Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,638
Tanzania ndo Taifa pekee hasa kwa miaka ya sasa ambapo kuanzia viongozi wake na wananchi ujidharau na kusifia mataifa mengine kwa kujipendekeza.

Wakati wa Baba wa Taifa haya mambo hayakuwepo. Hatukubembeleza mtu au Taifa. Hata Jomo Kenyatta enzi hizo alionja shubiri za Nyerere. Si mara ya kwanza Tanzania kuwa na vita ya maneno na ya kiuchumi na Kenya.

Rais Kamuzu Banda pia aliwahi onja joto ya jiwe. Nakumbuka mashuleni hadi tuliimba. "Banda wa malawi katuvalia ngozi simba, kututishia watanzania hatujali...hatujalii. Watanzania tulisimama wamoja. Banda kwa mkwara tu akafyata mkia. Lakini bado Tanzania tulibaki imara (Kwa sauti ya Msechu)

Viwanda viliendelea, tulisoma bure kuanzia chekechea au vidudu hadi chuo kikuu. Tulisafirishwa bure kwa wale wa boarding. Tulipewa daftari na kalamu shuleni. Kulikuwa pia na magari ya shule. Maduka ya serikali na mabasi ya serikali kila mkoa. Kulikuwa na viwanda mikoa mingi. Mabus ya wafanyakazi. Kulikuwa na bustani au park zilitunzwa vizuri. Watu tulienda kupumzika mandhari nzuri na familia. Miji ilipangiliwa. Barabara nyingi zilikuwa na miti pembeni. Leo hakuna kitu. Sijui vilienda wapi.

Pamoja na kiburi chetu hakuna kubembeleza. Tulifunga balozi hadi za uingereza na kukataa misaada yao. Ujerumani Mashariki nao tukawagomea. Israel na wengineo lkn bado Tanzania tulieshimika duniani.

Leo tumekuja na siasa za kubembeleza. Kujipendekeza, kusifia wengine. Leo Watanzania tunaona Wakenya kama ndo wakombozi wa uchumi wetu. Miungu wetu. Leo tunawapa rukhsa waingie mbungani kwetu. Wawe huru. Wawekeze kila sehemu. Ni vizuri. Lakini tunaijua vema Kenya? Nani alivunja umoja wa Afrika mashariki? Nani alidhurumu mali za umoja huo? Nani alitumiwa na majasusi kuvunja huo umoja?

Eti leo economic democracy yetu ni kujiona sisi wajinga ila mataifa mengine ni wajanja. Kazi yetu ni ziara za kusaini mikataba tunayopewa kusaini. Hata hatuna muda wakufikiria. Kisa hatutaki hudhi mtu.

Naomba ziara zingine watanzania tuwe tuna taarifiwa kabla ili tujue nini kinaenda fanyika na pia kama ni mikataba ijadiliwe kwanza bungeni na watanzania tuelewe.

Mtamsema sana vibaya Mwl. Nyerere lakini hatabaki kuwa mdiplomasia wa hali ya juu. Alikuwa mbabe lkn bado aliheshimika na mataifa makubwa.

Mtamsema vibaya na kumtukana Magufuli lkn nchi nyingi zilimtambua kuwa alisimama kwa masilahi mapana ya Tanzania. Hata Mkapa hakuwa na siasa za kubembeleza mataifa ya nje.

Angalia marekani, Uchina, Uingereza, Ujerumani na mataifa mengine wapi wanasera za kubembeleza na kusifia mataifa mengine. USA ilifikia sehemu kuweka vikwazo katika biashara na nchina japo USA inamtegemea China kwa biashara. Kikubwa ni kuangalia maslahi mapana ya nchi.

Eti leo tunasifia wakenya wanademokrasia zaidi ya Tanzania. Ni vizuri. Watanzania wanabaki kujidharau. Wanajiona wao si kitu. Kweli katika kukua tunaona mengi. Kujipendejeza sio kusifiwa ni kuzidi kudharaulika tu. Magufuli alikuwa mkorofi na mbabe. Lakini Tanzania iliheshimika. Hakuongea kiingereza lkn hotuba zake zilifatiliwa dunia nzima kusikia nini atasema. UN wenyewe walikubali kuwa alikuwa mtu aliependa Taifa lake na Afrika.

Korea kaskazini aijipendekezi lkn Marekani wanaogopa na kuheshimu Korea kaskazini. Duniani hapa mataifa makubwa yenye nguvu yote yalitumia ubabe.

Hata ukoloni ulifanyika kwa ubabe ili watawala wapate watakacho. Hata katika Biblia watawala hakuna alie kuwa lele mama. Hakuna alie jipendekeza na kusifia wengine.

Haya twendelee na kusifia, kubembeleza na kujipendekeza tuone hayo maendeleo. Hii awamu ya (-6<+4) imenikumbusha mbali hesabu za mlinganyo na magazijuto.

Hongera Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Nakupenda ila kuwa makini na washauri wako. Hasa huyo ambae wakati wake nchi ilimshinda. Hata alipoulizwa kwanini Tanzania ni masikini wakati ina kila kitu. Alijibu hata yeye hajui na anashangaa kwanini Tanzania ni masikini. Ulikiri mwenyewe hotuba yako ya Bungeni kuwa anakushauri sana pamoja na yule bwana aliesema ataendeleza majengo alojenga babake lakini hakashindwa akabakiza majungu tu kule kwetu minazini.

Baba yake alikuwa na aakili kubwa. Ange kuwepo kule minazini kungekuwa dubai ndogo. Tusisingizie Muungano. Tunapotezwa tu. Yule baharia aliijenga nchi yetu ya minazini wakati huo huo wa muungano. Hata Dar wakati huo haikujengwa kama baharia alivyo ijenga minazini. Leo tunabaki lalamikia muungano badala ya kujikita kuijenga nchi yetu.

Yangu macho. Twendelee kujipendekeza. Kusifia na kuona sisi hatuwezi jenga uchumi wetu isipokuwa wawekezaji. China ilikuwa sawa na Tanzania miaka ya nyuma. Leo ni Taifa kubwa. Je, walitumia sera ya kujipendekeza na kusifia wengine na kujidharau?

Wachina walifanya kazi hawakutegemea wawekezaji uchwara kama Kenya. Walisomesha vijana wao nje, wakaiba tekinolojia toka mataifa makubwa. Wakaunda tekinolojia yeo. Rushwa ikapigwa vita ni kunyongwa tu. Taifa likasimama.

Watanzani leo hatuna scholarship kwa ajili ya Watanzania pekee kama yalivyo mataifa mengine. Mfano Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia na mengineyo hasa kwenda kusoma nje. Nashangaa balozi zetu hazina ubunifu.

Viongozi wengi tulionao leo walipelekwa kusoma nje na serikali. Leo wamekuwa wabinafsi.

Tanzania tu vijana wanaakili kwenye ubunifu na sayansi. Tuwatumie hawa. Tuwajari. Nchi imebaki majungu. Nchi imekuwa siasa kila kitu. Tunajenga shortcut ya maisha.

Viongozi tuwe na maono. Maendeleo hayaji kwa kujipendekeza. Watu watapata machungu ya maisha ila baadae wataenjoy. Nchi zote upitia huko. Ndo tutaona maendeleo ya kweli.

Karibu tena Ikulu kwa remote control. Nawe waziri wa mambo ya nje ulikuwa katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje wakati wa team Msoga. Uliishia kutuletea Bush, Obama na hatukuona tija. Tulipata neti za mbu pekee.

Rais na baraza na taasisi waliishia kwenda nje. Nakuomba ubadilike. Mshauri vizuri mama. Najua anashaurika na akitulia ni kiongozi na Rais mzuri.
 
Kwanini watu mnaandika upumbavu maneno mengi hivi?

Enzi za Nyerere kuna mataifa tulikuwa hatujubaliani kwenye baadhi ya mambo lakini hayakuwahi kuwa maadui zetu.

Kwanza, Kuwa na migogoro na majirani siyo ufahari.

Pili, Kujisahihisha na kukubali jema la mwenzio siyo kujidharau wala udhaifu.

Ingekuwa ni kujidharau basi Wamarekani wangekuwa ni dhaifu sana.

Hakuna nchi inayoongoza kwa kujifanya iko chini kama Marekani. Sasa hivi ukiwasoma wamarekani mara zote wanaonesha kama nchi yako inaenda kupitwa na China au inazidiwa na China kwa baadhi ya mambo.

Una akili ndogo sana.
 
Enzi za mwalimu kulikuwa na bunge ambalo kwa sasa hatuna, mahakama ambapo kwa sasa hatuna, tumebaki na chama cha mapinduzi kwa mgongo wa dola, ndege inaandikwa hapa kazi tu? unategemea tupende taifa la hovyo kama hili? watu wanapigwa risasi mchana kweupe na kupotezwa, haya mambo enzi za mwalimu yalikuwepo? ubinafsi wa CCM umeharibu sn nchi.
 
Kwanini watu mnaandika upumbavu maneno mengi hivi?

Enzi za Nyerere kuna mataifa tulikuwa hatujubaliani kwenye baadhi ya mambo lakini hayakuwahi kuwa maadui zetu.

Kwanza, Kuwa na migogoro na majirani siyo ufahari.

Pili, Kujisahihisha na kukubali jema la mwenzio siyo kujidharau wala udhaifu.

Ingekuwa ni kujidharau basi Wamarekani wangekuwa ni dhaifu sana.

Hakuna nchi inayoongoza kwa kujifanya iko chini kama Marekani. Sasa hivi ukiwasoma wamarekani mara zote wanaonesha kama nchi yako inaenda kupitwa na China au inazidiwa na China kwa baadhi ya mambo.

Una akili ndogo sana.
Jazba ya Nini, kama ni hivyo ulivyoelewa wewe ni mzigo kabisa
 
Siku zote lazima ujifunze kwa waliotangulia. Kenya walishatangulia. Lazima tuangalie njia walizopita.

Ukiwa na jeuri kama ya Jiwe Ndio hayo ya kujiaminisha ujinga mwisho wa siku unaanza kuitumbukiza nchi kwenye shimo
Wakenya wameendelea nini ? Wana uchumi wa kati sawa nasi. Uchumi wao unatawaliwa na wachache. Ardhi inamilikiwa na wachache. Huku familia ya Kenyatta ikimiliki asilimia karibu 70 ya hyo nchi.
Nyerere hakuwa kuitetemekea. Na kunawakati alifunga mipaka. Eti Kenya wameendelea. Hujui Kenya.
 
Kenya wametangulia?
Siku zote lazima ujifunze kwa waliotangulia. Kenya walishatangulia. Lazima tuangalie njia walizopita.

Ukiwa na jeuri kama ya Jiwe Ndio hayo ya kujiaminisha ujinga mwisho wa siku unaanza kuitumbukiza nchi kwenye shimo
 
Wasukuma mna kazi Sana mwaka huu. Ndiyo basi tena Samia ndiye Rais wetu.

Yale maujinga yenu, mkiyataka nendeni Chato tumeyazika na Mwendazake
Mtu anae kimbilia kuji defend katika ukabila mara nyingi lazima ujiulize anatatizo gani. Mada yangu haijaongelea ukabila. Naheshimu makabila yote ya Tanzania kwani wazazi wangu hawatoki kabila moja pia jamaa na ndugu wameo na kuolewa makabila tofauti ya Tanzania. ebu watanzania tuache cheap politics na tujikite katika mambo yatayo leta maendeleo kwa Taifa letu. Hakuna kabila bora kuzidi jingine.
 
Naona watoto wa marehemu wakiwaya waya,wanatapa tapa mpaka sasa hawaamini kama baba yao hatunae tena na sasa Mama ndio kashikilia usukani.

Eti safari za mama tujuzwe kabla anaenda kufanya nn na mikataba anayoingia ipitiwe kwanza bungeni,Hivi SGR,uwanja wa chato,ununuzi wa ndege vilipitishwa na bunge lipi? Au wivu tu unawakereketa?
 
Kwanini watu mnaandika upumbavu maneno mengi hivi?

Enzi za Nyerere kuna mataifa tulikuwa hatujubaliani kwenye baadhi ya mambo lakini hayakuwahi kuwa maadui zetu.

Kwanza, Kuwa na migogoro na majirani siyo ufahari.

Pili, Kujisahihisha na kukubali jema la mwenzio siyo kujidharau wala udhaifu.

Ingekuwa ni kujidharau basi Wamarekani wangekuwa ni dhaifu sana.

Hakuna nchi inayoongoza kwa kujifanya iko chini kama Marekani. Sasa hivi ukiwasoma wamarekani mara zote wanaonesha kama nchi yako inaenda kupitwa na China au inazidiwa na China kwa baadhi ya mambo.

Una akili ndogo sana.
Mpumbavu ni yule anaedhani wengine ni wapumbavu. kwasababu hana muda wakutafakari jambo na kujiuliza kwa umakini. lini wakati wa Magufuli tulifunga balozi? Lini wakati wa Magufuli tuliingia vitani? leo unasahau sababu tu hujui historia. Wakati wa Nyerere tulipata uadi na nchi kadhaa. ndo maana nikataja baadhi ya hizo nchi.
Kwakua wewe ni mvivu kusoma unakurupuka kupinga bila kujua nini kimeandikwa ndani. Na hujui siasa za Marekani. Nani alikwambia Marekani inajishusha? Unaijua vema Marekani wewe? Sijaongelea tuwe na migogoro, nimeongelea hatuwezi jishusha na kujidharau. Soma mada uelewe si kusoma paragraph.
 
Back
Top Bottom