Hakuna redio inaomba sadaka kama Upendo FM

Hakuna redio inaomba sadaka kama Upendo FM

Aisee hii redio kila kipindi wanaomba sadaka, anatoka huyu mtangazaji akiingia mwingine ni kutaja namba za M-Pesa, mahubiri yao ni sadaka tu kila saa kuchangia sadaka.

Wanaanzishaje redio kwa kutegemea sadaka tu .
Kwani hiyo Sadaka unamtolea Mungu au unamtolea mwanadamu....SADAKA ni mpango wa Mungu na ipo kibiblia kabisa.

Mtu yeyote anayekusisitiza kutoa Sadaka anakukumbusha ujiwekee hazina yako mbinguni.
 
Aisee hii redio kila kipindi wanaomba sadaka, anatoka huyu mtangazaji akiingia mwingine ni kutaja namba za M-Pesa, mahubiri yao ni sadaka tu kila saa kuchangia sadaka.

Wanaanzishaje redio kwa kutegemea sadaka tu .
Ha ha ha

Kaka Redio hii ni ya kanisa, na wasikilizaji wakuu ni sisi wakristo hasa hasa waumini wa KKKT.

Tusipotoa sadaka hii Redio na TV wataendaje hewani? Mishahara yao je? Uboreshaji wa miundombinu ya matangazo je...

Lengo hasa la Redio na TV hii ni kulitangaza neno la Mungu ili lifike popote duniani kama alivyoagiza bwana wetu Yesu Kristo kwamba..Enendeni duniani kote......

Kwa hiyo hapa hakuna income nyingine yoyote zaidi ya sadaka...na sisi wakristo tunaamini kwamba ukishashiriki kulitangaza neno la Mungu kwa njia ya matoleo basi unabarikiwa na unajiwekeza hazina yako mbinguni, hapa duniani sisi tu wapita njia tu.

Kiroho, sadaka ina maana kubwa sana.
 
Ni kweli, wanaojua faida yake wanatoa kwa moyo na kwa furaha na HUDUMA wanaifurahia. Hujalazimishwa kutoa!! na hujalazimishwa kufungua steshen ya upendo radio!! Kwa nini ulalamike!!
huyo jamaa amekwama sana aise
 
Mara nyingi mada kama hizi huwa zina wachangiaji wengi kweli..mbali kabisa huwa ni kuponda tuu!

Hivi mnadhani chombo kurusha matangazo hewani ni bei ya kitoto? + leseni(kodi)?

Mambo mengine ulizeni acheni kuparamia vitu + ushabiki wa kutafuta umaarufu hapa jukwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo dar es salaam frequency ni 107.7
Ya Wapi hiyo Redio?Wengine tuko mbali huku Ipembe kya.mbuli,mnatunyima haki ya kuchangia kwa kina,JF ya wote.OK.hebu weka frikwensi hapa tusikie na site.Mtu. unaongea kama tunakuwa pamoja kusikiliza redio.hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hapo naona umewapa "hadhi" fulani!
Kusema "wanaomba sadaka" hapo unajaribu kuficha ukweli!
Hao jamaa ni wezi, ni kama wezi wengine.
Wanatumia kulaghai na kuwapumbaza watu kuwa mungu atawazidishia mara dufu!
Hawana tofauti na wale jamaa wa "Ile hela itume kwenye namba hii"

Staki shobo na mfia dini!
Sema ni sawa na forever living wananufaika wao..bora hata betting sikunmojamoja waweza mpiga KANJI
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Tutatoa Sadaka Zetu, Maana Hatulazimishwi
 
Hata hapo naona umewapa "hadhi" fulani!
Kusema "wanaomba sadaka" hapo unajaribu kuficha ukweli!
Hao jamaa ni wezi, ni kama wezi wengine.
Wanatumia kulaghai na kuwapumbaza watu kuwa mungu atawazidishia mara dufu!
Hawana tofauti na wale jamaa wa "Ile hela itume kwenye namba hii"

Staki shobo na mfia dini!
unakanyagwa wewe, kama hujui nguvu za MUNGU funga bakuli lako, au kwasababu ushajinunulia hirizi
??
 
Toa ikikupendeza,hakuna kitu cha bure kama unatenga muda wako kusikiliza radio kwanini usitoe sadaka?
Inaonekana mleta mada anapenda kitonga kwa sana.
Ila kama ni mwanaume angalia sana usije pumuliwa nyuma kwa kupenda vitu vya bure.
 
Mkuu kichwa Chako kazi yake ni kubeba nywele?Unadanganywa unakubali.Hiyo inamilikiwa na KKT DMP chini ya Malasusa.Dayosisi ya Kasikazini wana redio Sauti ya Injili mpaka Uchumi Bank ni ya kwao.Uwe Unatumia akili kidogo Basi.
mbona umehamaki hivo,kuna nani kwani?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watumishi wa Upendo Radio Mungu awabariki sana kwa kazi yenu nzuri. Msikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaowasema vibaya. Hata Yesu alisemwa vibaya! Sadaka ni utaratibu wa Mungu wa kugharimia Injili- hakuna namna Nyingine!! Mtu mmoja akikataa kutoa wako wengi zaidi watakaotoa.

hata mitume walienda kufanya kazi ikiwapo uvuvi, ushonaji maturubai n.k

hamna mahali mtu anaenda mbinguni kwa kutoa sadaka.Na sadaka siyo kupeleka tu makanisani, bali hata kuwapa maskini au wenye shida jambo ambalo makanisa yenu ya vodafasta hayasemi

mnahimiza waumini wanunue stika wabandike milangoni na kwny vyombo vyao vya moto na maji ya ai mafute viwalinde, wakt wachungaji wanalindwa na walinzi..

Ukweli ni mmoja tu, sasa hivi mnatumia makanisa kama njia ya kujipatia vipato visivyo halali. Hamuoni aibu mchungaji tangu anavaa skuna nyeupe, hadi ananunua vogue lakn bado anakamua watu maskini pengine hata mlo mmoja kwao ni shida.
 
Hawaishindi Redio Maria,wameacha kuhubili neno la Mungu wamekuwa watoza ushuru muda wote,hadi wanakela sisi waumini wao.
 
Sasa kama unamtusi Mungu gani unamtumikia na hayo matusi
unakanyagwa wewe, kama hujui nguvu za MUNGU funga bakuli lako, au kwasababu ushajinunulia hirizi
??
 
Wataanzishaje media kwa kutegemea sadaka ,kwanini wasitafute matangazo ,mbona redio zingine zinafanya vizuri kwa matangazo
Kuna baadhi ya matangazo hawawezi kuyakubali na kuyatoa kama redio zingine za mtaaani,mfano ya kamari na kubeti...wanafuata miongozo ya kidini...Hawaibi mkuu sababu kuna watu wanafaidika na hayo mafundisho na wao kwa hiari yao wapo willing kutoa.
 
Mkuu jibu kistaarabu naona shetani amekutawala hadi kwenye damu ndo maana una matusi mazito
Toa ikikupendeza,hakuna kitu cha bure kama unatenga muda wako kusikiliza radio kwanini usitoe sadaka?
Inaonekana mleta mada anapenda kitonga kwa sana.
Ila kama ni mwanaume angalia sana usije pumuliwa nyuma kwa kupenda vitu vya bure.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom