Hakuna tusi kubwa kama uporwaji wa Rasilimali za Nchi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,565
41,082
Kumekuwa na hadithi nyingi kwa sasa, baada ya umma wa Watanzania kupaza sauti dhidi ya watawala na makuwadi wachache waliowezesha uporwaji wa bandari za Tanganyika unaofanywa na Waarabu wa Dubai.

Mara tunasikia akina Nape wanasema eti kuna watu wanatukana, wanatumia lugha kali, watu watumie lugha za kistaarabu! Kauli kama hizi ni za maajabu makubwa.

Hakuna tusi kubwa linalozidi uporwaji wa rasilimali za nchi. Uporwaji huu ni kuwafanya Watanganyika wote hawana akili za kung'amua uharamia uliofanywa kupitia uwekezaji wa kishenzi uliohalalishwa na mkataba wa kishenzi, kwa kuwatumia washenzi wachache kuubariki uporwaji huo.

Mwizi na yeyote anayeshirikiana na mwizi, anayewezesha na kulinda wizi, ni mshenzi. Hakuna jina zuri kwa watu kama hao zaidi ya hilo.

Watawala wamewatukana Watanganyika wote. Wamewafanya watanganyika ni wapumbavu wasioweza hata kutambua kuwa wanaibiwa hata pale wanapoibiwa. Watawala wamewafanya watanganyika ni wapumbavu ambao wanaweza kuwa wanaimba nyimbo za kusifu wanapoibiwa.

Yaani mtu unaibiwa, wanataka usifu. Ukimwambia anayetaka kukuibia na wanaomsaidia kuwa ninyi ni washenzi, wanasema umetukana! Anayemwita mwizi ni mshenzi ametumia maneno tu ambayo hayana maumivu, lakini aliyepora na aliyewezesha uporwaji, anawapa hasara na maumivi Watanganyika wa leo na vizazi vingi vijavyo. Kuna tusi gani linalozidi athari za uporwaji wa rasilimali za nchi?

Watu walihoji sana hekima ya Rais kumchagua DCI mtu ambaye kwa kipimo chochote kile ungeweza kumwita ni haramia. Mtu aliyewaletea mateso watanzania wengi kupitia operation za utekaji na ubambikiaji watu kesi zisizo na dhamana. Leo eti ndiye DCI. Ukitaka kumjua vizuri mtawala, kama huijui vizuri hulka yake, angalia aina ya watu anaowateua kwenye nafasi mbalimbali. Ukiona anateua wala rushwa wengi, ujue yeye ni mla rushwa zaidi yao. Ukiona anawateua watu wanaoonea raia na kuwanyima haki zao, ujue yeye ni mkandamizaji zaidi wa haki za watu hata kama mdomoni anaimba haki. Ukiona anateua watu waongo ujue yeye ni mwongo zaidi.

Tukitaka kumjua vizuri Rais wetu, tuangalie historia na hulka za DCI, IGP, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, na wateule wake wote.

Aliyesifika sana wakati wa awamu ya 5 kwa utekaji, upotezwaji wa watu na ubambikiaji watu kesi, Rais amemwona ndiye anayemfaa sana kwenye utawala wake, akampa nafasi ya kuwa DCI. Na taratibu ameanza kazi yake iliyomfanya Rais avutiwe naye.

Hatupo salama. Hakuna wa kuja kutukomboa bali ni kwa jitihada zetu wenyewe. Wengine watakuja kutusaidia lakini hawawezi kuanza wao.

Bandari za Tanganyika ni rasilimali yetu na urithi kwa wazaliwa wetu. Tutawakaribisha wageni wenye dhamira njema kwa kuangalia maslahi yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo. Kwa mkataba wa kihuni wa DP World, sote wenye akili timamu na dhamira njema, tuseme HAPANA.

Jambazi akiingia nyumbani mwako, japo ni mwizi, na nyumba na mali alizokuja kuiba ni zako, lakini katika kupambana nalo, bado linaweza kukujeruhi, na hata kukuua. Na sasa amekwishaanza kuonesha makucha yake. Watu wameanza kubambikiwa kesi, haya ya sasa ya ubambikiaji kesu na pengine mengine mabaya zaidi ni lazima yatokee, kwa sababu hata siku moja haitegemewi jambazi akufanyie ustaarabu. Ukiamua kupambana na jambazi lililomo ndani ya nyumba yako, yategemee na ujiandae kwa yote.

Uporaji ni ushetani kwa sababu mambo hayo ni sehemu ya dhuluma. Shetani ana nguvu, na anaweza kukupa ushindi wa muda mfupi, lakini kamwe hawezi kukupa ushindi wa kudumu. Lakini mwisho wa yote, Watu wa Mungu, tutashinda.
 
Hili la bandari haliwezi kuisha.
Hili sio jambo dogo.

Kiufupi mh. Rais Samia aelewe, sisi hatuna Tanzania nyingine.
Sisi kote tutakakoenda, ni wageni. Hii ndio Ardhi na miliki yetu pekee.

Si anaona jinsi wahamiaji wanavyofanywa wakienda kuzamia huko Uhispania, Italia, Ufaransa, Ureno, n.k

Si aliona Uingereza iliwaombea wahamiaji wale hifadhi nchini Rwanda?!
Samia aelewe na aheshimu Dunia ilivyo. Mgeni hata kama ni mwekezaji analetwa kwa tahadhari kubwa sana, maana na yeye anakuja kutafuta faida, ni uongo tu kusema anatuletea mafedha kibao. Aah wapi!

Sasa watanganyika wanasema, uwekezaji sawa, ila huu mkataba HAPANA.

Sasa kwa nini unalazimisha. Wewe mh. Samia si ni ndg yetu.! Sasa kwa nini utake kutumia bunduki, wkt ndg zako wamesema hii HAPANA.
 
Tusipoipigania ardhi yetu sasa, wajukuu zetu watakuja kulazimika kushika mtutu wa bunduki huku nao wakiuliwa na vikundi vya waarabu kama huko Darfur.

Mapambano yaendelee mpaka mkataba huu batili ufutwe. Kisha tupambanie kuiangamiza CCM na vibaraka wake ifikapo 2024 na 2025
 
Hili la bandari haliwezi kuisha.
Hili sio jambo dogo.

Kiufupi mh. Rais Samia aelewe, sisi hatuna Tanzania nyingine.
Sisi kote tutakakoenda, ni wageni. Hii ndio Ardhi na miliki yetu pekee.

Si anaona jinsi wahamiaji wanavyofanywa wakienda kuzamia huko Uhispania, Italia, Ufaransa, Ureno, n.k

Si aliona Uingereza iliwaombea wahamiaji wale hifadhi nchini Rwanda?!
Samia aelewe na aheshimu Dunia ilivyo. Mgeni hata kama ni mwekezaji analetwa kwa tahadhari kubwa sana, maana na yeye anakuja kutafuta faida, ni uongo tu kusema anatuletea mafedha kibao. Aah wapi!

Sasa watanganyika wanasema, uwekezaji sawa, ila huu mkataba HAPANA.

Sasa kwa nini unalazimisha. Wewe mh. Samia si ni ndg yetu.! Sasa kwa nini utake kutumia bunduki, wkt ndg zako wamesema hii HAPANA.
Mungu akubariki kwa kuona mbali,Asante sana.
 
Back
Top Bottom