Hakuna redio inaomba sadaka kama Upendo FM

Hakuna redio inaomba sadaka kama Upendo FM

Aisee hii redio kila kipindi wanaomba sadaka ,anatoka huyu mtangazaji akiingia mwingine ni kutaja namba za mpesa ,mahubiri yao ni sadaka tu kila saa kuchangia sadaka.

Wanaanzishaje redio kwa kutegemea sadaka tu .
basi waibaidili jina waiite sadaka fm na jingle kuu iwe upendo ni sadaka. just kidding
 
sasa hizo sadaka si ndio zinatumika kulipa gharama za kurusha vipindi na kuwalipa presenters mkuu,hakuna mahubiri ya Bure kwenye Radio we toa tu
Ni kweli, wanaojua faida yake wanatoa kwa moyo na kwa furaha na HUDUMA wanaifurahia. Hujalazimishwa kutoa!! na hujalazimishwa kufungua steshen ya upendo radio!! Kwa nini ulalamike!!
 
Aisee hii redio kila kipindi wanaomba sadaka, anatoka huyu mtangazaji akiingia mwingine ni kutaja namba za M-Pesa, mahubiri yao ni sadaka tu kila saa kuchangia sadaka.

Wanaanzishaje redio kwa kutegemea sadaka tu .
kama unasikiliza na sadaka hutoi siyo vizuri, bora uskilize TBC inayoendeshwa kwa kodi yako.
 
Watumishi wa Upendo Radio Mungu awabariki sana kwa kazi yenu nzuri. Msikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaowasema vibaya. Hata Yesu alisemwa vibaya! Sadaka ni utaratibu wa Mungu wa kugharimia Injili- hakuna namna Nyingine!! Mtu mmoja akikataa kutoa wako wengi zaidi watakaotoa.
 
Aisee hii redio kila kipindi wanaomba sadaka, anatoka huyu mtangazaji akiingia mwingine ni kutaja namba za M-Pesa, mahubiri yao ni sadaka tu kila saa kuchangia sadaka.

Wanaanzishaje redio kwa kutegemea sadaka tu .
Mbona zipo na nyingine za kiisilamu na kikiristu.
 
Ya Wapi hiyo Redio?Wengine tuko mbali huku Ipembe kya.mbuli,mnatunyima haki ya kuchangia kwa kina,JF ya wote.OK.hebu weka frikwensi hapa tusikie na site.Mtu. unaongea kama tunakuwa pamoja kusikiliza redio.hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuchangia Radio sio jambo baya isipo haiendeshwi kikanisa watangazaji ni wahuni tu
Vipindi vibovu hakuna mpangilio mzuri
Matangazo ya biashara ni mengi wakati mwingine unafikiri sio radio ya injili

Upendo Radio Rekebisheni mpangilio mzima Tunachangia kusikiliza Neno la Mungu au Injili kwa kupitia Mahubiri Ibada Nyimbo. Kipindi cha salamu hakina mshiko
Ongezeni vipindi vya maombi
Matangazo ya biashara yatangazwe kwa utaratibu mzuri sio kupayuka na kuongea harakaka kama mashine za kukoboa na kusaga

Watangazaji wawe wenye upako sio wahuni tu

Radio Maria wako vizuri wanazungumza kwa upole na upendo ninyi ni kelele tuu
 
Hata hapo naona umewapa "hadhi" fulani!
Kusema "wanaomba sadaka" hapo unajaribu kuficha ukweli!
Hao jamaa ni wezi, ni kama wezi wengine.
Wanatumia kulaghai na kuwapumbaza watu kuwa mungu atawazidishia mara dufu!
Hawana tofauti na wale jamaa wa "Ile hela itume kwenye namba hii"

Staki shobo na mfia dini!
Kwa mini hautaki shobo na mfia dini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom