Uporwaji Wa Bandari za Tanganyika, Utakumbukwa na Kila Upande

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,077
Mabadiliko yoyote yale makubwa, huchangiwa na jambo fulani lenye kuamsha hisia za watu.

Mabadiliko huko nchi za kiarabu yaliamshwa na kijana mmoja msomi aliyekuwa amekosa kazi, akaamua kujiua.

Mabadiliko huko Sudani yaliamshwa na kupanda kwa bei ya mkate.

Mabadiliko ya sheria za kuzuia ubaguzi dhidi ya mtu mweusi huko Marekani, yalichochewa na mauaji ya Martin Luther King.

Haya matukio machache hayakuwa ndiyo sababu bali yaliamsha ari dhidi ya maovu mengi yaliyokuwepo kwenye jamii.

Tanzania siyo Tofauti na mataifa mengi yenye tawala mbaya zinazolalamikiwa na wananchi.

Tuna tatizo la katiba mbaya na yenye mapungufu mengi, lakini watawala wameziba macho na masikio.

Tuna watawala na vyombo vya dola visivyofuata sheria wala katiba, hata hiyo yenye mapungufu.

Tuna watawala wanaoishi kwa anasa kubwa katikati ya umaskini mkubwa huku wakiwarundikia wananchi maskini kodi na tozo kibao ili ziwawezeshe wao watawala kuishi kwa anasa.

Tuna watawala ambao wameifanya nchi ni mali ya familia fulani tu. Hao ndio baba zao walikuwa marais, mawaziri, makatibu wakuu; na watoto wao, japo hawana sifa yoyote, nao wanapewa nafasi kubwa na nzuri za utawala ndani ya Serikali.

Kuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana wengi wa kada mbalimbali.

Haya yote, wananchi wana chuki nayo kwa kiasi kikubwa. Sasa zaidi ya hayo yote, watawala kwa kiburi kikubwa, kwa faida zao na wazao wao, wameamua kupora bandari za Tanganyika na kumpa Mwarabu! Wamelipwa nini, na wataendelea kupata nini kwa huyo Mwarabu kipindi chote DP atakapokuwa akinufaika na hizo bandari, hakuna mwenye uhakika, ila kwa contents za mkataba, ni wazi kabisa hakuna mtu mwenye akili timamu ataweza kufikiria kuwa contents zile zinaweza kukubalika na mtu mwenye akili huru.

Watawala wetu kwa miaka mingi wamekuwa na kiburi cha kuwapuuza wananchi. Hata jambo liwe baya kiasi gani, hata wananchi wapaaze sauti kiasi gani, wanapuuzwa, watawala huendelea na yale wanayoyataka wao. Ni kama watanzania wote wamezaliwa kwaajili ya kuwatumikia watawala.

Ufedhuli wote huu, unahitaji something to trigger ili wananchi waweze kusema kuwa, sasa imetosha. Je, trigger itakuwa ni uporwaji wa bandari zote za Tanganyika, au tusubiri nyingine?

Hakuna jambo lililowahi kuamsha hisia za wananchi wengi kama hili suala la uporwaji wa bandari, si mjini, si vijijini.

Vyovyote iwavyo, bandari itakumbukwa na watawala na wananchi maisha yao yote, maana hakuna udhalimu usio na mwisho.

Ili mabadiliko yatokee dhidi ya watawala ni lazima watawala wabakie na kuishi katika kiburi, sawa na Muumba alivyomruhusu Farao abakie katika kiburi, na mwishowe akapigwa na pigo kuu la kufa kwa kila mzaliwa wa kwanza katika nyumba za Wamisri, na kisha wana wa Israel wakatoka katika utumwa wa Wamisri chini ya mkono wenye nguvu wa Mungu.
 
Ndugu mbona unashupaza sana shingo? Ulikuwa mnufaika wa upigaji wa Bandarini nini?

Kuna uporwaji gani wa Bandari kutokana na IGA?

Mbona unatumia nguvu nyingi sana kulazimisha vitu ambavyo havipo?
 
Kwa jinsi ilivyo, hii italeta shida kama za IPTL. Ipo siku watakataliwa
Naona tumeshupaza shingo zetu kama vile hakuna kinachoendelea
 
Ndugu mbona unashupaza sana shingo? Ulikuwa mnufaika wa upigaji wa Bandarini nini?

Kuna uporwaji gani wa Bandari kutokana na IGA?

Mbona unatumia nguvu nyingi sana kulazimisha vitu ambavyo havipo?
Huo upigaji muulizeni JK aliyemleta hao Chicks wa Karimagi. Kama mmeamua kumzunguka JK basi semeni wazi wazi acheni kujificha kwenye IGA.
 
Nadhani hakuna haja ya ccm kujidai kuwa watanzania wengi hawataki bandari yao iende tu bila kujua Nini hatma ya huo mkataba..hivi hawaoni Katiba,na tume huru havijapigiwa kelele Kama huu mkataba? Maana yake umekataliwa.
swala la bandari hata CCM linawaumiza, walijaribu kuwaita wajumbe wa nyumba kumikumi wakawagomea
 
Bandari za Tanganyika zimeenda kama utani vile.Hili ni la kukumbukwa .Hata wajenge iwe ya kisasa nk,kama wamepewa haitusaidii chochote zaidi ya aliyepewa
 
Back
Top Bottom