJJ,
Usituchekeshe hapa. Ulikuwa na nafasi ya kumuuliza Bw. Wangwe hayo maswali na hukuyauliza, sasa unayaleta JF ili iweje wakati hayupo?

Nimesikiliza mahojiano yako yote na Lissu pamoja na ya Wangwe. Ukweli ni kuwa Wangwe ndiye aliyetoka mshindi kidedea tena kwa sana na Lissu ameonekana kama vile ametumwa kuendelea kumchomea Wangwe.

Kama unataka kufanya mahojiano ya haki, mlete Mbowe sasa tusikie na yeye anasemaje kuhusu hizo shutuma. Au kama ikiwezekana waweke wote kwa pamoja, Mbowe vs Wangwe ili baada ya hapo tuweze kujua nani ni mkweli.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom