Hakuna mwanamke ambaye si 'wife material'

ALEX_ANDER

JF-Expert Member
Jul 8, 2014
570
812
Kuna hili neno "wife material" ambalo watu wengi hutumia kama "mukhtasari" wa sifa za mwanamke ambaye mtu fulani huwa anamuona anafanana mke bora kwa namna yake.

Binafsi baada ya kujifikirisha, nimekuja kutambua kuwa kila mwanamke ni "wife material", inategemea tuu na mjenzi yaani mwanaume anataka material ya aina gani katika kujenga ndoa yake.

Kwa hiyo basi:
1.Kwa mwanaume usije ukasema mwanamke fulani sio wife material, labda kiwango chako cha uashi hakijafikia kutambua jinsi ya kutumia materials aliyonayo.

2. Kwa mwanamke, Jua kuna fundi mwenye uwezo wa kujua jinsi ya kutumia materials uliyonayo ila bado hajajifikirisha.

Ukiona hakieleweki jua kuwa materials uliyonayo yanahitaji waashi waliotumia teknolojia iliyotumika kujenga Pyramids za Egypt.
 
Kuna wanawake wamekaa ovyo ovyoo tuu sasa mtu anauziwa cream ya kubadili ngozi bado... huyo huyo anauziwa dawa ya kuungua kwa cream hapo hapo alipofika mwanzo ...unafikiri wakuoa uyo.
 
Bro hata jambazi na katili huwa anaombea mke mwema kutoka kwa muumba!
Huwezi niambia mwanamke anagongwa ngozi kupindukia hasa wale wanawake namba A Eti atokee mtu aoe!
Ila kuna usivyovijua nikueleweshe.
Kuna aina 2 za wanawake.
Kuna wako kwa ajili ya starehe tu! Huyu ukioa hata kama una roho ya kifrimason kesho unafkuza.
Kuna wako wengine wametulia tena ukifatilia histori yake hufkirii mara 2 unavuta jiko na majivu yake
 
Huo ujenzi ndio wanaume wengi wasioutaka na pia nikwambie mkuu kuna baadhi ya sisi wanawake hatujengeki na hii mara nyingi inasababishwa na aina ya malezi tuliyopatiwa kuanzia chini.

Na ndio sababu kuna kausemi kanasema samaki mkunje angali mbichi. Ni wachache wenye uwezo wa kukunjuka pasi kuvunjika kwa kubadilishwa na mwanaume eti kisa anakutaka uwe hivi. Labda kama unavile vimapungufu vya kawaida hapo sawa vinabadilishika ila kuna mengine hayabadilishiki aisee.
 
Hata maandiko yanajua kuna ,, mwanamke mpumbavu abomoaye nyumba yake mwenyewe.

Nakuna mwanamke mwema ( wife material ) kama alivyo Kapeace.
 
Huo ujenzi ndio wanaume wengi wasioutaka na pia nikwambie mkuu kuna baadhi ya sisi wanawake hatujengeki na hii mara nyingi inasababishwa na aina ya malezi tuliyopatiwa kuanzia chini.

Na ndio sababu kuna kausemi kanasema samaki mkunje angali mbichi. Ni wachache wenye uwezo wa kukunjuka pasi kuvunjika kwa kubadilishwa na mwanaume eti kisa anakutaka uwe hivi. Labda kama unavile vimapungufu vya kawaida hapo sawa vinabadilishika ila kuna mengine hayabadilishiki aisee.
Tabia nikama rangi yangozi mkuuu.

Sema nn ,,amin nakuambia ,,MTU anayekupenda siku zote yupo tayari kubadilika kwaajili yako !!.
 
Binafsi baada ya kujifikirisha, nimekuja kutambua kuwa kila mwanamke ni "wife material", inategemea tuu na mjenzi yaani mwanaume anataka material ya aina gani katika kujenga ndoa yake.
Wife material ni suala "abstract". Hatuna marking scheme katika hili.

Wenzetu wanasema "Beauty is in the eye of beholder". Uzuri upo kwa observer. Ndiyo maana mwanamke mzuri kwangu anaweza asiwe mzuri kwako. Ni suala la je, "Definition ya uzuri kwako ni ipi"?.

The same applied to this, Hakuna mwanamke asiye wife material. Asipokuwa wife material kwako, basi kwa mwenzio ni wife material..

You nailed It boss.

Asalaam..
 
Na ndio sababu kuna kausemi kanasema samaki mkunje angali mbichi. Ni wachache wenye uwezo wa kukunjuka pasi kuvunjika kwa kubadilishwa na mwanaume eti kisa anakutaka uwe hivi. Labda kama unavile vimapungufu vya kawaida hapo sawa vinabadilishika ila kuna mengine hayabadilishiki aisee.
Umetisher emmyta .

Nimekuelewa sana. Mleta mada ni mbaguzi mno, kawalenga wenye IQ kubwa tu ndiyo wamuelewe. Sie kina moderate, severe kadhalika, sidhani kama tungeambulia kitu bila maelezo yako.

Ahsante kwa kunitafunia.
 
Kuna hili neno "wife material" ambalo watu wengi hutumia kama "mukhtasari" wa sifa za mwanamke ambaye mtu fulani huwa anamuona anafanana mke bora kwa namna yake.

Binafsi baada ya kujifikirisha, nimekuja kutambua kuwa kila mwanamke ni "wife material", inategemea tuu na mjenzi yaani mwanaume anataka material ya aina gani katika kujenga ndoa yake.

Kwa hiyo basi:
1.Kwa mwanaume usije ukasema mwanamke fulani sio wife material, labda kiwango chako cha uashi hakijafikia kutambua jinsi ya kutumia materials aliyonayo.

2. Kwa mwanamke, Jua kuna fundi mwenye uwezo wa kujua jinsi ya kutumia materials uliyonayo ila bado hajajifikirisha.

Ukiona hakieleweki jua kuwa materials uliyonayo yanahitaji waashi waliotumia teknolojia iliyotumika kujenga Pyramids za Egypt.
Nilidhani umefanya research, kumbe umejifikirisha!!
 
Duuh. Shukrani sana mkuu.

Nadhani hiyo pia imekuwa sababu ya kufanya huu uzi ukasuasua.
Hongera kwa kulitambua hilo.

Tuna hulka ya kuchangia Topic pendwa ambazo utamu wake huwa ni wa muda tu. Ni mbaya sana kwa mustakabali wa siha za bongo zetu.

Ni kulemaza upeo wa kung'amua mambo pasina kufahamu kuwa madhara yake ni makubwa sana ukilinganisha na faida kiduchu zilizomo katika mada pendwa.
 
Kuna hili neno "wife material" ambalo watu wengi hutumia kama "mukhtasari" wa sifa za mwanamke ambaye mtu fulani huwa anamuona anafanana mke bora kwa namna yake.

Binafsi baada ya kujifikirisha, nimekuja kutambua kuwa kila mwanamke ni "wife material", inategemea tuu na mjenzi yaani mwanaume anataka material ya aina gani katika kujenga ndoa yake.

Kwa hiyo basi:
1.Kwa mwanaume usije ukasema mwanamke fulani sio wife material, labda kiwango chako cha uashi hakijafikia kutambua jinsi ya kutumia materials aliyonayo.

2. Kwa mwanamke, Jua kuna fundi mwenye uwezo wa kujua jinsi ya kutumia materials uliyonayo ila bado hajajifikirisha.

Ukiona hakieleweki jua kuwa materials uliyonayo yanahitaji waashi waliotumia teknolojia iliyotumika kujenga Pyramids za Egypt.
Tuanze na umri wako kwanza
 
Huo ujenzi ndio wanaume wengi wasioutaka na pia nikwambie mkuu kuna baadhi ya sisi wanawake hatujengeki na hii mara nyingi inasababishwa na aina ya malezi tuliyopatiwa kuanzia chini.

Na ndio sababu kuna kausemi kanasema samaki mkunje angali mbichi. Ni wachache wenye uwezo wa kukunjuka pasi kuvunjika kwa kubadilishwa na mwanaume eti kisa anakutaka uwe hivi. Labda kama unavile vimapungufu vya kawaida hapo sawa vinabadilishika ila kuna mengine hayabadilishiki aisee.
aisee mpendwa umenena ukweli mwingiii afu mzitooo tena mtamuuu!
 
Back
Top Bottom