Kuna Rfiki yangu wa karibu sana zile dizaini za kutafutana kila jioni ,mimi ni mtu ambae naweza kukuambia sasa natoka na nani na kikweli moyo wake uko wapi ,hata mke wake first time anamutongoza second day akaniambia mdogo wangu nimeona mke ,akanipeleka nikamuona kiutani utani akawa anamtaja kila baada ya sentensi kilichofuata ni mimikuwa msimamizi wa harusi huyu mke wa rafiki yangu ni Mwanajeshi tena ni major na Jamaa siku ya kwanza kuonana alimkuta anawarukisha kichura wanaume pale makongo Jamaa ni jasiri balaa.
Aidha Huyu Rafiki yangu yaani niukimtaka demu hata awe na mamake nkimwambia tu broo nimeipenda hiikitu hanaga mshipa wa aibu atamfata atamleta ,kuna siku tulikamatwa na Traffic akatupiga faini Jamaa kwenda kulipa nikaona anacheklewa kushuka eti anabembeleza namba ,yaani kuna mda huwa namuangalia simmalizi ,yaani yeye hata mdada amtukane anatabasamu tu ,kuna siku aliomba namba ya rafiki wa mke wake mbele ya mkewe tukiwa pale mlimani city yaani kicheko kilinikaba nikakimbia kuchekla chooni.
Nachojiuliza kwa nyodo na pozi za huyu dada yaani hata umwmbie mambo sister atakujibu sema mambo dada (anajifanya anajua sana kiswahili) hivi kuna mnyama ashazama inbox ya dada kuomba game ya kirafiki ?Naamini huyu jamaa hizo ndo mambo zake bwege kamimi ntaishi kumuita dada.