Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara Duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara Duniani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alexism, Oct 26, 2011.

 1. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kuangali kupitia umoja wa mataifa kama kuna nchi hii inayo jiandaa kuazimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.Nimejiuliza maswali mengi mojawapo kwanini nchi inakataa kuwa member wa UN kwa mda wote huu tangia ijipatie uhuru wake?
  Kwa kufatilia zaidi ikanibidi ni ingie Google lakini huko pia sikupata web address ata home page ya hii nchi ya Tanzania Bara.
  Nimekuja shangaa kuona kwamba Tanzania Bara inatambulia na FIFA lakini UN haitambui duh hapo ni kawaza tena.Kurudi tena Google nikitaka kuangalia nchi ya Zanzibar wakanipa kila kitu yaani home page imejaa taharifa zote za Zanzibar mfano muundo wa serikali,ramani,wizara etc.
  Je Tanzania Bara ni nchi au siyo nchi na iko bara gani kwani hamna taarifa zinazoionesha kama hili taifa lina ishi hapa Duniani.Mwenye kujua anishulishe kwa njia zozote zile.
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi kabisa.
  Tanzania bara imesajiriwa katika nyoyo za watanzania tu.
   
 3. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hapa ndipo ninapo shindwa kumwelewa j.k. Nyerere. Kuua identity yetu kupoteza utaifa wetu kwa utashi na kupenda kwake sifa.
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Sasa na wewe unavuruga mambo. Umoja ni nguvu, Marekeni ina nguvu kwa ajili ya kuunganisha majimbo. majimbo yalikubali kuua utambulisho nwake na sasa wamesimama kidedea duniani. Alikuwa na nia safi tu.
   
 5. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wewe umekurupuka kwakuchangia bila kusoma mada lasivyo uwezo wako wakuelewa utakuwa ni mdogo sana:Mtoa thread hoja yake hapa nikwamba hakuna Nchi inayoitwa"TANZANIA BARA"Je wewe unaifahamu Nchi hiyo?Na je inatambulika duniani na kama tunavyoelewa Nchi zote zilizo huru ni Members wa UN,je Tanzania Bara ni mojawapo.Swala la umoja hiyo ni issue nyingine.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hiyo nia yake safi ilipotelea wapi? Maana tunaona ni kama kiini macho tu, hakuna Tanganyika wala Tanzania Bara eti Tanzania.
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Haya maswali hata ukiwauliza hao wanaoandaa sherehe za miaka 50 ya uhuru hawatakujibu.
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Hujasoma majibu yangu ya mwanzo. Soma juu kwanza upate niliyosema juu.
  Unaanza matusi, character assassination, wewe sio muungwana. Ngoja nikuache maana siko style ya kwako. Wewe sio kundi langu.
   
 9. M

  Mwadada Senior Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni kweli ndugu, nadhani tuna Tanzania iliyotokana na muungano kati ya mataifa mawili ambayo ni Zanzibar na Tanganyika. Na baada ya muungano Tanganyika imekuwa haitajwi kabisa sijui ni kwa makusudi au la viongozi wetu watakuwa na jibu natumai. Hivyo sherehe za kuadhimisha uhuru zinazo kalibia ni za uhuru wa iliyokuwa Tanganyika na sio Tanzania bara kama inavyo nadiwa kwani haikuwepo kabla ya muungano. Kwa hili huwa na wasifu wenzetu wa zanzibari kwa kudumisha utambulisho wao. Nadhani wakati umefika wa Watanganyika kurudisha utambulisho wetu wakati huo huo tukidumisha muungano. Nadhani inapaswa tuseme tunaazimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, ambayo itapendeza sana tukifufua utambulisho wake ambao umezimishwa kwa muda mrefu sasa.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,907
  Trophy Points: 280
  Ni swali gumu kwa watawala.Sijui nani anaweza kukujibu.Maswali kama haya kipindi cha nyuma ungeitwa mhaini,kwahiyo ndo maana muungano haukujadiliwa vya kutosha.Sasa uko exposed lakini watawala bado hakuna anayejisumbua.Nadhani huo muafaka na kafu ndo basi tena.
  Muungano ni weli unahitaji marekebisho,yesa mwalimu alikuwa na nia nzuri,lakini wananchi wapewe wanachotaka.Wakitaka Tanganyika wapewe.
   
 11. T

  Tetere Enjiwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama umekosa tanzania bara hebu jaribu Tanganyika, ninivyo jua mimi ni tanzania bara au Tanganyika, just wondering why wewe hukufikiria jina Tanganyika. Vilevile jaribu tanzania visiwani, sio Zanzibar. Hata hivyo umezungumzia Zanzibar napata taabu kwanini huku zungumzia Tanganyika?
   
 12. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mie sina kundi hapa Mkuu wala sihitaji kuwepo katika kundi lako kule Magamba ndo kuna makundi nilichofanya nikukusaidia kukuelewesha hoja hapa "kuna Nchi inayoitwa Tanzania Bara"?hii ndo Hoja Mkuu hizo Bla bla za Marekani kuungana na longolongo zingine unazotuambia hapa hazirelate na thread husika,saying ua not my character helps nothing let us discuss issues.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhanani kuna haja ya somo la uraia lifundishwe siyo tu shuleni , nafkiri hata barabarani, makanisani, misikitini , kwenye baa na kote kwenye mikusanyiko ya watu. Hivi Wakati Tanganyika inaungana na Zanzibar kulikuwa na Tanzania? Chemsha ubongo wako . Nimeamini sasa kweli humu JF kuna watu si raia wa nchi hii. ukiamua kusema Tanzania bara , sema pia Tanzania visiwani na ukiamua kusema Zanzibar, kumbuka pia kulikuwa na Tanganyika. Ila kwa kuwa hakuna serikali 3 ndiyo maana mmezoea kuita Tanzania bara na Zanzibar. Upo hapo? huwezi kupata Tanzania bara kokote ukishatoka nje ya mipaka ya nchi yetu, bali utapata Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama hujaelewa basi. Tatizo humu mmekalia majungu, chuki binafsi, roho mbaya. Jifunzeni historia ya nchi yenu mbona vitini vinavyoelezea historia ya Tanzania viko vingi?
   
 14. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Learning is about inquiry mkuu naona haujaelewa hapa labda nikurudishe nyuma.Mh.Dr.Shein ni raisi wa Zanzibar au Tanzania visiwani?Kuna katiba ya Zanzibar au Tanzania visiwani?
  Umesema ukiwandani ndo unaipata TZ BARA,je ukitoka nje Zanzibar inakufa?Kwani hata siku mmoja sijawai sikia ata soma int.media wakisema Tanzania visiwani bari ni Zanzibar na TZ bara haitajwi tena.
  Ukienda nje watu wa visiwani wanajitambulisha Wazanzibar na siyo watanzania wala watanzania visiwani. Ukiwandani Zanzibar inasimama na wana kila kitu cha kuifanya Nation-state je mbona Tanzania bara unayoisema inapotea kwani haina adhi yakuwa a Nation-state like Zanzibar.
  Hakuna nchi inayoitwa Tanzania bara duniani!!
   
 15. Ng'wanambula

  Ng'wanambula Senior Member

  #15
  Oct 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35

  Hapa muanzisha mada yuko sahihi kabisa.Wana jf na watanzania tunatakiwa kuelewa yafuatayo:
  1. HAKUNA NCHI INAYOITWA TANZANIA BARA NA HAIJAWAHI KUTOKEA HAPA DUNIANI,
  2. WAKUNA BINADAMU ALIYEWAHI KUISHI KWENYE HIYO NCHI ISIYOKUWEPO,
  3. NCHI ILIYOPATA UHURU 9 DECEMBA 1961 INAITWA TANGANYIKA NA SIYO TANZANIA WALA TANZANIA BARA
  4. NYERERE HAKUUA IDENTITY YA WATU WA TANZANIA BARA MAANA HAIJAWAHI KUWEPO,LABDA SEMA ALIUA IDENTITY YA WATANGANYIKA
   
 16. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Pana watu na viatu.
  December 9, 1961 TANGANYIKA ilipata uhuru.
  January 12, 1964 ZANZIBAR ilifanya mapinduzi.
  April 24, 1964 TANGANYIKA na ZANZIBAR ziliungana na kuunda JAMHURI YA MUUNGANO WA TANGANYIKA na ZANZIBAR.
  Jina la Tanzania lilikuja baadae na ubara na uvisiwani umepamba moto mwishoni mwa miaka ya themanini tu.
   
 17. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  hawezi kuizungumzia Tanganyika kwakuwa hiyo nchi ya Tanganyika ilijibadilisha na kuitwa Tanzania. Kwahiyo imebaki historia.

  Ameamua kuzungumzia Tanzania Bara kwa kuhusisha na sherehe ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara (hawajasema Tanganyika), kwahiyo anajiuliza hiyo Tanzania Bara iko wapi?.
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Mzee, hivi kwa mfano mwaka 1970 anazaliwa mtoto (wa kike kwa mfano) na kupewa jina Maria Joseph. Then miaka 25 baadaye Maria anaolewa na Anthony Kulawa hivyo akachukuwa jina la mume wake na kuitwa Maria Kulawa. Baada ya miaka miwili Maria na Anthony Kulewa wanapata mtoto wa kiume na kumuita Jacob na hivyo kuwafanya wazazi hawa kuitwa Mama Jacob na Baba Jacob.

  Hivi kama huyu Mama Jacob (au hata Baba Jacob) akifanya birthday anatakiwa ahesabu tangu alipozaliwa na kuitwa Maria Joseph au tangu alipoolewa na kuitwa Maria Kulewa, na ahesabu tangu alipopata mtoto na kuitwa Mama Jacob? Na tukumbuke kuwa kila linapotokea badiliko kwenye jina kile cheti cha ubatizo kinabakia vile vile (Maria Joseph)

  Sasa, uhai wa Tanzania bara uhesabiwe kuanzia kuzaliwa (Maria Joseph/Uhuru 1961) au ndoa (Maria Kulewa/Jamhuri ya Muungano 1964). Na kama tutahesabu uhai wa Tanzania tofauti na tarehe ya kuzaliwa tutafanya hivyo kwa evidence ipi? Kwamba Tanganyika ilikufa - lini? ikazikwa - wapi? Na hivi ni kweli Tangayika ilikufa au ilibadilisha jina? Swali la la msingi hapa ni hili, tunasherehekea uhai nchi huru au jina?
   
 19. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  nimekuelewa ndg.

  Ardhi ni ileile, na wananchi ni walewale.

  Tatizo linalozungumzwa hapa si nchi ya Tanzania bali ni hili jina Tanzania Bara lini nchi hii ilibatizwa kutoka Tanganyika to Tanzania Bara?.

  Kwanini Zanzibar ibaki kuwa Zanzibar na Tanganyika iwe Tanzania Bara?
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,907
  Trophy Points: 280
  Mkuu mfano wako ni mzuri lakini hauendani vyema na issue hii.
  Utashangazwa vipi na watu kudai Tanganyika na huku ukiwa haushangazwi kuwa bendera ya Taifa kuabudiwa kiana?
   
Loading...