Hakuna mpango wowote wa kuwanasua Watanzania na umasikini uliyotopea!

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Nilimsikiliza Rais Dkt. Samia akigusia suala la behewa zetu used akisema, zimeagizwa ili zianze kutumika kabla ya zile mpya na nzuri na zenye gharama kubwa kuja, na ambapo amesema zitakuja mwaka kesho 2023.

Swali la kujiuliza, kulikuwa na uharaka gani wa kutumia pesa zingine ambazo ninahisi hazikuwekwa hata kwenye bajeti kuagiza hizo behewa kama siyo kutapanya fedha za walalahoi?

Leo tuko mwezi December 2022 na kesho kutwa tu tayari 2023, ambapo behewa zetu zitakuja kwa mujibu wa maelezo ya Rais, tunafanya uharaka huu wa nini ili hali hata SGR yetu haijakamilika kujengwa kwake?

Ama kweli, mkipigwa umasikini saana na siku ya kupata hamtaamini kama mmepata, mtazipanya mali kana kwamba kesho haipo tena, na hii ni kwasababu mlishazoea maisha ya umasikini!

Tujiulize, tumenunua behewa za dhalula Kwa mabilioni ya fedha na ambapo mwaka kesho tu, behewa hizo hazitatumika tena, huu siyo ufujaji wa fedha kweli?

Kwa nini tusingesubiri zilizo kwenye order na ambazo ni mpya na nzuri?

Maswali ni mengi majibu ni 00!
 
Back
Top Bottom